EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,477
- 15,347
Uingereza imehalalisha kisheria ndoa za jinsia moja baada ya mswada uliopitishwa na bunge lao jana kuwa sheria kusainiwa na Malkia leo Jumatano saa tisa na dakika sita mchana kwa saa za Uingereza.
Sheria hiyo inajulikana kama Marriage (Same Sex Couples) Act 2013. Ndoa za jinsia moja zitaanza kufungishwa rasmi kuanzia katikati ya mwaka 2014.
Sheria hiyo mpya inaungwa mkono na viongozi wa vyama vyote vya siasa nchini humo akiwemo Waziri Mkuu wa sasa David Cameron. Cameron alipata upinzani mkali kutoka kwa baadhi ya wabunge wa chama chake cha Conservative.
Hata hivyo, mswada huo ulipitishwa kiulaini kabisa na kuwa sheria baada ya kuungwa mkono na wabunge wengi wa vyama vya Labour na Liberal Democrats.
Sheria hiyo inaruhusu mpaka ndoa za kidini za jinsia moja, lakini hailazimishi madhehebu ya dini kufungisha ndoa hizo ndani ya madhabahu yao. Pia makanisa, misikiti, nk hayatashtakiwa mahakamani kwa kukataa kuwafungisha ndoa watu wanaotaka kufunga ndoa ya kidini.
Church of England ni moja ya makundi ya kidini yaliyopinga ndoa za jinsia moja.