Uingereza kuzindua noti za plastiki Tanzania tuna cha kujifunza hapa

mitindo huru

JF-Expert Member
Apr 26, 2016
1,610
1,601
Benki kuu nchini uingereza imezindua noti mpya ambayo imetengenezwa kwa kutumia plastiki nyepesi inayojulikana kama polymer.

Benki hiyo imesema kuwa kwanza wataanza na majaribio kwa paundi tano kisha watafata na paundi kumi na ishirini.

Lakini uingereza sio nchi ya kwanza kutumia noti ya aina hiyo kwani pia kuna mataifa mengine zaidi ya 20 duniani wanatumia noti za plastiki, mataifa hayo ni kama Canada, Scotland, New Zealand, Australia n.k

Faida za noti hiyo ya plastiki ni
1. Ni vigumu kuifoji kutokana na namna plastiki yake ilivyo.

2. Ukisahau mfukoni wakati wa kufua haiaribiki hivyo kumsaidia mtumiaji kuepuka hasara.

3. Huipunguzia serikali gharama za kuchapisha ela kila mwaka kwani zinachukua mda mrefu kuchakaa.
 
Kapicha mkuu
1464893689566.jpg
1464893698005.jpg
1464893704170.jpg
1464893710265.jpg
1464893715137.jpg
 
Mbona hata Msumbiji tu noti zao ni bora sana, zina kiwango cha hali ya juu. Ni kama plastic laini.
 
Mbona hata Msumbiji tu noti zao ni bora sana, zina kiwango cha hali ya juu. Ni kama plastic laini.
Ni kweli ndugu hata ile kwacha ela ya zambia kabla ya hivi sasa ilikuwa kama plastiki laini ila ilikuwa ukifulia inachakaa, hii ya uingereza ni tofauti mana hata ukifua haiaribiki.
 
Hayo mambo ya ugunduzi, ufunguzi nakadhalika tuwaachie wadhungu watusaidie maana Mungu alikuja kwa ajili yao, sie hatuyawezi hayo
 
Back
Top Bottom