Uingereza kuzindua noti za plastiki

Uingereza kuzindua noti za plastiki

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,276
Benki kuu ya uingereza imetangaza kuzinduliwa kwa noti za plastiki za paundi 5.
Noti hiyo ya paundi tano itakuwa ya kwanza katika kipindi cha miaka 100 ambapo sarafu ya nchi hiyo imekuwa ikichapishwa kwenye karatasi.

Plastiki hiyo inayofahamika kwa jina halisi 'polymer' ni nyepesi na itahitaji wino maalum kutumiwa kuchapishwa pande zote mbili.

Hata hivyo uingereza sio taifa la kwanza kutumia noti za plastiki, mataifa zaidi ya 20 duniani tayari yanatumia noti zilizotengenezwa kutokana na plastiki.

Mataifa hayo ni pamoja na Scotland, Australia, New Zealand, na Canada.
Benki kuu ya uingereza inasema kuwa noti za plastiki (polymer) ni bora kuliko zinazotumika sasa za karatasi kwasababu zinadumu zaidi na pia hazichafuki.
1f49df568519d9cc4cb641a8d46e26f3.jpg
 
Sisi zetu zinachakaa baada ya siku moja
 
Sisi kwetu lini haya ya uzinduzi wa kitu chochote kipya au akili zetu zimeishia hapa.
 
waje waone 500 zetu dah kama zimechapishwa Stationary
 
Back
Top Bottom