Uimara wa CHADEMA Umethibitika kwa sakata la Slaa

Uimara wa CHADEMA Umethibitika kwa sakata la Slaa

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Baada ya Uvumi kuwa Dr Slaa kaihama CHADEMA. Kuna vitu nimejifunza na kujiridhisha kuwa CHADEMA kwa sasa ni taasisi kubwa ambayo hamna aliye juu yake.

Baada ya uvumi ule nilitarajia kuona watu wengi wakiungana na Dr Slaa kimtazamo ili angalau walioanzisha na waliotengeneza uzushi huo wapate faraja.

Lakini cha kushangaza Dr aligeuka adui namba moja wa wana CHADEMA na wapenda mabadiliko wote
Ishara zimejionyesha wazi, Kama kweli ikatokea Dr kutokukubaliana na wenzake anaisha kisiasa kabisa.

Kifupi yaliyotokea juu ya Dr na CHADEMA yamekuwa msaada na kipimo tosha kwa CDM juu ya uimara na uthabiti wa taasisi hiyo kwa sasa.
Chadema imedhiirisha ni chama cha upinzani imara Africa. Na mfano wa kuigwa east Africa.
 
hapana wengi wapo kimya bcs hawana taarifa za uhakika .subiri Dr ajitokeze hadharan utaona mgawanyiko
 
Cdm c imara kama unavyodhani, kwanza kwa kuungana na vyama vingine tuu hiyo ni sababu kuwa haina nguvu , kama haitoshi kumtegemea kada wa ccm kuwa ndio mgombea ngazi ya urais hiyo ni sababu ingine tena kudhihirisha udhaifu , sababu ya tatu ni kitendo cha kuweka sharti la kupokea kiasi cha fedha ili kuachia nafasi ya mgombea wa urais huo ni udhaifu mkubwa zaidi, kwa ujumla cdm na upinzani bado ni wachanga sana,. Na udhaifu wa kuamini kuwa wingi wa washabiki cyo ukubwa wa chama kwani kwa siasa watu hao leo wanaweza kukuunga ww na kesho wakamuunga mwingine.
 
Mwaka huu ni mwaka wa mabadiliko,hatuhitaji ujinga utakaoirudisha CCM madarakani.Hata mimi nilikuwa ninaunga mkono dr aondoke tu.Mabadiliko kwanza masharti baadaye.
 
mkuu hujui lolote huku site subiri atangaze ndyo utajua kwnye box la kura kunanini?
 
Dr. Hawezi kutuangusha. Mimi madhani atakuws kwenye ibada ya kufunga na kusali faragha.
 
hapana wengi wapo kimya bcs hawana taarifa za uhakika .subiri Dr ajitokeze hadharan utaona mgawanyiko

Dr slaa yupo cdm na ataendelea kuwapo dr slaa ninayemjua mimi sio mtu wa mawaa ni msomi na anauelewa wa kifikra anajua ni nini wananchi wanachokiihitaji sio mroho wa madaraka kama wengine wanavyowaza utu uzima dawa namtakia maisha marefu dr wa ukweli mpambanaji na mpenda haki.
 
chadema ni taasisi tena ni strong institution hata angekuwa baba wa taifa nyerere sembuse dr slaa mm nilikuwa mmoja wa wafuasi wake na nitaendelea kumuheshim bt when it comes to movement 4 change sitokubali kuwa mfwasi wa mtu anae ona chama kipo njia panda yeye ata kutoka na kukanusha kashindwa je ingekuwa wanamsema vibaya mkewe au watoto wake angekaa kimya inatakiwa afahamu ya kwamba watanzania wamemjua kupitia siasa na uwezi kufanya siasa bila ya chama kukudhamini
 
Chadema ni chama cha wana nchi dr ni mwajiriwa nguvu ya umma ndio sisi tuliyo mpa dr umarufu bila sisi dr hayupo apumzike ikiwezekana daima....

umeongea point nzuri sana mkuu. Nikweli ndani ya chama hamna aliye bora au maarufu kuliko chama.

Kama kuna mtu anazani akiondoka chadema basi chadema itakufa. Mtu huyo anajidanganya tena sana.

Chadema kwa sasa ni taasisi na sio mtu flani.

Sisi kama wanachama na makundi makubwa ya wananchi wapenzi na wapenda mabadiliko ndio tulio ushikilia uai wa chama na siyo mtu

kama dr atakua amezira basi chama kitaendelea kuwepo na kuzidi kufanya vizuri zaida katika medani za siasa,
 
Ndio Ukweli huo. Chama hiki kipo #Imara sana. Hii inawapa shida sana CCM na TISS yao
 
Ndio Ukweli huo. Chama hiki kipo #Imara sana. Hii inawapa shida sana CCM na TISS yao

We fikiri huu upepo una week na zaidi kuhusu mnyika na Dr lakini ndio kwanza mtaani na kwenye vijuwe watu wamezidi kushikamana.
Kitu ambacho kimekuwa tofauti na matarajio ya Ccm na raia Tanzania
Walitaraji ziwe zimerudishwa kadi nyingi sana lakini cha ajabu CDM wanazidi kupokea watu wa Ccm kila siku
Hawa jamaa hawana bahati kabisa ndio maana napenda kuwaita Wafuuu.!!
 
Dr slaa yupo cdm na ataendelea kuwapo dr slaa ninayemjua mimi sio mtu wa mawaa ni msomi na anauelewa wa kifikra anajua ni nini wananchi wanachokiihitaji sio mroho wa madaraka kama wengine wanavyowaza utu uzima dawa namtakia maisha marefu dr wa ukweli mpambanaji na mpenda haki.

out from your mind
 
Akiondoka atenda wapi? Cuf, NCCR, NLD etc vyote vyetu Ukawa. Kirudi CCM atakuwa msaliti. Kifipi yuko kati. Ss tunamtaka na asituletee nyodo.
 
mm pia nilimuamini Dr. Slaa kama kasusa basi kila la heri vita yetu cyo mtu vita yetu ni mfumo mmbaya wa ccm kwa hiyo yy kama anataka kuisaidia ccm sawa tu
 
Back
Top Bottom