Uimara wa CHADEMA Umethibitika kwa sakata la Slaa

Uimara wa CHADEMA Umethibitika kwa sakata la Slaa

Baada ya Uvumi kuwa Dr Slaa kaihama CHADEMA. Kuna vitu nimejifunza na kujiridhisha kuwa CHADEMA kwa sasa ni taasisi kubwa ambayo hamna aliye juu yake.

Baada ya uvumi ule nilitarajia kuona watu wengi wakiungana na Dr Slaa kimtazamo ili angalau walioanzisha na waliotengeneza uzishi huo wapate faraja.

Lakini cha kushangaza Dr aligeuka adui namba moja wa wana CHADEMA na wapenda mabadiliko wote
Ishara iliyojionyesha wazi, Kama kweli ikatokea Dr kutokukubaliana na wenzake anaisha kisiasa kabisa.

Kifupi yaliyotokea juu ya Dr na CHADEMA yamekuwa msaada na kipimo tosha kwa CDM juu ya uimara na uthabiti wa taasisi hiyo kwa sasa.
Chadema imedhiirisha ni chama cha upinzani imara Africa. Na mfano wa kuigwa east Africa.
.

kaka kupuuzwa kwa Slaa hakuifanyi cdm moja kwa moja kua chama imara, think twice the consequences, dnt look directly bt also indirectly
 
Amna ata mmoja anayejua ukweli kaaeni kmya na mfunge midomo yenu slaa kafAnyaje,,lowasa ufisadi wake nini mbona mkapa aliye uza nchi amsemi nyie ni masikin ndo sababu mnapoteza mda jf
 
CONFIRMED: Dkt. Slaa bado yupo Chadema na anaendelea na majukumu yake kama kawaida,kwani muda wa kuchukua fomu hadi unaisha na kuongezwa hakuwahi kwenda kuchukua fomu na wala hakuwahi kuzuiwa kuchukua fomu kwani zinatolewa ofisini kwake.
 
Chama imara ambacho kwa tariban miaka 20 iliyopita kimeshindwa kuandaa viongozi wenye sifa za kugombea nafasi ya uraisi na kinategemea wagombea waliokataliwa toka kwenye chama wanachokiita cha MAFISADI CCM!!
 
Mwaka huu ni mwaka wa mabadiliko,hatuhitaji ujinga utakaoirudisha CCM madarakani.Hata mimi nilikuwa ninaunga mkono dr aondoke tu.Mabadiliko kwanza masharti baadaye.

Tuko wengi tunaoafiki swala hili. Kama anataka kujiengue na aende tu kwa sababu tuko CHADEMA kwa sababu ya CHADEMA na si kwa sababu ya mtu. Mbowe, Slaa, Lema, Myika mkitaka kuondoka ondokeni tu mtuachie CHADEMA. Lakini wakae wakijua kwamba, Yote waliyoyafanya wakiwa CHADEMA yatakuwa kazi bure na hayatakumbukwa tena. Umaarufu wao wameupatia CHADEMA. Nje ya CHADEMA hawana huo umaarufu.
 
Mie nshawazoea hao....tulipo mtimua yule bwana mkubwa Mzito, waliongea weeeee,oh mmetupa jembe, sijui nini,sie tukajinyamazia wakachoka wenyewe, leo wamepata biashara nyingine PADRI, wanachonga weee, eti tumetupa jembe, kila anayetoka Chadema jembe, mtachoka wenyewe CHADEMA SIO CHAMA CHA MTU MMOJA MMOJA anyetaka aende mwana kwenda wote hao umaarufu wao umeanzia Chadema........
 
Akisusa c tunasonga maana hamna namna

Well said .Asante umenifariji sana .napendekeza hiwe kauli mbiu rasmi kwa wanachadema na wanamabadiliko wote Tanzania .wakati huu kipenzi wetu Dr Slaa yuko akitafakari .na mpaka siku ccm atunayo tena madarakani.
 
Chadema ni ss wanachama,chadema sio dr slaa
 
Dr Slaa bado yupo Imara kabisa subirini kesho atakavyotekea mkutano mkuu wa Chama sijui ccm na act na kagazeti kao raia Tanzania wataficha wapi nyuso zao.
 
mkuu hujui lolote huku site subiri atangaze ndyo utajua kwnye box la kura kunanini?

Site wapi huko kiongozi? Sisi wote huku tuko site hakuna anayeishi ndani ya keyboad. Sampling ya wanaochangia hapa kutoka SITE mbalimbali inaonyesha kama mleta mada alivyoelezea.
 
Dr Slaa hawezi kuisaidia ccm isianguke wanajichosha tu

Na kinachoonekana ni Ccm kumpumbaza Dr slaa
Kumvika ufalme wa kichama ambao kihalisia haupo
Na wao Ccm swala hili kwao ni kete muhimu ya ushindi
Baada ya wao kupasuka wanajuwa wakiingia kwenye uchaguzi Ukawa wakiwa wamoja nchi imeondoka
Wapo radhi sasa kutumia mabillion lakini Dr aendelee kupumbazika kwa faida yao
Ndio maana likitokea hilo hasira za wapenda mabadiliko na laana zitaelekezwa bila kificho kwa Dr
Na kwa hili lazima Slaa atafakari kwa kina na awasikilize wenzake na si kelele za lumumba kwa faida ya taifa
 
Kumbe ukweli mnaujua KUWA hata kuondoka kwa EL CCM hakuwezi kukiteteresha Chama.Punje ya wali kudondoka hakumalizi wali kwenye sahani.
 
Baada ya Uvumi kuwa Dr Slaa kaihama CHADEMA. Kuna vitu nimejifunza na kujiridhisha kuwa CHADEMA kwa sasa ni taasisi kubwa ambayo hamna aliye juu yake.

Baada ya uvumi ule nilitarajia kuona watu wengi wakiungana na Dr Slaa kimtazamo ili angalau walioanzisha na waliotengeneza uzushi huo wapate faraja.

Lakini cha kushangaza Dr aligeuka adui namba moja wa wana CHADEMA na wapenda mabadiliko wote
Ishara zimejionyesha wazi, Kama kweli ikatokea Dr kutokukubaliana na wenzake anaisha kisiasa kabisa.

Kifupi yaliyotokea juu ya Dr na CHADEMA yamekuwa msaada na kipimo tosha kwa CDM juu ya uimara na uthabiti wa taasisi hiyo kwa sasa.
Chadema imedhiirisha ni chama cha upinzani imara Africa. Na mfano wa kuigwa east Africa.

dr Slaa ni mtu mwenye busara na mtu anayeona mbali.
CDM ilikuwa chaguo la watanzania kwa sababu ya kupinga ufisadi , sasa mafisadi yote yametimkia CDM
CCM imebaki safi , na kwa hesabu za haraka haraka , Lowassa ni fisadi aliyetemwa kutoka CCM bahada ya chama na vyombo vya dola kumwona ni FISADI , mm nawshngaa wanaomshabikia Lowassa , hao waliomkataa ndio wenye dola , sitegemei wakabidhi nchi kwa mtu waliye mkataa . Ni aibu kulipa fisadi papa nchi
Dr Slaam ww ni mwanamme huwezi kaa meza moja na fisadi , TUMEKUEEWA
 
Cdm c imara kama unavyodhani, kwanza kwa kuungana na vyama vingine tuu hiyo ni sababu kuwa haina nguvu , kama haitoshi kumtegemea kada wa ccm kuwa ndio mgombea ngazi ya urais hiyo ni sababu ingine tena kudhihirisha udhaifu , sababu ya tatu ni kitendo cha kuweka sharti la kupokea kiasi cha fedha ili kuachia nafasi ya mgombea wa urais huo ni udhaifu mkubwa zaidi, kwa ujumla cdm na upinzani bado ni wachanga sana,. Na udhaifu wa kuamini kuwa wingi wa washabiki cyo ukubwa wa chama kwani kwa siasa watu hao leo wanaweza kukuunga ww na kesho wakamuunga mwingine.

ukubwa au udogo wa chama cha siasa upimwa kwa vigezo vipi vingine zaidi ya kutandaa kwake?
 
Back
Top Bottom