Uhusiano wa semantik na pragmatik | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhusiano wa semantik na pragmatik

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Anita Baby, May 17, 2012.

 1. Anita Baby

  Anita Baby JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 1,199
  Likes Received: 261
  Trophy Points: 180
  Msaada jaman nipen uhusiano huo.
   
 2. Fredrick Ishengoma

  Fredrick Ishengoma Verified User

  #2
  May 17, 2012
  Joined: May 6, 2012
  Messages: 80
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nielewavyo:

  Semantic inaangalia zaidi maana ya maneno na grammar kwenye sentensi bila kujali context au mazingira ya sentensi hiyo yalipotumika wakati Pragmatic yenyewe inaangalia maana ya maneno katika sentensi pamoja na mazingira ya sentensi na jinsi ilivyotumika .
  Ntatoa mfano kwenye sentensi ya kiingereza:

  Mfano: "He was so tired he could sleep for days."

  Semantically, we would need to take that sentence to mean exactly that. But, in casual conversation, the listeners and speaker might tell you that the guy was just saying he was really, really tired, and using those words to convey that meaning, instead of saying, 'he was really tired'.


  :A S-coffee:
   
 3. Omonto wa-hene

  Omonto wa-hene Senior Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 179
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Ndiyo Ainta Baby! Pamoja na msaada uliopewa na Kaka yako Ishengoma, nami ninakuongezea kwa kifupi sana. Semantiki ni tawi la Isimu ya lugha linalohusika na maana. Ukiwasoma wataalam wabobezi wa eneo hili wanaanza kwa kutoa maana ya maana ambapo wanatoa maana zipatazo 23 au zilinganazo na hizo; ilhali Pragmatiki ni tawi la Isimu Jamii linalojishughulisha zaidi na matumizi ya lugha kulingana na muktadha kama alivyoonesha Ishengoma. Ingawa amenisikisha kutokupatia mfano kwa lugha ya Kiswahili yenye ukwasi wa maneno kakimbilia kutoa kimfano alichokaririshwa huko darasani na ambacho ukikitazama kindakindaki utabaini kuwa kiko 'too mechanical'!!!! Nadhani alitaka akuoneshe 'nshomile bwana'!!!!!!!
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  mambo ya tataki haya sitaki hata kuyaona,,,kamuulize prof YUNUS LUBANZA
   
 5. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2012
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Naomba na mimi nijaribu kuchangia. Sijui muuliza swali alitaka tofauti ya maana au matumizi. Nakubaliana na waliochangia ila nataka nitoe angle ya matumizi.

  Mara nyingi utasikia mtu akisema hizo ni 'semantic' hapa anamaanisha kinachogombewa sii cha tofauti sana ni suala tu la kucheza na maneno au kutheorize.

  Pia utasikia watu wakisema jaribu kuwa pragmatic katika jambo hili ...
  hapa akimaanisha jaribu kutoa nafasi kwa kuzingatia manufaa halisi yanayoweza kupatikana katika hili jambo na siyo nadharia- kwa maneno mengine kuwa practical oriented katika hili

  sijui kama imesaidia wadau
   
 6. Omonto wa-hene

  Omonto wa-hene Senior Member

  #6
  May 21, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 179
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Sungura Mpole inawezekana utakuwa umesaidia kiasi fulani katika mchango wa ufafanuzi ulioutoa. Ila tu mi nimekereka namna ulivyojitahidi kuwa chotara katika mchango wako. Sina hakina kama 'uswa-kinge' ulioutumia hapa utawasaidia sana wanajamvi wenzetu ambao lugha hiyo haipandi. Ningekusifu sana kama ungeamua kubadili msimbo kabisa na uwasilishe mchango wako kwa Kiingereza kuliko ulivyoamua kuchanganya msimbo. Ninaamini wakati mwingine utachangia kwa kuwafikiria hata na wanajamvi wengine.

  Ninawasilisha!!!
   
 7. k

  kajuka JF-Expert Member

  #7
  Nov 2, 2013
  Joined: May 9, 2013
  Messages: 387
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  elimu nzuri sana.
   
 8. k

  klf Member

  #8
  Nov 5, 2013
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwa Kiswahili mbona hutumika "semantics" = umbomaana (sarufimaana)
  Pragmatics = sijui lakini "pragmatist = myakinifu, wa-
   
 9. K

  Kashindye Samadali New Member

  #9
  Feb 3, 2017
  Joined: Jan 25, 2017
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Napata mkanganyiko watu wanatumia sana kiingereza kuliko kiswahili hivyo kufanyaje wangine tushindwe kuelewa Mimi ninavyojua hata ni matawi ya isimu ambayo yanashughulika Na maana za mofimu hapo semantiki inahusu maana za mofimu katika tungo Na pragmatiki maana za mofimu kulingana Na muktadha kikubwa zipo sababu nyingi za kuhusiana huko bila kwa Leo namba niishie hapa maana wino wa kalamu yangu umeniishia Nawasilisha kwa wasomaji husika.
   
 10. CONSTRUCTIVE THOUGHT

  CONSTRUCTIVE THOUGHT JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2017
  Joined: Jul 10, 2015
  Messages: 1,167
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Umeombwa kutoa uhusiano, wewe unatofautisha!
   
 11. CONSTRUCTIVE THOUGHT

  CONSTRUCTIVE THOUGHT JF-Expert Member

  #11
  Feb 14, 2017
  Joined: Jul 10, 2015
  Messages: 1,167
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Umejaribu vizuri, hebu njoo tena na maboresho unaweza patia.
   
 12. Mr Q

  Mr Q JF-Expert Member

  #12
  Feb 14, 2017
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 6,056
  Likes Received: 7,079
  Trophy Points: 280
  Ukielewa utofauti wake vizuri basi kujua uhusiano linaweza lisiwe jambo gumu kwako

  Na hata hivyo ukiwa unaelezea uhusiano wa kitu basi kutofautisha hakuepukiki.
  Ahsante
   
 13. CONSTRUCTIVE THOUGHT

  CONSTRUCTIVE THOUGHT JF-Expert Member

  #13
  Feb 14, 2017
  Joined: Jul 10, 2015
  Messages: 1,167
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Naona unataka ku-violet quantity of maxims.
   
Loading...