Basi Nenda
JF-Expert Member
- Jul 29, 2017
- 20,789
- 47,984
Wakuu habarini za muda huu,
Zimeanzishwa thread nyingi kuhusu Franco na Mobutu, historia ya Mobutu imeelezwa na ya Franco pia, leo naleta historia ya uhusiano wa watu hawa wenye majina makubwa Africa na ulimwenguni, mwanasiasa na gwiji la muziki.
KUNYONGWA KWA KINA EVARISTE KIMBA
Mnamo mwaka 1965 Mobutu anakua rais wa Zaire na kuagiza kunyongwa kwa watu zaidi ya 6 wengi wao wakiwa mawaziri wa serikali aliyoipindua katika eneo la matonge jijini Leopold Ville (Kinshasa) kwa kosa la uhaini, mamilioni ya watu wanashuhudia hadharani, mmoja wao ni Franco, baada ya hapo Franco akatunga nyimbo iitwayo Luvumbu Ndoki (Luvumbu mchawi) hii ni hadithi ya kikongo kuhusu Mfalme Luvumbu aliyeuwa ndugu zake wa karibu kwa ajili ya kujinufaisha.
Nyimbo hii inaonekana na mamlaka kama dhihaka kwa mobutu kutokana na kitendo chake cha kunyonga mawazili wale Franco anakamatwa na kuachiwa alafu anakimbilia Brazaville kwa miezi 6 mpaka pale mambo yalipokuwa shwari.
AUNTHENTICATION POLICY (Zairenisation)
Mnamo mwaka 1971 mobutu anabadili jina la Congo kuwa Zaire, sarafu kua Zaire, pamoja na miji kuitwa majina ya kiafrika, Leopoldville inakua Kinshasa, Elizabeth Ville inakua Kisangani na kadhalika, kutokana na sera ya uafrika mpaka majina ya watu yanabadilishwa.
Bendi ya Franco, Tp Ok jazz inaandamana na mobutu nchi nzima kueneza sera ya mobutu na kutoa album iitwayo belela unthenticite na congress ya mpira.
MALIPO YA KAZI
Mobutu anampa Franco eneo la ardhi pale Kinshasa, Franco anajenga night club iliyoitwa un Deux trois, pia Mobutu baada ya kubinafsisha kampuni za kigeni anampa Franco kampuni ya muziki iitwayo mazadi.
JACKY NA HELEINE(nyimbo za Franco)
Franco añatoa nyimbo mbili Jacky na heleine ambazo serikali iliziona hazina maadili na kumpa Franco kifungo cha miezi 6 jela, na bar yake kufungwa miezi 2, alivobisha kua hazina maadili mama yake alisikilizishwa, yote haya yalifanywa na Kengo wa Dondo aliyekua attorney general.
Mobutu anamtoa jela Franco baada ya week 3 na kumshusha cheo Kengo wa Dondo kua balozi wa Zaire nchini Ubelgiji, Franco anaimba nyimbo ya kumponda Kengo iitwayo trailleur (anasema fundi nguo akikinyanganya sindano utawachomaje watu? Yaani kengo kaporwa madaraka na Mobutu)
Franco anaimba lettre a mr le directeur general (barua kwa director general) nyimbo ambayo añawaponda viongozi wa serikali kwa rushwa na usimamizi mbovu, hii inachukuliwa na wengi kama diss song kwa Mobutu.
Mwka 1984 anaimba nyimbo ya kumsifu Mobutu iliyoitwa Candida na biso, wakati wa uchaguzi ambapo watu walitakiwa kujibu ndio au apana kama wanamtaka Mobutu, hakukua na wapinzani.
Mobutu alifadhili band nyingi kubwa za muziki nchini Zaire, ikiwemo TP OK JAZZ
KIFO CHA FRANCO
Franco anafariki jijini Ubelgiji mwka 1989, Mobutu akiwa Ufaransa ziarani,
Mobutu anatangaza siku 4 za maombolezo na radio zote kupiga nyimbo za Franco tu, mwili wa Franco unapelekwa Palais du people kuagwa
Mobutu aliporudi aliitembelea familia ya Franco pamoja na kaburi.
Kwa kiasi kikubwa Mobutu alimtumia Franco katika ku mobilize watu kwenye siasa zake na pia Franco alinufaika sana kwa kuendesha magari ya kifahari kama mercedes benz na kuishi vizuri, kuliko wanamuziki wengi wa Congo na nje ya Congo

,mkuu ,franco alipendwa sana na wazee enzi hizo,