Simba zee 33
JF-Expert Member
- Sep 15, 2020
- 1,374
- 1,558
Habari wakuu,
Kwa kweli mafahali wanapopigana nyasi huumia.
Ni ukweli usiojificha Tanzania na Kenya Hatuna uhusiano mzuri wa kidiplomasia na unazidi kutetereka.
Athari zake tunazipata Sisi wananchi haswa Wakulima wa mpunga na mahindi.
Wakuu, tujue kila magunia matatu ya mpunga au mahindi mawili yalikua yanaenda Kenya.
Kwa sasa Wakenya wananunua Mahindi kule Mexico na mchele Vietnam sasa, nani anaumia?
Matunda yanaozea shambani kuanzia mananasi, maembe, matunda damu nk
Baada ya Tanzania kuharibu uhusiano na wafanyabiashara wenye asili ya India mpaka mazao kama:
Korosho
Mbaazi
Dengu
Ufuta, n.k
Kukosa bei kabisa sasa ni zamu yetu walima mahindi na mpunga. Leo hii mazao sio tu ni bei rahisi Bali pia hata mnunuzi hakuna.
Je, Jakaya alitabiri kweli kwa kusema uhusiano wetu na Kenya hautatetereka labda tupate kiongozi mjinga. Mpumbavu tena wa ajabu?
Akasema watu wa aina hio ni wachache, je ni wachache au ni mmoja tu?
Naandika kwa uchungu sana maana roho inaniuma.