Abdalah Abdulrahman
JF-Expert Member
- Aug 29, 2019
- 222
- 201
Hivi karibuni kumetokea uvumi katika mitandao ya kijamii kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya ugonjwa wa corona na Teknolojia ya 5G.Miongoni mwa hoja zinazotolewa ni kama zifuatazo:-
1. Kuwa karibu na 5G kuna sababisha corona, ndio maana nchi zilizo athirika zaidi ni zile zilizoanza kutumia teknolojia hii.
2. Teknolojia ya 5G inatoa miaonzi ambayo inasababisha kansa, na kuharibu kabisa vinasaba (DNA) vya binadamu.
3. Kuna dhana kuwa Corona imeanza China kutokana na China kuwa ya kwanza kujenga minara ipatayo 100,000 kwa ajili ya 5G.
4. Ipo dhana kuwa kinga dhidi ya corona itakuwa na kipandikizi cha kielekroniki (micro chip) kitakachopandikizwa kwenye mwili wa binadamu kuzuia athari za 5G. Ndio maana Bill Gate anadhamini utengenezaji wa dawa na kinga ili zisambazwe kwenye nchi maskini kwa malengo ya kiusalama.
Dhana zote hizi ni uongo, na ukweli kuhusu mfumo wa mawasiliano wa 5G ni unapatikana katika sayansi ya mionzi pamoja na ile ya mawasiliano kama ifuatavyo:-
Mfumo wa 5G kama ilivyo mifumo mingine kabla yake, mfano 2G, 3G, na 4G ambao mpaka sasa hivi unatumia/kusafiri kwa njia ya mawimbi ya redio (radio waves) ambayo ni aina moja wapo ya mionzi isiyo ainishi (non ionizing radiation) kama ilivyo katika spectra ya mionzi (electromagnetic spectrum).Mfano wa mionzi iliyo katika kundi hili la mionzi isiyo ainishi ni ile inayotumika katika microwave, ile ya jua (ultraviolet) nk.
Mionzi ainishi ambayo inaweza kuleta madhara kwenye mwili wa binadamu ni ile ya x-ray, alpha, betta, gamma ray na neutron na ile ya ultra-violet light ambayo ipo mwisho wa spectra ya mionzi (electromagnetic spectrum). Mionzi inayotokana na 5G haipo katika kundi hili.
Kwa kuwa mionzi inayotokana na 5G sio ainishi, ni wazi kuwa mionzi hii haiwezi kusababisha madhara ya cancer, kubadili kinasaba au kusababisha matatizo ya mifumo ya kupumua au yanayofana na hayo ndani ya mwili wa binadamu.
Madhara yanayoweza kupatikana katika teknolojia ya 5G ni kama yale yanayoweza kupatikana katika teknolojia ya 2G, 3G, na 4G, ambayo pia yanaweza kupatikana katika microwaves, ultraviolet ambayo ni kuongeza joto la seli.
Mfano ukiongea na simu kwa muda mrefu unapata maumivu kwani seli za sehemu za sikio ni laini. Vivyo hivyo tunashauriwa kutopakata laptop ili joto linaloongezeka kutokana na kupakata laptop lisiathiri sehemu za uzazi ambazo seli zake ni laini na ni rahisi kuathiriwa na joto.
Binafsi ninaweza kutoa mjumuisho ufuatao katika hili:-
Moja kuna upotoshaji unaofanyika kwa makusudi au kwa kutokujua kuhusu mionzi na corona, upotoshaji huu unaweza kuwa na madhara ya kiafya kwa watu kutokuchukua tahadhari stahiki kwa ugonjwa huu wa corona na kuongeza hofu ambayo haipo.
Pili, upotoshaji huu unalenga pia kujipatia kipato kwa wale wanaotafuta idadi kubwa ya watu wanaosoma makala zao katika mitandao ya kijamii.
Tatu, upotoshaji huu unaweza kuwa unafanywa na mataifa makubwa kama Marekani na washirika wake ambayo yanahofu na China kwenye Teknolojia ya 5G.
Vile vile upotoshaji huu unaweza kuwa na athari za kuhofia Teknolojia ya 5G ambayo ndio dunia inapoelekea na hivyo kuwabakisha watu nyuma.