Uhuru wa wachunguzi huru

Uhuru wa wachunguzi huru

Wenzetu hawako kama unavyofikiria, wanajali ukweli wa kazi yao na sio anayewalipa, na hii ndiyo sifa inayowatambulisha na kufanya kazi yao iheshimike na kukubalika dunia nzima.
 
Tokea Mh. Lissu anusurike kwenye shambulio dhidi ya uhai wake siku ashara na kitu zilizopita, kumekuwepo na sauti kadhaa zinazodai au zinazotaka tukio hilo lichunguzwe na wachunguzi 'huru' kutoka nje ya nchi.

Sababu yake kubwa ni kwamba vyombo vya ndani [ya nchi] vya usalama haviko huru kuweza kufanya uchunguzi huo kwa sababu vyenyewe ndivyo vinavyoshukiwa kupanga na kutekeleza jaribio hilo ili kutimiza matakwa ya mtu au watu wa huko serikalini na kwenye CCM.

Hisia hizo [za kuishuku na kuituhumu] nazielewa. Hivyo watu wanaotaka kuona wachunguzi huru wakichunguza nao nawaelewa.

Ila, kuna vitu vinanitatiza kidogo kuhusu huo u huru wa hao wachunguzi na utayari wa kambi ya Lissu na kambi ya serikali kuyakubali matokeo ya huo uchunguzi wao endapo utatokea.

La kwanza, ni nani atayeingia gharama za hao wachunguzi?

Tuseme CHADEMA na wafadhili wao ndiyo wataingia hizo gharama.

Kama hivyo ndo itavyokuwa, je, hao wachunguzi watakuwa huru kiasi gani ilhali wanalipwa na upande wa mnusurika wa jaribio?

CHADEMA kweli inaweza kuwalipa hao wachunguzi huru halafu hao wachunguzi watoe uchunguzi ambao ni kinyume na madai ya CHADEMA [kwamba serikali kupitia vyombo vyake vya usalama ndiye mhusika]? Kama wataletwa na CHADEMA maana yake ni kwamba wao ni waajiriwa wa hicho chama. Akili yangu haioni ni jinsi gani hao wachunguzi huru wanaweza kutoa matokeo yaliyo kinyume na hisia za watu waliowaajiri.

Je, serikali nayo ipo tayari kweli kuyakubali matokeo ya hao wachunguzi huru ambao huenda wakalipwa na hicho chama pinzani?

Na vipi kwa mfano serikali ikubali ujio wa hao wachunguzi na iingie gharama kwa kazi watayoifanya, je, CHADEMA ipo tayari kuyapokea na kuyakubali matokeo ya huo uchunguzi hata kama yakiwa tofauti na vile wao wadhaniavyo?

Kumbuka, kama serikali ndiyo itayoingia gharama za hao watu maana yake ni kwamba watakuwa wanaitumikia serikali iliyopo madarakani ambayo ni ya CCM.

Kwa mtaji huo hao wachunguzi huru watakuwa wapo huru kiasi gani?

Hili suala ni gumu kwa kweli. Kila ninapowaza na kuwazua sipati majibu.

Sijui nyie wadau mnalionaje hilo suala.

Jumapili njema.

Nimeongea na FBI wamecheka sana halafu wakauliza nchini kwenu mnazungumza lugha gani. Nilipojibu kiswahili ndio wakaona ni kituko suala la uchunguzi wa hivi kufanywa na FBI.

Ila walisema wao wanafanya kazi za taifa la Marekani. Huenda nje inapotokea ishu kama ya ubalozi wao kupigwa. Na ni brainer wapelelezi wao wanashirikiana na polisi, jeshi na wapelelezi wa nchi husika. Usitegemee wafike uwanja wa fisi kwenda kuhoji watuhumiwa.

Na hilo la gharama kuna zaidi ya gharama. Vifaa na miundo mbinu. Hivi polisi wanafukuzaje gari ya watuhumiwa kwenye foleni ya magari ya bongo

https://www.fbi.gov/about/leadership-and-structure/international-operations

The Role of the Legal Attaché
The FBI legal attaché works with the law enforcement and security agencies in their host country to coordinate investigations of interest to both countries. The role of legal attachés is primarily one of coordination, AS THEY DO NOT CONDUCT FOREIGN INTELLIGENCE GATHERING OR COUNTERINTELLIGENCE INVESTIGATIONS. The rules for joint activities and information sharing are generally spelled out in formal agreements between the U.S. and the host nation.

Typical duties of a legal attaché include coordinating requests for FBI or host country assistance overseas; conducting investigations in coordination with the host government; sharing investigative leads and information; briefing embassy counterparts from other agencies, including law enforcement agencies, as appropriate, and ambassadors; managing country clearances; providing situation reports concerning cultural protocol; assessing political and security climates; and coordinating victim and humanitarian assistance.


WANAOTAKA FBI WAJE BE CAREFUL WHAT YOU WISH.
 
Ukirudia kusoma hiki ulichoandika nadhani hutaamini macho yako. Sijui una umri gani lakini nikukumbushe tukio la kulipuliwa ubalozi wa Marikani hapa Dar. Ni FBI ndio walikuja nchini kufanya upelelezi na hata kugundua ni nani walihusika. Sijui kama unakumbuka mauaji ya Padri kule Zanzibar? Kikwete aliruhusu wapelelezi kutoka nje waje wasaidie kufichua wahusika wa mauaji yale. Kwa hiyo mjomba uhuru wa nchi hauuzwi kwa kuruhusu wapelelezi wa nje kuja kusaidia hawa wa ndani. Labda hujui tu kwamba baadhi ya hao wapelelezi wetu wamepata mafunzo kutoka kwa hao wazungu unaowaogopa.
Alipokuja Obama Tanzania ikulu ya Magogoni ilikuwa chini ya walinzi wa Kimarekani.
 
Msichanganye private investigators na FBI. Hawa wanalipwa private. Wakiweka ushahidi mezani unaweza kutumika mahakamani.
 
Despite its domestic focus, the FBI also maintains a significant international footprint, operating 60 Legal Attache (LEGAT) offices and 15 sub-offices in U.S. embassies and consulates across the globe. These overseas offices exist primarily for the purpose of coordination with foreign security services and do not usually conduct unilateral operations in the host countries.[6] The FBI can and does at times carry out secret activities overseas,[7] just as the CIA has a limited domestic function; these activities generally require coordination across government agencies.

Federal Bureau of Investigation - Wikipedia


NAANZA KUHISI KUNA UZINGUAJI KATIKA HILI JAMBO LA KUSEMA FBI WAKO TAYARI KUJA KUFANYA UPELELEZI KATIKA UGOMVI WA KUKU NA WANAWE.
 
Kama ni hivyo ina maana tunarudi kwenye original post, je nani atawalipa?

UN International Independent Investigation kuna fund nyingi sana kuzidi ata za ukimwi...Kumbuka hapa tunaongelea the president of TLS na kosa waliofanya Maccm ni kushindwa kumzuia kupata huo Upresident Mwakyembe alijua ili ndo maana akajaribu kujitutumua na kutishia kwa vijisheria vya kishenzi.
 
The UK has a budget of $1.04 trillion. The US has a budget of over $3.8 trillion. They can easily afford the cost of sending Scotland Yard or FBI for few weeks to conduct an independent investigation. Also, to receive money for services rendered to a poor third world country would be shameful for U.K. or U.S.
If you really mean it, hao US na UK wafute madeni wanayotudai ambayo walitumia uhuni kutuingiza mkenge.
====
Hoja yako NN ina mashiko. Ili kuondoa utata huu, kwa maandishi na kutangaza hadharani, chadema wawaahidi watanzania kuwa watakubaliana na matokeo hayo ambayo serikali itawajibika kuyatoa kutoka kwa hao wachunguzi huru. maana ni serikali yenye mamlaka ya kualika wachunguzi huru kutoka nje ya nchi. Ila nasisitiza wachunguzi hao wasitoke nchi ambazo hatuko sawa katika masuala ya mapambano ya kiuchumi (IPTL, Barrick, nakadhalika). Ingekuwa vyema wachunguzi watoke Russia, Ama nchi za schendinavia ambazo haziko kwenye umoja NATO!!
 
Kuna mtu kapost mitandaoni anashangaa kwamba Kibiti wameuliwa watu zaidi ya 40 lakini hatukusikia habari za wapelelezi wa kimataifa kuja kuwatafuta wauaji!!.

Wakati wanauliwa wale wananchi wasio na hatia humu mitandaoni kulijaa kejeli nyingi za ajabu, tena nyingine kutoka kwa hawa ambao wanataka wapelelezi wa kimataifa waje kufanya uchunguzi wa jaribio la mauaji.

Yaani mauaji ya watu zaidi ya 40 hayakustahili kufanyiwa uchunguzi wa kimataifa, lakini jaribio moja tu ndilo muhimu kwa sasa kwa taifa letu!!.

Mungu na anisamehe kama nimemkwaza mtu yoyote yule, ni katika kujaribu kuchangia mawazo yangu katika jumapili ya leo.
 
Labda tujiulize jambo moja, wale wapelelezi waliofichua mauaji ya Robert Ouko wa Kenya walilipwa na nani? Na kwa nini findings zao zilikubaliwa na kila MTU?

Acha masikhara wewe.

Matokeo ya uchunguzi wa hao wachunguzi yalikubaliwa na kila mtu?

Unajua maana ya kila mtu wewe?
 
Kuna mtu kapost mitandaoni anashangaa kwamba Kibiti wameuliwa watu zaidi ya 40 lakini hatukusikia habari za wapelelezi wa kimataifa kuja kuwatafuta wauaji!!.

Wakati wanauliwa wale wananchi wasio na hatia humu mitandaoni kulijaa kejeli nyingi za ajabu, tena nyingine kutoka kwa hawa ambao wanataka wapelelezi wa kimataifa waje kufanya uchunguzi wa jaribio la mauaji.

Yaani mauaji ya watu zaidi ya 40 hayakustahili kufanyiwa uchunguzi wa kimataifa, lakini jaribio moja tu ndilo muhimu kwa sasa kwa taifa letu!!.

Mungu na anisamehe kama nimemkwaza mtu yoyote yule, ni katika kujaribu kuchangia mawazo yangu katika jumapili ya leo.

..ni jambo la kawaida mikasa inapomkuta mtu MAARUFU ukilinganisha na wananchi wa kawaida

..kwa mfano msiba wa KANUMBA ulipewa coverage kubwa zaidi kuliko msiba wa MV BUKOBA ambapo wananchi 600+ walipoteza maisha.
 
This is a very good and interesting question!!! Rudely answer, their purpose is to try as much as they can to distort the development ambitions of targeted country
What benefits they get after spending their budget for this investigation?
 
Kuna mtu kapost mitandaoni anashangaa kwamba Kibiti wameuliwa watu zaidi ya 40 lakini hatukusikia habari za wapelelezi wa kimataifa kuja kuwatafuta wauaji!!.

Wakati wanauliwa wale wananchi wasio na hatia humu mitandaoni kulijaa kejeli nyingi za ajabu, tena nyingine kutoka kwa hawa ambao wanataka wapelelezi wa kimataifa waje kufanya uchunguzi wa jaribio la mauaji.

Yaani mauaji ya watu zaidi ya 40 hayakustahili kufanyiwa uchunguzi wa kimataifa, lakini jaribio moja tu ndilo muhimu kwa sasa kwa taifa letu!!.

Mungu na anisamehe kama nimemkwaza mtu yoyote yule, ni katika kujaribu kuchangia mawazo yangu katika jumapili ya leo.

Shhhh....can't say that...
 
Hpo ndpo nashangaa na mimi, wenye maelezo yote wako nje.

..hivi kungekuwa hakuna mtu aliyesalimika basi Polisi wangekuwa hawana njia ya kuwatafuta watuhumiwa?

..Najua dereva na TL ni victims na mashahidi muhimu ktk tukio hili. Lakini siamini kama bila wao Polisi hawawezi kufanya uchunguzi na kuwabaini magaidi waliofanya shambulizi lile.

..Tukio lile limefanyika mchana kweupe ktk MAKAO MAKUU YA NCHI. Tena wakati wa vikao vya BUNGE.

..Kwa maana hiyo ulinzi ulipaswa kuwa umeimarishwa.

..Kwenye nchi za wenzetu watuhumiwa wa matukio kama haya hukamatwa within 48 hours.

Nyani Ngabu
 
Hawahitaji pesa wanachohitajinibarua ya serikali ya kuwaruhusu tu
 
Back
Top Bottom