Uhuru wa wachunguzi huru

Uhuru wa wachunguzi huru

International independent investigation ssi Jeshi ni watu just Professionals sawa na hao Wachina wanaotujengea barabara.
 
Chamsingi apone aje atuambia ni nani mhusika, Kile kichwa kimelala muda wote uo nadhani kimejicharge nasasa kitaweza kuona tusivyoona.
 
International independent investigation ssi Jeshi ni watu just Professionals sawa na hao Wachina wanaotujengea barabara.
Kama ni hivyo ina maana tunarudi kwenye original post, je nani atawalipa?
 
ndugu yangu,omba yasikutokee wewe maana kuna msemo unasema MSIBA USIKIE KWA MWENZIO.
Comment yako inahusiana vipi na maoni yangu? Kama hujanielewa ni kwamba Chadema wanapaswa kujijengea uwezo wa kukusanya taarifa za kiitelijinsia kwa manufaa ya Chama ....issue si kusema tu flani kahusika ....wanapaswa kwenda hatua zaidi ya hapo otherwise hili litaisha kama yalivyoisha ya nyuma kibao ...
 
Serekali ikubali kwanza ujio wa wachunguzi huru, kukataa kwao kunanifanya wazidi kuwa kwenye mazingira ya kutuhumiwa. Ku fund project na kuinfluensi matokeo ni jambo linalo wezekana ingawa si rahisi kwa taasisi kubwa kama hizo.
Pale Soweto Arusha cdm wali dai kuundwa kwa tume ya kimahakama bado serekali ilikataa!
 
Comment yako inahusiana vipi na maoni yangu? Kama hujanielewa ni kwamba Chadema wanapaswa kujijengea uwezo wa kukusanya taarifa za kiitelijinsia kwa manufaa ya Chama ....issue si kusema tu flani kahusika ....wanapaswa kwenda hatua zaidi ya hapo otherwise hili litaisha kama yalivyoisha ya nyuma kibao ...
nimetoa maoni hayo baada ya wewe kusema CHADEMA kuomba uchunguzi huru kwa kilichompata LISSU ni SIASA ZA KUPOTEZEANA MUDA.
 
Vyombo vya usalama vitamkamata nani ikiwa mashahidi wa muhimu wote wapo Nairobi?
Polisi mkoani dodoma walikuwa na nafasi ya kumuhoji dreva wa Lissu kipindi bado akiwa nchini hawakufanya hivyo, mtu kafika Nairobi ndiyo wanasema anatakiwa kwa mahojiano!
Huu ni upuuzi wa hali ya juu! kuna wanaosema kuwa vyombo vya usalama vya Tz ilikuwa off kwa muda wakati tukio hili linafanyika!!
 
Labda tujiulize jambo moja, wale wapelelezi waliofichua mauaji ya Robert Ouko wa Kenya walilipwa na nani? Na kwa nini findings zao zilikubaliwa na kila MTU?
 
Nakubaliana na hoja za Nyani Ngabu.

Pia hebu fikirieni:

Vyombo vya kijasusi vya Marekani na/au Uingereza vije Tanzania kuchunguza kama vyombo vya dola vya TZ (polisi, usalama wa taifa, n.k.) walihusika na shambulizi la Lissu? Are you guys nuts?

Ni nchi gani duniani itaruhusu vyombo vya kijasusi vya taifa jingine waje wapeleleze mfumo wao wa ulinzi na usalama?

Halafu unawasikia viongozi wa juu kabisa wa CDM, ambao wanawania kuja kuiongoza TZ siku moja, wanaishauri serikali iruhusu huu ujinga.

CDM, you guys are not ready for prime time. Subirini miaka kadhaa ili mkomae kisiasa. Pathetic!
 
Kuna mda hutumiagi akili. hilo Ni changamoto? Ata mashahidi wangekuwa wamekufa upepelezi ungefanyika na wahusika wangepatikana think out of box.

....Sahihi kabisa mkuu, kuna channel moja Azam TV (Discovery Investigative...) aisee wanaonyesha live cases za kiuchunguzi ambapo hata pale ambapo mtu ameuwawa 5 - 10 yrs back bado muuwaji anakamatwa tuu.
 
Tokea Mh. Lissu anusurike kwenye shambulio dhidi ya uhai wake siku ashara na kitu zilizopita, kumekuwepo na sauti kadhaa zinazodai au zinazotaka tukio hilo lichunguzwe na wachunguzi 'huru' kutoka nje ya nchi.

Sababu yake kubwa ni kwamba vyombo vya ndani [ya nchi] vya usalama haviko huru kuweza kufanya uchunguzi huo kwa sababu vyenyewe ndivyo vinavyoshukiwa kupanga na kutekeleza jaribio hilo ili kutimiza matakwa ya mtu au watu wa huko serikalini na kwenye CCM.

Hisia hizo [za kuishuku na kuituhumu] nazielewa. Hivyo watu wanaotaka kuona wachunguzi huru wakichunguza nao nawaelewa.

Ila, kuna vitu vinanitatiza kidogo kuhusu huo u huru wa hao wachunguzi na utayari wa kambi ya Lissu na kambi ya serikali kuyakubali matokeo ya huo uchunguzi wao endapo utatokea.

La kwanza, ni nani atayeingia gharama za hao wachunguzi?

Tuseme CHADEMA na wafadhili wao ndiyo wataingia hizo gharama.

Kama hivyo ndo itavyokuwa, je, hao wachunguzi watakuwa huru kiasi gani ilhali wanalipwa na upande wa mnusurika wa jaribio?

CHADEMA kweli inaweza kuwalipa hao wachunguzi huru halafu hao wachunguzi watoe uchunguzi ambao ni kinyume na madai ya CHADEMA [kwamba serikali kupitia vyombo vyake vya usalama ndiye mhusika]? Kama wataletwa na CHADEMA maana yake ni kwamba wao ni waajiriwa wa hicho chama. Akili yangu haioni ni jinsi gani hao wachunguzi huru wanaweza kutoa matokeo yaliyo kinyume na hisia za watu waliowaajiri.

Je, serikali nayo ipo tayari kweli kuyakubali matokeo ya hao wachunguzi huru ambao huenda wakalipwa na hicho chama pinzani?

Na vipi kwa mfano serikali ikubali ujio wa hao wachunguzi na iingie gharama kwa kazi watayoifanya, je, CHADEMA ipo tayari kuyapokea na kuyakubali matokeo ya huo uchunguzi hata kama yakiwa tofauti na vile wao wadhaniavyo?

Kumbuka, kama serikali ndiyo itayoingia gharama za hao watu maana yake ni kwamba watakuwa wanaitumikia serikali iliyopo madarakani ambayo ni ya CCM.

Kwa mtaji huo hao wachunguzi huru watakuwa wapo huru kiasi gani?

Hili suala ni gumu kwa kweli. Kila ninapowaza na kuwazua sipati majibu.

Sijui nyie wadau mnalionaje hilo suala.

Jumapili njema.
Wauaji ni watu wenye mioyo migumu sana, ila kwa kuwa damu ya mwanadamu ni ya ajabu kupindukia always huwa wanajistukia!

Kwenye biblia kuna mistari hii!

3 Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana.
4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake;
5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.
6 Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?
7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.
8 Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani] Ikawa walipokuwapo uwandani,Kaini akamwinukia Habili nduguye,akamwua.
9 Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?
10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.

Hapo nilipobold maandiko yanaonyesha jinsi gani muuaji wa kwanza duniani, Kaini alivyomjibu Mungu kifedhuli!!

Point yangu ni kuwa upande wa waliomdhuru Lissu always watakataa katakata!! na watafanya kila wawezalo kuwaaminisha watu kuwa wao hawahusiki.

Kwa maoni yangu naamini kamwe serikali hawatokubali kamwe wachunguzi huru waje!!!

Kuhusu hoja kuwa wachunguzi huru watakuwa huru kiasi gani, naamini kuwa kwa watu kama scotland yard sio watu cheap kiasi hicho kwamba wakubali kuacha weledi wao eti kwa kuwa wana njaa ya pesa, au eti kwa kuwa kuna chama tawala Vs Chama pinzani, halafu hawa jamaa si huwa wanaweka fact zote?
 
Nyani Ngabu.

..Timu huru ya Wachunguzi inatakiwa itoke ktk nchi mojawapo zinazotupa misaada.

..Nchi hiyo ndiyo itakayogharimia uchunguzi huo

..Ikiwezekana watoke nchi zaidi ya moja.

..lingine labda ni kuwaomba UN. Nakumbuka Jaji Mkuu Mstaafu Othman Chande alikuwepo kwenye tume ya UN iliyoundwa na SG Ban Ki Mun kuchunguza kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa UN Dag Hamaskjolg kilichotokea miaka ya 60. UN decided to re-opened that investigation.

NB.

..kwa maoni yangu hapa tulipofika serikali/CCM na CDM wanahitaji MSULUHISHI WA KIMATAIFA.

..lazima CCM na CDM wabadili misimamo na mienendo yao on how to co-exist with one another. Msuluhishi wa kimataifa can help them figure that out.
 
Tokea Mh. Lissu anusurike kwenye shambulio dhidi ya uhai wake siku ashara na kitu zilizopita, kumekuwepo na sauti kadhaa zinazodai au zinazotaka tukio hilo lichunguzwe na wachunguzi 'huru' kutoka nje ya nchi.

Sababu yake kubwa ni kwamba vyombo vya ndani [ya nchi] vya usalama haviko huru kuweza kufanya uchunguzi huo kwa sababu vyenyewe ndivyo vinavyoshukiwa kupanga na kutekeleza jaribio hilo ili kutimiza matakwa ya mtu au watu wa huko serikalini na kwenye CCM.

Hisia hizo [za kuishuku na kuituhumu] nazielewa. Hivyo watu wanaotaka kuona wachunguzi huru wakichunguza nao nawaelewa.

Ila, kuna vitu vinanitatiza kidogo kuhusu huo u huru wa hao wachunguzi na utayari wa kambi ya Lissu na kambi ya serikali kuyakubali matokeo ya huo uchunguzi wao endapo utatokea.

La kwanza, ni nani atayeingia gharama za hao wachunguzi?

Tuseme CHADEMA na wafadhili wao ndiyo wataingia hizo gharama.

Kama hivyo ndo itavyokuwa, je, hao wachunguzi watakuwa huru kiasi gani ilhali wanalipwa na upande wa mnusurika wa jaribio?

CHADEMA kweli inaweza kuwalipa hao wachunguzi huru halafu hao wachunguzi watoe uchunguzi ambao ni kinyume na madai ya CHADEMA [kwamba serikali kupitia vyombo vyake vya usalama ndiye mhusika]? Kama wataletwa na CHADEMA maana yake ni kwamba wao ni waajiriwa wa hicho chama. Akili yangu haioni ni jinsi gani hao wachunguzi huru wanaweza kutoa matokeo yaliyo kinyume na hisia za watu waliowaajiri.

Je, serikali nayo ipo tayari kweli kuyakubali matokeo ya hao wachunguzi huru ambao huenda wakalipwa na hicho chama pinzani?

Na vipi kwa mfano serikali ikubali ujio wa hao wachunguzi na iingie gharama kwa kazi watayoifanya, je, CHADEMA ipo tayari kuyapokea na kuyakubali matokeo ya huo uchunguzi hata kama yakiwa tofauti na vile wao wadhaniavyo?

Kumbuka, kama serikali ndiyo itayoingia gharama za hao watu maana yake ni kwamba watakuwa wanaitumikia serikali iliyopo madarakani ambayo ni ya CCM.

Kwa mtaji huo hao wachunguzi huru watakuwa wapo huru kiasi gani?

Hili suala ni gumu kwa kweli. Kila ninapowaza na kuwazua sipati majibu.

Sijui nyie wadau mnalionaje hilo suala.

Jumapili njema.

Serikali pekeyake ndio yenye mamlaka ya kufanya uchunguzi wa matukio kama hayo na hata kama kwa njia moja ama nyingine wakija wachunguzi wa kutoka nje Serikali inawahpjibu wa Kulipia gharama hizo

Miaka ya Nyuma nyie mlipokuwa watoto, kuna Mabweni ya Shule ya Shauri Tanga iliyopo Kilimanjaro yaliungua moto na kuuwa wanafunzi wengi sana, kuna wachunguzi maalum kutoka nje waliitwa kuja kuchunguza hilo tukio na Serikali ililipia gharama zote ingawa shule haikuwa ya Serikali

So hakuna ubaya kwa Serikali kuita vyombo vyenye ueledi na vinavyotambulika kimataifa ili wafanye uchunguzi wa Tukio kubwa la Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 mchana wa juakali, sehemu inayolindwa na Askari wa Serikali 24/7
 
Tokea Mh. Lissu anusurike kwenye shambulio dhidi ya uhai wake siku ashara na kitu zilizopita, kumekuwepo na sauti kadhaa zinazodai au zinazotaka tukio hilo lichunguzwe na wachunguzi 'huru' kutoka nje ya nchi.

Sababu yake kubwa ni kwamba vyombo vya ndani [ya nchi] vya usalama haviko huru kuweza kufanya uchunguzi huo kwa sababu vyenyewe ndivyo vinavyoshukiwa kupanga na kutekeleza jaribio hilo ili kutimiza matakwa ya mtu au watu wa huko serikalini na kwenye CCM.

Hisia hizo [za kuishuku na kuituhumu] nazielewa. Hivyo watu wanaotaka kuona wachunguzi huru wakichunguza nao nawaelewa.

Ila, kuna vitu vinanitatiza kidogo kuhusu huo u huru wa hao wachunguzi na utayari wa kambi ya Lissu na kambi ya serikali kuyakubali matokeo ya huo uchunguzi wao endapo utatokea.

La kwanza, ni nani atayeingia gharama za hao wachunguzi?

Tuseme CHADEMA na wafadhili wao ndiyo wataingia hizo gharama.

Kama hivyo ndo itavyokuwa, je, hao wachunguzi watakuwa huru kiasi gani ilhali wanalipwa na upande wa mnusurika wa jaribio?

CHADEMA kweli inaweza kuwalipa hao wachunguzi huru halafu hao wachunguzi watoe uchunguzi ambao ni kinyume na madai ya CHADEMA [kwamba serikali kupitia vyombo vyake vya usalama ndiye mhusika]? Kama wataletwa na CHADEMA maana yake ni kwamba wao ni waajiriwa wa hicho chama. Akili yangu haioni ni jinsi gani hao wachunguzi huru wanaweza kutoa matokeo yaliyo kinyume na hisia za watu waliowaajiri.

Je, serikali nayo ipo tayari kweli kuyakubali matokeo ya hao wachunguzi huru ambao huenda wakalipwa na hicho chama pinzani?

Na vipi kwa mfano serikali ikubali ujio wa hao wachunguzi na iingie gharama kwa kazi watayoifanya, je, CHADEMA ipo tayari kuyapokea na kuyakubali matokeo ya huo uchunguzi hata kama yakiwa tofauti na vile wao wadhaniavyo?

Kumbuka, kama serikali ndiyo itayoingia gharama za hao watu maana yake ni kwamba watakuwa wanaitumikia serikali iliyopo madarakani ambayo ni ya CCM.

Kwa mtaji huo hao wachunguzi huru watakuwa wapo huru kiasi gani?

Hili suala ni gumu kwa kweli. Kila ninapowaza na kuwazua sipati majibu.

Sijui nyie wadau mnalionaje hilo suala.

Jumapili njema.
Wazungu sio kama wewe. Waite scotland yard kama kenya walivyofanya baada ya kifo cha Ouko uone wanavyoumbuka.Acha kuwa mpambe kwenye mambo ya ajabu
 
Nakubaliana na hoja za Nyani Ngabu.

Pia hebu fikirieni:

Vyombo vya kijasusi vya Marekani na/au Uingereza vije Tanzania kuchunguza kama vyombo vya dola vya TZ (polisi, usalama wa taifa, n.k.) walihusika na shambulizi la Lissu? Are you guys nuts?

Ni nchi gani duniani itaruhusu vyombo vya kijasusi vya taifa jingine waje wapeleleze mfumo wao wa ulinzi na usalama?

Halafu unawasikia viongozi wa juu kabisa wa CDM, ambao wanawania kuja kuiongoza TZ siku moja, wanaishauri serikali iruhusu huu ujinga.

CDM, you guys are not ready for prime time. Subirini miaka kadhaa ili mkomae kisiasa. Pathetic!
nikukumbushe tu,Zanzibar tu hapo alivyouawa PADRI waliwahi kuja.na ubalozi wa marekani ulivyolipuliwa waliwahi kuja hii unaizungumziaje?na vyombo vyetu ulivyovitaja vilikuwepo.
 
Walikuja kuchunguza mauaji ya padri. Kinachombwa na CDM sasa ni hao wapelele waje wachunguze vyombo vyetu vya usalama kwa sababu ndivyo vinavyoshutumiwa. Can't do that.
 
Mkuu unafahamu kitu chochote kuhusu National Security? Na je, Unafahamu maana ya Nchi kuwa huru? Tuna vyombo vya usalama vilivyo huru na kamwe kuachia wazungu kuja kuchunguza nchi ni kuuza uhuru na pia kuuza nchi yenyewe.
Acheni kuwa mnarahisisha mambo. Kibiti mbona kina Mbowe na timu yake hawakuomba uchunguzi huru? Wanataka kuficha madhambi yao eeh!?

Ukirudia kusoma hiki ulichoandika nadhani hutaamini macho yako. Sijui una umri gani lakini nikukumbushe tukio la kulipuliwa ubalozi wa Marikani hapa Dar. Ni FBI ndio walikuja nchini kufanya upelelezi na hata kugundua ni nani walihusika. Sijui kama unakumbuka mauaji ya Padri kule Zanzibar? Kikwete aliruhusu wapelelezi kutoka nje waje wasaidie kufichua wahusika wa mauaji yale. Kwa hiyo mjomba uhuru wa nchi hauuzwi kwa kuruhusu wapelelezi wa nje kuja kusaidia hawa wa ndani. Labda hujui tu kwamba baadhi ya hao wapelelezi wetu wamepata mafunzo kutoka kwa hao wazungu unaowaogopa.
 
Nakubaliana na hoja za Nyani Ngabu.

Pia hebu fikirieni:

Vyombo vya kijasusi vya Marekani na/au Uingereza vije Tanzania kuchunguza kama vyombo vya dola vya TZ (polisi, usalama wa taifa, n.k.) walihusika na shambulizi la Lissu? Are you guys nuts?

Ni nchi gani duniani itaruhusu vyombo vya kijasusi vya taifa jingine waje wapeleleze mfumo wao wa ulinzi na usalama?

Halafu unawasikia viongozi wa juu kabisa wa CDM, ambao wanawania kuja kuiongoza TZ siku moja, wanaishauri serikali iruhusu huu ujinga.

CDM, you guys are not ready for prime time. Subirini miaka kadhaa ili mkomae kisiasa. Pathetic!
Mkuu hivi USA wana haja gani na kuichunguza Tz wakati details nyingi za Tz wanazo? teknolojia zote za vyombo vya ulinzi na usalama vya Tz zinatoka nje na zote kwa USA ni vitu vinavyjulikana kinagaubaga maana wao walishapitia hivyo makumi ya miaka iliyopita hivyo hatuna cha msingi saaaaaaaana cha kuwaficha.

Kwa taarifa yako tu USA wana taarifa za kila mtumiaji wa computer hii ni kwa kuwa kwenye hard disk kuna namna ambayo USA wana access na taarifa zilizohifadhiwa humo wakitaka unalijua hili???

High tech co. zote za sillicon valley zina uhusiano mkubwa sana na vyombo kama CIA na FBI hivyo wao kupata taarifa si jambo kubwa saana unalijua hili!

Hivi kipindi kile cha ajali ya MV bukoba si Mkapa kupitia Jeshi la wanamaji wa Tz aliomba msaada South Africa???

Halafu scotland yard si walienda Kenya kipindi fulani kuchunguza mauaji kule na baadhi ya vyombo vya usalama vya Kenya vilichunguzwa??

We ulitaka chadema wahamishe magoli waseme mtuhumiwa wa mtu wao ni yule wanayeamini kuwa siye???

Mkuu thamani ya uhai wa mtu haiwezi kulinganishwa maslahi mufilisi ya siasa za hovyo zinazoendelea Tz, ni zawadi toka kwa Mungu!!
 
Kumbe wanao chati humu ni ukawaaaa tyuuuu uwiiii hawana kazi za kufanyaaa CCM chapa kazi tulijenge taifa wakulijengua wako kwenye vikao hila hawataweza
 
Back
Top Bottom