Uhuru wa wachunguzi huru

Uhuru wa wachunguzi huru

Mwandishi Wetu, Zanzibar

ASKARI wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), wamewasili Zanzibar kufanya uchunguzi wa kuwabaini waliomuua kwa kumpiga risasi, Padri Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki.

Kamishna wa Polisi wa Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisema kwa simu jana kuwa wapelelezi wa kigeni wamewasili Zanzibar na tayari na wameanza kazi hiyo.
Wapelelezi hao wameingia kazini kushirikiana na wenzao wa Tanzania kuwasaka wauaji wa padri huyo aliyepigwa risasi Februari 17, mwaka huu.

Padri Mushi aliuawa asubuhi alipokuwa akienda kuongoza ibada katika Kanisa la Mtakatifu Teresia, Beit el Raas, nje kidogo ya Mji wa Zanzibar na kuzikwa Kitope, Kaskazini Unguja Februari 20, mwaka huu.

“Wapelelezi kutoka nje wamefika na wapo kazini,” Kamishna Mussa alisema bila ya kutaja wanatoka nchi gani.

Pia Kamishna Mussa hakutaka kueleza ni lini wapelelezi hao walifika Zanzibar na idadi yao kwa maelezo kwamba hizo ni siri za Polisi na zikivuja, zitaingilia uchunguzi wanaoufanya.
Hata hivyo, vyanzo vya ndani ya Serikali, vililithibitishia gazeti hili kuwa FBI walikuwa wameanza kuwasaka wauaji wa Padri Mushi.

Kutua kwa wapelelezi hao wa Marekani kunafuatia kauli iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete katika salamu zake za rambirambi baada ya mauaji ya Padri Mushi kuwa ameliagiza Jeshi la Polisi kutumia nguvu zake zote pamoja na kushirikiana na vyombo vingine vya usalama vya ndani na mashirika ya upelelezi ya nchi rafiki katika kufanya uchunguzi wa mauaji hayo.

Awali, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alihusisha tukio hilo na vitendo vya ugaidi wakati akitoa tamko la Serikali na kueleza kuwa Rais Kikwete ameidhinisha Serikali kugharamia wapelelezi kutoka nje.

Pia ujio wa FBI unaweza kuhusishwa moja kwa moja na dhamira iliyoonyeshwa mapema na Serikali ya Marekani iliyokuwa tayari kusaidia upelelezi wa mauaji hayo na hiyo ilibainishwa katika salamu za rambirambi za kifo hicho na Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt.
Vyanzo mbalimbali kutoka ndani ya Serikali vimeeleza kuwa kabla ya kuanza kwa operesheni hiyo, maofisa wa FBI walifanya mazungumzo na Waziri Nchimbi na viongozi wengine wa Serikali kwa ajili ya kuangalia ni namna gani watafanya shughuli hiyoreturnoa hawa jamaa wa FBI walifanya vikao na maofisa wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), ili kuweka sawa mazingira ya kufanya upelelezi huu,” kilisema chanzo kingine.

Habari zaidi zinaeleza kuwa uchunguzi wa wapelelezi hao wa FBI na wale wa Tanzania hautajikita katika kusaka wauaji wa Padri Mushi pekee, bali watakwenda mbali zaidi na kuchunguza wale wote wanaojihusisha na wimbi la vurugu za kidini nchini ambalo linatishia amani.

Hii itakuwa mara ya pili kwa FBI kuja nchini kufanya operesheni kubwa ya upelelezi. Mwaka 1998 walifika kuchunguza kulipuliwa kwa Ubalozi wa Marekani na kugundua kuwa Kundi la Al-Qaeda lilihusika.

Aidha hiyo ni mara ya tatu kwa wapelelezi wa Tanzania kushirikiana na wageni kuchunguza matukio ya uhalifu baada ya mwaka 1984, Idara ya Upelelezi ya Uingereza, Scotland Yard ya Uingereza kuchunguza kuungua kwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Habari zaidi zinaeleza kuwa kabla ya ujio wa FBI, Serikali ya Tanzania ilizungumza na taasisi za upelelezi za nchi tano ili kuongeza nguvu. Taasisi nyingine zinazodaiwa kuombwa kufanya kazi hiyo ni pamoja na Scotland Yard na Shirika la Upelelezi la Israel, Mossad.

Akizungumzia upelelezi wa mauaji ya Padri Mushi, Kamishna Mussa alisema watu kadhaa wametiwa mbaroni kwa mauaji lakini asingeweza kutaja idadi.

Kuuawa kwa padri huyo ni miongoni mwa matukio ya kushambuliwa kwa viongozi wa dini huko Zanzibar baada ya kumwagiwa tindikali Katibu wa Mufti, Fadhil Soraga, kupigwa risasi kwa Padri Ambrose Mkenda wa Kanisa Katoliki na kuuawa kwa Sheikh Ali Khamis shambani kwake huko Kidoti, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Lissu angekua padri au askofu hao FBI,Mossad Wangesharuhusiwa kuja
Unafiki mbaya sana.

FaizaFoxy Ritz Return Of Undertaker mshana jr Mwanahabari Huru Nyani Ngabu
 
Mkuu unafahamu kitu chochote kuhusu National Security? Na je, Unafahamu maana ya Nchi kuwa huru? Tuna vyombo vya usalama vilivyo huru na kamwe kuachia wazungu kuja kuchunguza nchi ni kuuza uhuru na pia kuuza nchi yenyewe.
Acheni kuwa mnarahisisha mambo. Kibiti mbona kina Mbowe na timu yake hawakuomba uchunguzi huru? Wanataka kuficha madhambi yao eeh!?
Kama kweli munaamini akina Mbowe ndio wahusika, acheni uchunguzi huru ili akina Mbowe waumbuke.

Kwa nini mnakuwa na kigugumizi ilihali mnajinasibu hamuhusiki, mnatapatapa nini!!

Acheni uchunguzi huru tupatiwe ukweli wa hili jambo.

Endeleeni kutapatapa hivyo hivyo lakini mkumbuke hii damu mliyoimwaga mchana kweupe kwenye makazi ya Viongozi wa serikali haitawaacha salama daima.
 
Mwandishi Wetu, Zanzibar

ASKARI wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), wamewasili Zanzibar kufanya uchunguzi wa kuwabaini waliomuua kwa kumpiga risasi, Padri Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki.

Kamishna wa Polisi wa Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisema kwa simu jana kuwa wapelelezi wa kigeni wamewasili Zanzibar na tayari na wameanza kazi hiyo.
Wapelelezi hao wameingia kazini kushirikiana na wenzao wa Tanzania kuwasaka wauaji wa padri huyo aliyepigwa risasi Februari 17, mwaka huu.

Padri Mushi aliuawa asubuhi alipokuwa akienda kuongoza ibada katika Kanisa la Mtakatifu Teresia, Beit el Raas, nje kidogo ya Mji wa Zanzibar na kuzikwa Kitope, Kaskazini Unguja Februari 20, mwaka huu.

“Wapelelezi kutoka nje wamefika na wapo kazini,” Kamishna Mussa alisema bila ya kutaja wanatoka nchi gani.

Pia Kamishna Mussa hakutaka kueleza ni lini wapelelezi hao walifika Zanzibar na idadi yao kwa maelezo kwamba hizo ni siri za Polisi na zikivuja, zitaingilia uchunguzi wanaoufanya.
Hata hivyo, vyanzo vya ndani ya Serikali, vililithibitishia gazeti hili kuwa FBI walikuwa wameanza kuwasaka wauaji wa Padri Mushi.

Kutua kwa wapelelezi hao wa Marekani kunafuatia kauli iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete katika salamu zake za rambirambi baada ya mauaji ya Padri Mushi kuwa ameliagiza Jeshi la Polisi kutumia nguvu zake zote pamoja na kushirikiana na vyombo vingine vya usalama vya ndani na mashirika ya upelelezi ya nchi rafiki katika kufanya uchunguzi wa mauaji hayo.

Awali, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alihusisha tukio hilo na vitendo vya ugaidi wakati akitoa tamko la Serikali na kueleza kuwa Rais Kikwete ameidhinisha Serikali kugharamia wapelelezi kutoka nje.

Pia ujio wa FBI unaweza kuhusishwa moja kwa moja na dhamira iliyoonyeshwa mapema na Serikali ya Marekani iliyokuwa tayari kusaidia upelelezi wa mauaji hayo na hiyo ilibainishwa katika salamu za rambirambi za kifo hicho na Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt.
Vyanzo mbalimbali kutoka ndani ya Serikali vimeeleza kuwa kabla ya kuanza kwa operesheni hiyo, maofisa wa FBI walifanya mazungumzo na Waziri Nchimbi na viongozi wengine wa Serikali kwa ajili ya kuangalia ni namna gani watafanya shughuli hiyo.

“Pia hawa jamaa wa FBI walifanya vikao na maofisa wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), ili kuweka sawa mazingira ya kufanya upelelezi huu,” kilisema chanzo kingine.

Habari zaidi zinaeleza kuwa uchunguzi wa wapelelezi hao wa FBI na wale wa Tanzania hautajikita katika kusaka wauaji wa Padri Mushi pekee, bali watakwenda mbali zaidi na kuchunguza wale wote wanaojihusisha na wimbi la vurugu za kidini nchini ambalo linatishia amani.

Hii itakuwa mara ya pili kwa FBI kuja nchini kufanya operesheni kubwa ya upelelezi. Mwaka 1998 walifika kuchunguza kulipuliwa kwa Ubalozi wa Marekani na kugundua kuwa Kundi la Al-Qaeda lilihusika.

Aidha hiyo ni mara ya tatu kwa wapelelezi wa Tanzania kushirikiana na wageni kuchunguza matukio ya uhalifu baada ya mwaka 1984, Idara ya Upelelezi ya Uingereza, Scotland Yard ya Uingereza kuchunguza kuungua kwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Habari zaidi zinaeleza kuwa kabla ya ujio wa FBI, Serikali ya Tanzania ilizungumza na taasisi za upelelezi za nchi tano ili kuongeza nguvu. Taasisi nyingine zinazodaiwa kuombwa kufanya kazi hiyo ni pamoja na Scotland Yard na Shirika la Upelelezi la Israel, Mossad.

Akizungumzia upelelezi wa mauaji ya Padri Mushi, Kamishna Mussa alisema watu kadhaa wametiwa mbaroni kwa mauaji lakini asingeweza kutaja idadi.

Kuuawa kwa padri huyo ni miongoni mwa matukio ya kushambuliwa kwa viongozi wa dini huko Zanzibar baada ya kumwagiwa tindikali Katibu wa Mufti, Fadhil Soraga, kupigwa risasi kwa Padri Ambrose Mkenda wa Kanisa Katoliki na kuuawa kwa Sheikh Ali Khamis shambani kwake huko Kidoti, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Kumbe Polisi waliomba.. ahaa.. sasa kama ni hivyo unaonaje na Polisi yetu ikaomba hawa jamaa waje "kuongeza nguvu", unafikiri watafanya kazi peke yao bila polisi kuhusika??

Bado nachelea hili neno "wachunguzi huru"... Bado nahitaji kueleweshwa..
 
Nyani Ngabu unajua ukweli na unapotosha tu. FBI au Scotland yard hawahitaji kulipwa na Tanzania. Wanachohitaji ni ruhusa tu toka serikali ya TZ.

Marekani na UK wana budget ya misaada kwa nchi maskini na malipo yatatoka humo.

Mbona kwenye kupigwa mabomu Dar tuliwaita hao FBI na Scotland yard?
 
Ukitoa uhuru unaotokana na finance issues kwa wachunguzi ....kuna issues za kidiplomasia ....sometimes nchi hizi zina maslahi yao ....hao wachunguzi wanaweza kutumia huo mwanya kwa faida za kidiplomasia zaidi .....Chadema wamekuwa wakijinadi kwa intelijinsia yao ....waitumie watoe ushahidi hata kama serikali haitochukua hatua .....haya mengine ni siasa tu za kupotezeana muda .....
 
Intelligence ya Chadema inaonesha wahusika ni walewale jamaa zetu wa mhimili.
 
Vyombo vya usalama vitamkamata nani ikiwa mashahidi wa muhimu wote wapo Nairobi?

...wa muhimu wote wapo Nairobi? Usisahau waliokuwa Dodoma hotel siku ya shambulizi; pia walinzi wa eneo anapoishi Lissu; na majirani zake waliokuwa nyumbani siku hiyo.
 
Vyombo vya usalama vitamkamata nani ikiwa mashahidi wa muhimu wote wapo Nairobi?
Vipi wale waliomuua Mawazo shahidi alikimbilia Nairobi?? Vipi yule aliyemtisha Nape kwa Bastola kwani Nape alikimbilia Nairobi?? Acha kuweweseka
 
Mkuu unafahamu kitu chochote kuhusu National Security? Na je, Unafahamu maana ya Nchi kuwa huru? Tuna vyombo vya usalama vilivyo huru na kamwe kuachia wazungu kuja kuchunguza nchi ni kuuza uhuru na pia kuuza nchi yenyewe.
Acheni kuwa mnarahisisha mambo. Kibiti mbona kina Mbowe na timu yake hawakuomba uchunguzi huru? Wanataka kuficha madhambi yao eeh!?
Zanzibari walipokua FBI mauwaji ya Padri hukuona??
 
Ninachojua mimi kinachoombwa kwa hivi vyombo vya uchunguzi ni msaada,wanachohitaji wao ni maombi rasmi kutoka nchi husika na sidhani kama kuna malipo yoyote hapo zaidi ya gharama za kutoa ushirikiano utakapohitajika,kama serikali zao huwa zinajitolea kuja kufundisha majeshi yetu bure itakuwa kuombwa kufanya uchunguzi kwa jambo moja tu?kinachoshindikana mara nyingi ni utashi maana mpaka serikali iamue kuruhusu kuomba huo msaada ni kwamba kweli inakuwa na dhamira ya dhati ya kuwapata wahalifu.
 
We ndo hujatumia akili! anachomaanisha huo upelekezi ungekuwa huru kiasi gan kwa maana ungeweza kuegemea kwa upande uliowaleta na kuwalipa, ungeanza hapo kujadili
utaegemea vipi ??
wao watatafuta wahusika na evidence kama vyombo vya usalama havihusiki it means watakosa evidence zinazo walink na tukio
 
Mkuu unafahamu kitu chochote kuhusu National Security? Na je, Unafahamu maana ya Nchi kuwa huru? Tuna vyombo vya usalama vilivyo huru na kamwe kuachia wazungu kuja kuchunguza nchi ni kuuza uhuru na pia kuuza nchi yenyewe.
Acheni kuwa mnarahisisha mambo. Kibiti mbona kina Mbowe na timu yake hawakuomba uchunguzi huru? Wanataka kuficha madhambi yao eeh!?

kwanini mnapenda kuanza sentensi za kutishia?kwanini wewe unaefahamu chochote usielezee kile unachofahamu?kama kuuza nchi serikali hii iliyopo madarakaki ilishauza kitambo sasa wewe unaogopa nini?

Hivi unadhani kwa akili yako hao wazungu unaowasemea hapa wamekaa wanasubiri nafasi hiyo tu ya kuja kufanya uchunguzi huru ili kutufanyia ushushushu?unafeli kufikiri hivyo,hao wazungu unaowasema wana watu wao wa intelijensia hata huko kwenye makinikia usifikiri hizo kampuni za uwekezaji zinakuja kiboyaboya tu.
 
Mi nadhani suala la nani anayelipa sio ishu naamini kwa sababu watakaokuja ni professionals watafanya kazi accordingly na isitoshe watatoa vielelezo ku back up their findings!
Tatizo la miafrika na Miccm.... bro,inakuja na swali dhaifu.....they don't believe so called professionalism
 
Ukitoa uhuru unaotokana na finance issues kwa wachunguzi ....kuna issues za kidiplomasia ....sometimes nchi hizi zina maslahi yao ....hao wachunguzi wanaweza kutumia huo mwanya kwa faida za kidiplomasia zaidi .....Chadema wamekuwa wakijinadi kwa intelijinsia yao ....waitumie watoe ushahidi hata kama serikali haitochukua hatua .....haya mengine ni siasa tu za kupotezeana muda .....
ndugu yangu,omba yasikutokee wewe maana kuna msemo unasema MSIBA USIKIE KWA MWENZIO.
 
Back
Top Bottom