Uhuni wa Hospitali ya Jeshi Lugalo

Uhuni wa Hospitali ya Jeshi Lugalo

Status
Not open for further replies.

fisi 2

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
3,284
Reaction score
4,652
Ni tarehe 10 June 2018 namfikisha mwanangu amevunjika mkono ili apatiwe tiba. Tunalipia kila kitu natoka kulipia nakutana na Mama mmoja analia mwanae mkono wake umeunga vibaya baada ya kutibiwa hapo hapo na wamenwambia akalipie wauvunje wauunge tena.

Nafika kwa dokta muhusika namkuta Dada mwingine na mwanae wa miaka 3 nae mkono umeunga vibaya inabidi nae wauvunje waunge upya. Najipa moyo nikisema bahati mbaya. Mwanangu anafungwa POP naambiwa rudi baada ya siku 14.

Tarehe 25 June 2018 narudi POP inatolewa X Ray majibu mkono umeunga vibaya. Inabidi tuuvunje tuunge upya!! MMMH. Watoto hawa ni 2-5 years.

Jamani hii ni biashara au nini? Nidhamu iko wapi?

Naomba Advocate humu niwashtaki Lugalo Hospital. Sasa hivi naelekea MOI tu ila nina uchungu sana.

======

UPDATES: 14 Julai 2018

Habari hii imekanushwa..

Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania limekanusha taarifa zilizosambazwa kupitia mitandao ya kijamii kuhusu malalamiko juu matibabu ya mtoto anayedaiwa kuvunjika na kupatiwa huduma katika Hospitali kuu ya jeshi ya Lugalo.

Akizungumza na waandishi wa habari Leo Jijini Dar es Salaam msemaji mkuu wa Jeshi Kanali Ramadhani Dogoli alimtaka aliyejinasibisha kama mlalamikaji kuwasilisha malalamiko yake kama yana ukweli ili hatua zichukuliwe kwa wahusika.

“ Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ linamtaka malalamikaji alete taarifa kwenye uongozi ili kama matukio hayo yametokea tuweze kuchukua hatua kwa wahusika” Alisema kanali Dogoli.

Aliongeza kuwa iwapo aliyedai kulalamika atashindwa kufanya hivyo jeshi litaaamini kuwa mlalamikaji alikusudia kuichafua hospitali yetu kwa maslahi binafsi na kwa sababu hiyo tutamtafuta haraka na kumchukulia hatua zinazomstahili.
 
Ni tarehe 10 June 2018 namfikisha mwanangu amevunjika mkono ili apatiwe tiba. tunalipia kila kitu natoka kulipia nakutana na Mama mmoja analia mwanae mkono wake umeunga vibaya baada ya kutibiwa hapo hapo na wamenwambia akalipie wauvunje wauunge tena. nafika kwa dokta muhusika namkuta Dada mwingine na mwanae wa miaka 3 nae mkono umeunga vibaya inabidi nae wauvunje waunge upya. mh najipa moyo nikisema bahati mbaya. Mwanangu anafungwa POP naambiwa rudi baada ya siku 14. tarehe 25 June 2018 narudi POP inatolewa X Ray majibu mkono umeunga vibaya. Inabidi tuuvunje tuunge upya????? MMMH. Watoto hawa ni 2-5 years. jamani hii ni biashara au nini??? Nidhamu iko wapi???? Naomba Advocate humu niwashtaki Lugalo Hospital. Sasa hivi naelekea MOI tu ila nina uchungu sana.
Lugalo ni shiiiiida hasa kwenye idara ya watoto kule mwenge kuna uzembe mwingi kwa Madokta wa watoto ushauria wao kwa asilimia kubwa ni sawa na wa waganga wa kienyeji, watoto wengi hufariki na wengine kulemaa kwa uzembe wao, hata wajawazito wengi wanaokwenda kupata Huduma huko hulalamikia taratibu zao kwa sasa, idara za huduma za Afya walitizame hilo kwa jicho la tatu.
 
Jambo la kujiuliza hao madakitari wa Lugalo ni experts wa hizo fani? au ni clinical officers wa jeshi waliosoma ukumbwani kutowa huduma ya kwanza kwewezao incase ya emergence.
Nadhani suala la uhakiki wa vyeti na ujuzi wao linabidi kufanyiwa uchunguzi vizuri, yapo malalamiko mengi sana ni wakati mkuu wa Hosptal azinduke afanye mabadiliko kila idara kwenye hiyo Hosptal.
 
Mkuu kwanza wewe una tatizo

Unakutana na mtu zaidi ya mmoja analalamikia tatizo lile lile bado unampeleka mgonjwa wa shida ile ile

Tukikuita mpumbavu tutakuwa tumekosea?
huyo Dokta anayetumia watoto kufanya mazoezi ya kuuga mifupa yafaa afukuzwe kazi mara moja pengine ana vyeti feki
 
Ni tarehe 10 June 2018 namfikisha mwanangu amevunjika mkono ili apatiwe tiba. tunalipia kila kitu natoka kulipia nakutana na Mama mmoja analia mwanae mkono wake umeunga vibaya baada ya kutibiwa hapo hapo na wamenwambia akalipie wauvunje wauunge tena. nafika kwa dokta muhusika namkuta Dada mwingine na mwanae wa miaka 3 nae mkono umeunga vibaya inabidi nae wauvunje waunge upya. mh najipa moyo nikisema bahati mbaya. Mwanangu anafungwa POP naambiwa rudi baada ya siku 14. tarehe 25 June 2018 narudi POP inatolewa X Ray majibu mkono umeunga vibaya. Inabidi tuuvunje tuunge upya????? MMMH. Watoto hawa ni 2-5 years. jamani hii ni biashara au nini??? Nidhamu iko wapi???? Naomba Advocate humu niwashtaki Lugalo Hospital. Sasa hivi naelekea MOI tu ila nina uchungu sana.
Pole nyingi Mkuu.
 
Lugalo ni shiiiiida hasa kwenye idara ya watoto kule mwenge kuna uzembe mwingi kwa Madokta wa watoto ushauria wao kwa asilimia kubwa ni sawa na wa waganga wa kienyeji, watoto wengi hufariki na wengine kulemaa kwa uzembe wao, hata wajawazito wengi wanaokwenda kupata Huduma huko hulalamikia taratibu zao kwa sasa, idara za huduma za Afya walitizame hilo kwa jicho la tatu.
Mwenge na Lugalo main campus zina uhusiano gani?
 
Pole sana mkuu.
Yani hii nchi hii. Wanageuza majaribio kwenye miili yetu na ya watoto wetu?
Kwa vile ni Jeshini nadhani hata Wizara haitafuatilia. Maana Jiwe alishawahi sema kuwa kile kivuko chake kibovu anakipeleka jeshini sasa ole wake atakayekiandika.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom