Mkuu FGM, kwa mujibu wa hozo nondo, BASHE sio raia halali. Ili kuwa raia halali wa Tanzania ni lazima
- Uraia wa kuzaliwa, ila pia lazima mmoja wa wazazi wako awe ni rais pindi ilipozaliwa!.
- Bashe ana haki zote za uraia wa Tanzania wa kuzaliwa, bila ubishi, ila wakati anazaliwa, wazazi wake wote wawili walikuwa sio raia!. Hivyo pamoja na kuzaliwa na haki zote za uraia wa Tanzania wa kuzaliwa, kufuatia wazazi wake wote wawili kuwa sii raia wakati anazaliwa, alipaswa baada ya kufikia "the age of majority", umri wa miaka 18, alipaswa kula kiapo cha kuukana uraia wa wazazi wake, ili kuuhalalisha "birth right" yake ya uraia wa Tanzania!.
- Bashe amelikwepa hilo kwa kufanya forgery ya vyeti vya kuzaliwa vya mama yake na baba mzaa mama ili kujihalalisha kuwa yeye ni raia halali wa Tanzania kwa kigezo cha kuzaliwa Tanzania na mmoja wa wazazi wake, Mama ni Mtanzania!.
- Vile vyote viwili ni forgery, vyote viwili vimetolewa tarehe siku moja na kusainiwa na mtu mmoja aliyekuwepo sehemu mbili tofauti!.
- Hakuna chuki yoyote binafsi dhidi ya Bashe, bali hitaji lake ni dogo tuu, wala halihitaji kutoa matangazo magezetini, anachotakiwa kufanya ni kuukana tuu uraia wa wazazi wake wakati alipozaliwa!. Angekuwa ndio anaomba uraia ingembidi kutoa tangazo gazetini kwa siku mbili mfufulilizo!.
Wanabody, haya masuala ya uraia sio politics, ni mambo ya kufuata sheria taratibu na kanuni, nothing more,
nothing less, ila pia lazima nikiri wazi kabisa, Tanzania tuna double standars sana!. Ile hoja ya Mchungaji Mtikila, kuna nanii pia hakuwa raia halali, kwa sababu alizaliwa nchumbiji, na alikuja nchini akiwa na umri wa miaka 6, huku nchini ni upande wake wa umamani, hata jina la che ni la upande wa umamani!, hakusikilizwa!.
P.