Uhamiaji wanafanya nini? Kumbe Hussein Bashe si Raia! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhamiaji wanafanya nini? Kumbe Hussein Bashe si Raia!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by gwaigwa, Sep 24, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. g

  gwaigwa Member

  #1
  Sep 24, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Leo kuna barua nimeikuta ofisini kwetu ikijadiliwa na wakubwa, ni kutoka kwa mdau mmoja wa Nzega anayejiita Maganga Masanja amemwaga data za uraia wa Basha nimeisoma nikashangaa yaani mpaka mtu agombee nafasi kubwa ndiyoi haya yanajulikana, vipi angeingia mpaka akatawala nchi tungefanyaje?

  Gwaigwa.

  habari kamili hii hapa chini kwa kweli inashtua soma mwenyewe na angalia viambatanisho pia kama vielelezo

  Maganga Masanja,

  NZEGA.

  TABORA
   

  Attached Files:

 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Hussein Bashe anaonekana ni tishio sana kwa ccm nzega!
   
 3. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,582
  Likes Received: 4,692
  Trophy Points: 280
  Jamani Benjamin William Mkapa naye siyo raia, yeye ni M'meto toka Msumbiji.
   
 4. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Hiii kali
   
 5. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  magamba bana?
   
 6. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Sasa mbona hawam-deport kama sio raia
   
 7. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  SIwezi kusoma
   
 8. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #8
  Sep 24, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hii sinema nyingine tamu.
   
 9. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #9
  Sep 24, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  MASHA ALIMSAFISHA KITAMBO, UNAKUMBUKA HII...

  KITENDAWILI cha uraia wa Hussein Bashe, mgombea ubunge Nzega (CCM) aliyeenguliwa, kimeibua mapya.
  Wiki iliyopita, Waziri wa Mambo ya Ndani, Laurance Masha aliutangazia ulimwengu kuwa Bashe ni raia halali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Akahoji, "Nani mwenye mamlaka ya kusema Bashe si raia? Nikiwa waziri mwenye dhamana nasema, Bashe ni raia halali na hakuna atakayebadilisha uamuzi huu."

  Aliyesema kuna utata katika uraia wa Bashe, ni Rais Jakaya Kikwete, tena ndani ya vikao halali vya chama chake.
  Taarifa zinasema, ndani ya ukumbi wa mkutano Kikwete alisimama kidete kutetea hoja yake kwamba Bashe si raia. Alisema amepata "taarifa za vyombo vya usalama," zinazothibitisha utata wa uraia wa Bashe.Wengine waliondeleza kauli ya rais, ni viongozi wakuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Katibu Mkuu Yusuf Makamba na Katibu Mwenezi John Chiligati.

  Masha amenukuu vifungu kadhaa vya sheria ya uhamiaji akisema vinahalalisha uraia wa Bashe.
  Kwa mfano, ananukuu vifungu Na.5 (1) na Na. 7 (8) vya Sheria Na. 7 ya uraia ya mwaka 1995 na kusema, "Bashe ni raia halali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tena kwa kuzaliwa." Anasema tayari amejulisha Bashe kuhusu uamuzi huo.
  Je, Masha hakushauriana na Kikwete, Makamba na Chiligati kabla ya kutoa uamuzi waliofikia? Kama walishauriana, kwa nini wanaanika nguo za ndani hadharani?Kama walishauriana, kipi kinachompa ujasiri Masha hadi kuamua kupigana na mwamba? Nani aliyemhakikishia usalama wake kisiasa na kimaslahi?

  Akiongea kwa kujiamini, Masha alisema kwa mujibu wa nyaraka zilizopo na taarifa zilizofikia wizara yake, "…suala la uraia wa Bashe halina utata." Katika maelezo yake, Masha anasema Bashe ni raia halali wa Tanzania, tena kwa kuzaliwa. Hili nalo lina utata. Hata Bashe anajua hilo; kwamba si raia wa kuzaliwa.Masha anajua kuwa wakati Bashe anazaliwa, baba yake mzazi alikuwa hajaomba uraia. Alikuwa raia wa Somalia. Alipoomba uraia wa Tanzania, hakumwingiza Bashe katika maombi aliyowasilisha katika fomu zake za kuomba uraia.

  Aidha, Bashe mwenyewe amekana uraia wa Somalia akiwa na miaka 25.Kama haya ndiyo maelezo ya Bashe, kwamba baba yake alipoomba uraia hakumuingiza yeye katika maombi yake; hiki ambacho Masha anaita, "Bashe raia wa kuzaliwa" kinatoka wapi? Kimelenga nini? Kama Bashe hakuzaliwa Tanzania, na baba yake hakuzaliwa nchini na hata wakati baba anaomba uraia, Bashe akiwa na miaka kumi; nani basi rai wa kuzaliwa? Je, Masha amelenga nani na kwa faida ipi?

  Kama Kikwete anasema Bashe si raia, huku Masha anasema tofauti, nani aaminike na yupi apuuzwe? Inawezekana Masha anajua vema nani anamtumikia, lakini siyo rais Jakaya Mrisho Kikwete na serikali yake.Ingekuwa Masha anatumikia Kikwete, waziri na rais wasingepanda gari moja, lakini wakaelekea tofauti. Ama wotateremka na kila mmoja aende zake, au mmoja atabaki kwenye gari.
  Lakini ukiyatafsiri vema haya utayafupisha kwa kauli hii: Kikwete ana serikali mbili. Zipi? Serikali anayozunguka nayo na nyingine iliyo kivulini.

  Katika nchi zote ambako rushwa imekomaa na ufisadi umekuwa dini, dola linakuwa na sura mbili. Serikali mbili, mabunge mawili na mahakama mbili.Kunakuwa na waasi wasioonekana kama majini ya Sheikh Yahya Hussein. Wanabaki kivulini.
  Watatenda bila kuafikiana na wanaishi kwa kuviziana na kuzomeana. Hatimaye aliyeko kivulini anaangusha serikali iliyo wazi na iliyochaguliwa.

  Wakati siyo rahisi kujua Masha yumo katika serikali ya dola lipi, katika hali ya kawaida, asingeweza kwenda kinyume na Kikwete, kama asingeweza kuwa na uhakika wa usalama wake kisiasa. Sasa kuna wenye maoni kuwa hatua ya Masha "kumsafisha" Bashe imedhihirisha kuwa yeye na yule aliyemteua, wamo serikali tofauti. Hoja ni je, hali hiyo inavumilika? Nani atamvumilia mwenzake?

  Hii ni kwa sababu, kama taarifa ambazo Kikwete alizikusanya zilikuwa na usahihi, lazima Masha angejua. Vinginevyo, Kikwete awe amekusanya taarifa zake kwa "njia za panya."
  Vilevile kama taarifa za Masha zingekuwa sahihi, hakukuwa na sababu ya kumiliki usahihi huo peke yake bila bosi wake kujua. Hali hii yaweza kuleta maana moja tu: kwamba mmoja wao anapokea taarifa za wapambe na huenda mitaani au zilizoandaliwa kwa nia mbaya.

  Kama maelezo ya Masha ndiyo sahihi, nani aliyesababisha Kikwete kupeleka taarifa tofauti ndani ya vikao vya chama chake?
  Taarifa ambazo rais alipeleka NEC na CC zimepitia kwa Masha? Je, waliomfikishia rais taarifa hizo walimueleza waziri kabla au baada ya kuzipeleka kwa rais? Je, rais baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wandani wake alimpelekea waziri wake taarifa alizopata? Naye waziri alizihakiki na kuthibitishia rais kuwa taarifa alizonazo juu ya Bashe hazikuwa na chembe ya mashaka?
  Je, inawezekana kila mmoja alificha taarifa zake ili aweze kumuumbua mwenzake katika vikao? Rais ana nafasi hiyo? Je, waziri ana fikra za kujiangamiza?

  Ambayo hayakutendeka ndiyo yangeonyesha umakini wa serikali; uthabiti katika kufikia maamuzi na ufasaha wa taarifa.
  Hayohayo ambayo hayakutendeka ndiyo yangeondoa kila chembe ya shaka na hata tuhuma za unafiki kutoka kwa wote wanaohusika. Hapa serikali ingeweza kuwa na hadhi mbele ya wananchi.Kwa hali ilivyo sasa, Kikwete analazimika kutoka hadharani na kuseme haamini waziri wake, na kwamba kuwepo kwake serikalini kumetokana na shinikizo kutoka nje.

  Lakini nani ataamini kuwa rais haamini waziri wake? Nani anaweza kuamini kuwa waziri wa mambo ya ndani – mjumbe katika vikao vya ulinzi na usalama – anakwenda kinyume cha aliyemteua? Uamuzi wa Masha wa kujitosa kutetea Bashe, hata kwa kauli zenye utata, unachukuliwa na wengi kuwa njia ya kuonyesha kuwa ana msuli wa nje kuliko wa ndani ya serikali ya Kikwete.
  Kwa upande mwingine, Bashe amenukuliwa akisema haivi na Ridhiwani, mtoto wa Kikwete. Hivyo inachukuliwa kuwa uamuzi wa Kikwete huenda ulilenga kumfurahisha mwanae.

  Bali kuna hili pia: Masha si mjumbe wa vikao vya CC na NEC ambamo Kikwete alisimamia Bashe kuenguliwa. Hivyo, Masha hakupaswa kumuandikia barua Bashe. Ingebidi kukiandikia chama chake na kumpa nakala Bashe. Badala yake, Masha amepeleka barua kwa Bashe na kunakiri barua yake hiyo kwa mtendaji mkuu wa chama, Makamba.
  Itachukua muda, si mfupi, kujua chanzo cha purukushani hizi na tabia inayoelekeza mwenendo mzima ambao wengi wanaita sasa kuwa maasi ya ndani kwa ndani.
   
 10. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #10
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Rage nae vp?
   
 11. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #11
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,054
  Likes Received: 4,619
  Trophy Points: 280
  Stop lying, acha umbea umbea, fanya kazi upate maisha bora au soma with all ur powers to be like Hussein Bashe....
  u seem to have some personal battle with Bashe......
  Acha upuuzi......

   
 12. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #12
  Sep 24, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Wacha Wafu wazike Wafu wao.
   
 13. p

  pilau JF-Expert Member

  #13
  Sep 24, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 1,523
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Kwa kweli muda wa kupitia neno hadi neno sina.... kuzungumzia uraia wa Bashe ni kurudi kinyumenyume.. alipogombea ubunge mlisema sio raia baada ya siku chache akaidhinishwa na Uhamiaji.. inaonekana kila ukifika wakati wa uchaguzi uraia wake unaingizwa walakini, uchaguzi ukiisha anakuwa raia safi... acheni majungu. ... mwenye akili timamu atajua dhahiri na wazi kwamba hapa kuna mkono wa mtu aliyetumwa na wabaya wake baada ya kupewa kitu kidogo kumharibia Bashe ......... nimewastukia
   
 14. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #14
  Sep 24, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,357
  Trophy Points: 280
  Wasomali wana tabia ya kutosahau asili zao..mwacheni apande to the highest position mje muone balaa lake,.rage katufundisha mengi
   
 15. Dotworld

  Dotworld JF-Expert Member

  #15
  Sep 24, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 3,929
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Dr. Kupeng'e  Maganga Masanja,
  NZEGA.
  TABORA
  +255786731566 (DSO)
  18th Sept. 2012

  Katibu Mkuu,
  Chama Cha Mapinduzi Makao Makuu DODOMA.

  Mheshimiwa,
  Yah: Taarifa Kuhusu Ndugu Husein Mohamed Bashe

  Tafadhali husika na kichwa cha barua hii hapo juu.

  Mimi ni mkazi wa Nzega na ni mwanachama hai wa CCM hapa Nzega. Nimeshuhudia na kusikia mengi yakisemwa kuhusu wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika chama hapa Nzega nikaona ni vyema kama mwanachama na kama raia mwema nikatoa taarifa nilizonazo ili mzifanyie kazi wakati mkiwajadili wagombea wa nafasi mbalimbali na pia mkajiridhisha kuhusu taarifa hizi ili mfanye maamuzi yanayofaa kwenye vikao vyenu. Mimi nimefuatilia swala hili kwa kusoma maelezo aliyoyachapisha Huseni Bashe kwenye mitandao na pia kuongea na baadhi ya wazee wa hapa mjini Nzega(walioipokea familia ya shehe Mohamed Ibrahim na mkewe) na kubaini ukweli ufuatao, pia nimesoma sheria ya uraia(The Tanzania citizenship act, principal legislation, Chapter 357 revised edition, 2002)

  Ndugu Husein Mohamed Bashe ama Husein Mohamed Ibrahim Bashir (tunashangaa kwa nini jina lake limekuwa likibadilika badilika – wengine wakidhani ni katika kutafuta uhalali wa kujiita Mnyamwezi kama nyaraka zake za kughushi Uraia zinavyoonyesha), ambaye anajulikana hapa Nzega kama mtoto wa Shehe Mohamed Ibrahim, alizaliwa Nzega Mnamo Tarehe 26/08/1975 (kumbukumbu rasmi za kuzaliwa kwake zinapatikana Ofisi ya Vizazi na Vifo, Nzega - kwenye cheti chake cha halali cha kuzaliwa; Shule ya Msingi Kitongo, Nzega, aliposajiliwa darasa la kwanza Mwaka 1984; na Chuo Kikuu Mzumbe alipodahiliwa kuanza masomo ya shahada ) na wazazi wake wote wawili wakiwa wasomali pure kutokea Somalia, na wote hawa hawakuwa Raia wakati Huseni akizaliwa. Baba yake Husein amepata Uraia 1987 kwa taratibu za kuomba kisheria. Mama yake Huseni anayejulikana kwa jina la Zainab Abdi hajawahi kuwa raia wa Tanzania na hajawahi kuomba na kupewa Uraia (hivyo anaishi nchini kinyume cha sheria).

  Kwa kuwa wazazi wote wawili wa Huseni hawakuwa raia wakati wanamzaa yeye na wadogo zake wote watano kwa mujibu wa sheria wote hawa si raia na wako ndani ya Tanzania kinyume cha sheria.

  Kama raia mwema nimepata taarifa kwamba kuna mtandao wa wasomali ambao wameingia nchini siku hizi na wametengeneza genge la kutafuta uhalali wa kuishi nchini hapa na kutawala nyanja mbalimbali za uchumi na jamii na hivyo nikahofia kwamba isije kuwa ndugu Huseni naye ni mmoja wapo uki zingatia amekuwa akifanya jitihada za kina na kwa kutumia nguvu kubwa sana ya pesa (ambazo hatujui anazipataje ukilinganisha na hali ya maisha ya familia yake na wazazi wake hapa Nzega) kutafuta ubunge na uongozi ndani ya chama tawala. Wengine hapa Nzega wamekuwa wakisema kwamba anatafuta ubunge kwa nguvu namna hii ili ahalalishe uraia wake wa uongo alionao na atafute namna ya kuingiza ndugu zake nchini Tanzania kwa kutumia nguvu ya kisiasa. Watu wengi wamepata mashaka hapa Nzega na kuna minong'ono kwamba anafadhiliwa na huo mtandao wa kiharamia wa kisomali wenye nia ya kutafuta namna ya kupenyeza watu wao kwenye system. Hili hasa ndiyo limenitisha na kunifanya niamue kutoa taarifa hii ili vyombo vya dola vilifanyie kazi na ukweli uthibitike.

  Mwaka 2005 aligombea Ubunge na alipewa alama ya D kwa sababu ya ‘utata' wa Uraia wake.

  Mwaka 2008 aligombea uenyekiti wa UVCCM Taifa na vikao vilimjadili na kuonyesha utata kwenye uraia wake, na hapo alikimbia kutengeneza kiapo cha kugushi cha haraka haraka cha kuthibitisha uraia wake.

  Watu wengi, na mimi nikiwemo tulibaki na mashaka yetu kwamba ni katika mazingira gani mtanzania wa kuzaliwa atalazimika kula kiapo kuthibitisha uraia wake? Hivi ni wangapi kati yetu wamewahi kufanya hivyo? Kwangu hili limekuwa likinipa mashaka makubwa na kunifanya niamue kufanya ufuatiliaji wa kina.

  Mwaka 2010 aligombea ubunge na alikatwa jina na vikao vya juu vya CCM kwa sababu ile ile ya ‘utata' kwenye uraia wake. Mwaka 2010 Waziri wa Mambo ya ndani Laurence Masha alithibitisha kwenye vyombo vya habari kuwa ndugu Huseni Bashe ni raia japokuwa hapa Nzega ambapo wanamfahamu ndugu huyu na chimbuko la familia yake toka wanaingia walibaki na mashaka yao. Hali hii na wasiwasi nilionao juu ya mtandao huu vimenifanya kuandika waraka huu ili kukiomba chama kitupe ukweli wa swala hili ni nini na pengine kumtaka Huseni Bashe, mama yake na wadogo zake wafuate taratibu za halali za kutafuta uraia wao.

  Hata hivyo pamoja na waziri wa mambo ya ndani kutoa uthibitisho huo kwenye vyombo vya habari hakumpa ndugu Huseni Bashe hati yoyote ile ya kumpa Uraia. Hivyo maneno yale yanabaki kuwa kauli ya kisiasa isiyo na mashiko yoyote yale kisheria kwa mujibu wa sheria hiyo niliyoitaja hapo juu.

  Kwa kuwa baba yake alipewa uraia tarehe 27/05/1987 baada ya kuishi kwa hati ya ukazi kwa muda mrefu na kuamua kuomba uraia na kufuata taratibu zote hakuna utata kwamba alikuwa raia wa Somalia kwa muda wote kabla ya hapo. Hata Huseni mwenyewe amejaza kwa kuthibitisha hili kwenye fomu yake ya kugombea Ubunge kuwa baba yake alizaliwa mwaka 1947 sehemu inayoitwa Buroa, Mkoa wa Buroa kule Somalia. Japokuwa maelezo yaliyopo kwenye mtandao aliyoyatoa kumshambulia mbunge wa nzega mheshimiwa dr. Kingwangallah anaandika hadithi tofauti kwamba baba yake alizaliwa Tabora mjini.

  Uraia wa mama yake unabaki kuwa ni swala lenye kuhitaji uchunguzi na uthibitisho. Huseni hutoa maelezo ya kwamba mama yake ni mnyamwezi wa Tabora jambo ambalo halikubaliki maana hata Kiswahili, achilia mbali kinyamwezi, hakifahamu vizuri na pia hata muonekano wake ni wa kisomali bila shaka yoyote. Kwa maelezo ya Husein Bashe kwenye andiko la kashfa kwa mbunge wa nzega dr. kingwangallah anadai kuwa wazazi wa mama yake ni wazaliwa wa Tanzania, Sumbawanga (Baba yake na Mama Husein) na Boma Ng'ombe (bibi yake na mama Husein) kwamba walichagua uraia wa Tanzania kutoka ule wa Somaliland wakati wa Uhuru lakini hakuna kumbukumbu hata moja kuwa waliandikwa kwenye rejista ya raia wa Tanzania waliosajiliwa kama ‘aliens' kwa mujibu wa sheria iliyokuwa inatambua uraia wa kuandikishwa, yaani ‘citizenship by registration' ya watanzania minorities wakati tukipata uhuru. Habari hizi zinaonekana ni za uongo kwa kuwa tayari tuna ushahidi wa cheti cha kugushi cha mama yake na mama Husein Bashe (aliyejulikana kwa jina la Amina bint Ahmed) na tuna taarifa kwamba babu yake kizaa mama na Husein alitokea kijiji cha Belibeli kule Somaliland akiingia Tanzania na mkewe bi Amina na watoto (akiwemo mama Husein – Zainab bint Abdi).

  Alichokifanya Huseni Bashe ili apate Uraia

  Kwa mujibu wa sheria ili upate uraia wa Tanzania ni lazima uwe umeishi nchini kwa kibali cha ukazi na umeishi kwa kipindi kisichopungua miaka 10, saba kati ya hiyo uwe umeishi mfululizo huku ukiwa mwema na mwenye faida kwa nchi kijamii ama kiuchumi (second schedule, conditions for citizenship by naturalization, section 9(1) ya sheria niliyoitaja hapo juu) . Na maombi hayo yanaanzia kwenye kata unayoishi (kanuni namba 8 iliyomo kwenye Tanzania citizenship regulations (section 28)) pia alitakiwa mwombaji (Huseni Bashe) kutangaza kwenye magazeti ya kila siku kwa siku 2 zinazofuatana (kanuni ya 3 ya kanuni nilizozitaja hapo juu). Mpaka naandika hapa hakuna gazeti wala mtu hata mmoja katika niowahoji aliyekumbuka kuona tangazo la namna huyo kumhusu Husein Bashe.

  Kwa kufuata utaratibu huu unaoelekezwa na sheria na kanuni zake alijua angepoteza matumaini ya kuingia kwenye siasa mapema na ingewezekana kuwa ndiyo ukomo wake kabisa. Aliamua kutafuta njia fupi ya kupata uhalali wa uraia wake kwa kugushi hati za kuzaliwa za mama yake mzazi na za bibi yake kizaa mama (ambazo naziambatanisha hapa). Kwa kufanya hivi alijua atapata uhalali wa kutumia kipengele cha sheria kinachosema kama mzazi wako mmoja ni mtanzania na wewe umezaliwa Tanzania basi unaukana tu uraia wa mzazi mmoja ambaye hakuwa mtanzania wakati unazaliwa. Hivyo alipata mwanya wa kuukana uraia wa baba yake na kudai amebaki na uraia wa mama yake (ambaye alidai kuwa ni mnyamwezi na hata kwenye hati ya Husein Bashe inaonekana hivyo).

  Hati ya kuzaliwa ya mama yake mzazi na Husein Bashe ninayo kivuli chake na nitakiambatanisha na barua hii pia cha bibi yake. Vyeti vyote hivi ni vya kugushi na hili tumelithibitisha RITA. Cheti cha mama yake Huseni Bashe kina taarifa zifuatazo:- No. of Entry 3032, Namba ya cheti A. 17404 na kimesainiwa na L. M. Manson tarehe 14/02/1984, kimetolewa wilayani Tabora, na kinadai mama yake Husein Bashe, mwenye jina la Zainab bint Abdi alizaliwa Government European Hospital na ni wa kabila la Isihakia kutokea Somalia. Na kile cha Bibi yake Husein Bashe kina No. of entry 3508, na namba ya cheti A 17399, na kimesainiwa na A. B. Hodgson, kimetolewa wilaya ya Moshi tarehe 14/02/1984, amezaliwa Boma la Ng'ombe, na jina lake ni Amina Binti Abeid, na ni wa kabila la Isihakia. Jambo la kuvutia ni kwamba kwenye vyeti vyote hivi aliyesaini ni mtu mmoja (japokuwa ni mikoa miwili tofauti na siku moja).

  Mbali na RITA kukana kutokuvitambua vyeti hivi kuna kila alama ya kugushi kwenye nyaraka hizi kwanza vyote vimesainiwa na kutolewa siku moja, na mtu mmoja kwenye mikoa tofauti na serial number za kufuatana (17404 na 17399!) pia walioandikwa kusaini wana majina tofauti yanayoonesha kuwa ni foreigners (Manson na Hodgson). Watu wenye majina hayo hawajawahi kuwepo Tabora wala Moshi. Pia hakujawahi kuwa na hospiali yenye jina hilo lililotajwa hapa Tabora na ni kitu kisichowezekana kwa ofisa wa serikali kukosea jina la Boma Ng'ombe na kuandika Boma la Ng'ombe pia kuandika kwamba ipo wilaya ya Moshi badala ya wilaya ya Hai.

  Uchunguzi wangu umebaini kuwa mama yake hakuzaliwa Tanzania na kwamba aliingia Tanzania kupitia Rundugai akiambatana na wazazi wake na wajomba wa Huseni Bashe (mmoja yupo Dodoma – maarufu kama Charles mnene, na ambaye alinipa historia hii bila kujua ninachokifanya) wakati huo mama yake mzazi Husein akiwa na umri wa miaka 8/9.

  Alitafuta njia fupi ya kujipatia uraia ili kukwepa mlolongo wa taratibu kwa sababu za kisiasa. Kiuhalali – alitakiwa alipofikisha umri wa miaka 18 aanze kuishi kwa kibali cha ukazi kwa kipindi cha miaka 10 ndipo afanye maombi yake rasmi ya kupatiwa Uraia jambo ambalo lingemnyima sifa ya kugombea uenyekiti wa UVCCM Taifa mwaka 2008, hivyo alikwepa akapita njia fupi. Sasa kwa kufanya hivyo amevunja sheria kwa kugushi nyaraka za uraia za mama na bibi yake na ana kosa la kujibu kisheria, yeye na pamoja na bibi na mama yake.

  Anachotakiwa kufanya kwa sasa kuhusiana na Uraia wake

  Anatakiwa kuomba kibali cha ukazi na aishi kwa kipindi cha miaka 10, 7 kati ya hiyo ikiwa ni ya mfululizo na akiwa ni mtu mwema na mwenye faida kwa nchi kijamii na kiuchumi ndipo afanye upya maombi ya uraia.

  Tabia ya kugushi nyaraka na taarifa mbalimbali

  Amekuwa akidanganya umri wake kwa kuwa na siku mbalimbali za kuzaliwa – ushahidi ni taarifa alizojaza kwenye fomu mbalimbali za kugombea nafasi za Uongozi kwenye chama, mfano mwaka 2005 alipogombea ubunge alijaza amezaliwa mwaka 1976, mwaka 2010 alipogombea ubunge alijaza kuwa amezaliwa mwaka 1978. Pia mwaka 2007 alikuwa anagombea Ujumbe wa Halmashauri kuu ya Mkoa alijaza kuwa amezaliwa mwaka 1977. Siku yake ya kuzaliwa imekuwa ikibadilika badilika kutokana na mahitaji ya wakati huo. Siku yake ya kuzaliwa ilibadilika ili apate fursa ya kugombea UVCCM mwaka 2008 (kwa kushusha umri wake akidhi vigezo) na tarehe hiyo inapatikana pia kwenye kiapo chake cha Uraia anachotumia (hivyo nacho ni batili) na pia kwenye kitambulisho chake cha mpiga kura (kama inavyoonyesha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura). Ukitaka kuamini kuwa amedanganya umri linganisha taarifa hizi na za mdogo wake aliyemuachia ziwa anayejulikana kwa jina la Ismail Mohamed, ambaye naye amezaliwa mwaka huo huo wa 1978. Kiapo chake cha uraia kilipatikana tarehe 24/09/2008 akiwa na umri wa miaka 30, umri ukiwa ni wa uongo kwa kuwa alikuwa amefoji vyeti vya kuzaliwa.

  Pia mwaka 2005 akigombea Ubumbe aliandika kuwa ana digrii mbili, ya kwanza ya Mzumbe nay a pili
  (MBA) ya UNISA, ambayo hakuwa nayo na mpaka leo hii hana.

  Pia amewahi kufukuzwa kazi sehemu mbalimbali kwa udanganyifu:- alidanganya NMB benki kuwa anaumwa kumbe amelala nyumbani kwa uvivu wa kwenda kazini. Bosi wake alipozidi kumtafuta na aliposikia kuwa kuna hatari ya kufukuzwa kazi aliamua kutafuta daktari wa uongo ili amfunge POP ndipo akaenda kuripoti huku akiwa anatembea akichechemea kwa msaada wa magongo mpaka kwa bosi, watu wakampa pole nyingi pale ofisini. Alipoingia na kumueleza bosi wake kuwa hakuja kazini kwa sababu alivunjika mguu bosi alimhoji kwa nini hakuchukua seek sheet na kwa nini hakutoa taarifa, akashindwa kujibu. Pamoja na hali aliyokuwa nayo bosi aliamua kumkabidhi barua ya kumfukuza kazi; Husein alilia sana na kisha akatupa magongo akaondoka bila kuchechemea tena kama alivyoingia. Watu wakashangaa na kuangua vicheko. Pia amewahi kufukuzwa kazi pale Celtel kwa kosa la uzembe na kutokuweka sawa hesabu zake. Amewahi kufukuzwa kazi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya pesa na kampuni nyingine ya wazungu wa Afrika Kusini iliyokuwa inatengeneza kadi za mabenki.

  Haya ni baadhi ya mambo niliyoweza kukusanya dhidi ya mtu huyu ambayo nadhani mnahitaji kuyajua ili kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi. Je ni kweli Tanzania inahitaji kuongozwa na vijana wa namna hii?

  Natanguliza shukrani zangu za dhati nikitarajia mtu huyu atapata anachostahili. Wako mtiifu,


  Maganga Masanja (kwa sababu za kiusalama nimeficha jina halisi ila ukitaka kunipata kwa maswali ama kwa ushahidi fika kwa DSO Nzega na mimi nitajitambulisha pale)

  Mwanaccm Mwaminifu, Nzega.
  Nakala:

  1. Mwenyekiti wa CCM – Kwa taarifa
  2. Naibu Katibu Mkuu, Mh John Chiligati (Mb.) – kwa ufuatiliaji (maana amekuwa akikutaja kwenye hotuba zake kwamba ulimsingizia kwa chuki zako)
  3. Mwenyekiti wa CCM (M) Tabora – kwa taarifa
  4. Katibu wa CCM (M) Tabora – kwa ufuatiliaji na uthibitisho
  5. Mkurugenzi Mkuu Usalama wa Taifa – kwa uchunguzi wa kina na uthibitisho
  6. Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU – kwa uchunguzi wa kina na uthibitisho
  7. Msajili wa vyama vya siasa – ndugu John Tendwa – kwa ufuatiliaji wa hatua zitakazochukuliwa na chama cha mapinduzi
  8. DPP – kwa upelelezi na hatua za kisheria
  9. DCI – kwa upelelezi na hatua za kisheria
  10. Kamishna Mkuu Uhamiaji – kwa upelelezi na hatua za kisheria
  11. Waziri wa mambo ya ndani ya nchi – kwa taarifa
  12. Uhamiaji, Nzega – kwa taarifa
  13. Usalama wa Taifa, Nzega – kwa taarifa
  14. Mbunge Nzega – kwa taarifa
  15. DC Nzega – kwa taarifa
  16. CCM Nzega – kwa taarifa


  ===

  Attachment 1:

  [​IMG]


  ===

  Attachment 2:


  [​IMG]  ===

  Attachment 3
  [​IMG]

  [​IMG]

  Attachment 4:
  [​IMG]

  .
  [​IMG]

   

  Attached Files:

 16. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #16
  Sep 24, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,354
  Trophy Points: 280
  chama cha hovyo hata definition ya uraia na uzalendo hawaijui
   
 17. T

  Tata JF-Expert Member

  #17
  Sep 24, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,730
  Likes Received: 646
  Trophy Points: 280
  Huyu Maganga Masanja ni kiboko. Inaonekana ametumia muda wa kutosha na pesa kufanya utafiti wa kuthibitisha uraia wa Bashe. Kama yaliyosemwa ni ya kweli, basi nchi hii tuna safari ndefu sana katika kupambana na ufisadi. Huyu ni kiongozi mtarajiwa na ameghushi nyaraka kwa kiasi kikubwa. Ina maana akipata uongozi hatasita kughushi nyaraka kwenye mambo ya kitaifa ili apate faida binafsi.
   
 18. F

  FJM JF-Expert Member

  #18
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Huu ni uhuni. Bashe ni raia halali kwa mujibu wa taratibu na sheria za uhamiaji Tanzania. Sijui kwa nini watu wanaendeleza hizi porojo za kizamani. Wanashindwa kupambana na huyo kijana kwenye ulingo wa siasa, sasa wanajificha kwenye uraia wake! Very sad!
   
 19. T

  Tata JF-Expert Member

  #19
  Sep 24, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,730
  Likes Received: 646
  Trophy Points: 280
  Pilau acha uvivu wa kusoma. Kama ni njaa inakusumbua nakushauri upate "Pilau" kwanza kisha utulie na kupitia neno hadi neno katika barua hiyo. Kuna mambo mazito yameandikwa ambayo, ikiwa yana ukweli, yanaeleza kwa kina kiwango cha uadilifu wa Bashe na kama anastahili kuwa kiongozi wa kitaifa. Huyu jamaa haongei tu siasa bali ameweka vielelezo vya kuthibitisha kuwa Bashe siyo raia halali wa nchi hii.
   
 20. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #20
  Sep 24, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mwandishi ana kiwango kikubwa sana cha kujiamini; huo kwangu ndio uzalendo
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...