Watanzania wenzangu, tufike mahali tukatae kwa nguvu zote ubabaishaji na uhuni wa aina ya Bashe. Kwa mfano hata kama kisheria Bashe angeweza kuwa raia wa Tanzania lakini kwa mambo aliyofanya ni wazi ameonesha HANA MAADILI wala SIFA za uongozi.
Mfano ni viambatanisho vilivyoko hapa. Chukulia mathalan Kiambatanisho Namba 4. :-
- Hapa Bashe alisoma elimu ya sekondari 1991-1998, jumla ya miaka 8 kwa nini?
- Miaka yake ya kuzaliwa pamoja na majina tofauti tofauti anayotumia sehemu tofauti tofauti
- Baba yake alizaliwa 1928 au 1947? Na je ni Msomali au Mtanzania?
Narudia tena rai yangu, Watanzania tufike mahali tukatae kwa nguvu zote aina ya watu wa Bashe, hata kama ni genius wa aina gani. Uhuni huu umelifikisha Taifa hapa lilipo. Uhuni huo huo umeifikisha CCM kaburini. Kama CCM inakufa kwa sababu ya aina ya mambo kama haya basi na Taifa hili pia linaweza kuangamia kwa gonjwa hilo hilo.