Uhamiaji Tanzania: Bila dhumuni la safari hakuna kupewa pasi ya kusafiria (Passport)

Nikiambatanisha kiambata cha usa lottery kinachotaka nijaze taarifa za passport kabla sijatuma maombi kitakubalika?
Uhamiaji jibuni hili Marekani Lottery hii iko kisheria .Passport mtatoa au mtabania?
 
Ilikuwa hivo ila inatakiwa ibadirishwe sehemu. Mfano una sababu ya kusafiri mfano unaenda kutembea tu Kenya au kukutana na rafiki yako Kenya au nchi yoyote bado wanakudai uoneshe barua ya mwaliko wa huko unakotaka kwenda.
 
Ushapata hiyo lottery au unamaanisha tangazo tu la hiyo bahati nasibu?
Jamaa watataka barua ya mualiko na sio tangazo la fursa, ila kanyooshe mkono wako mkuu utaipata kirahisi tu.
Fomu inatakiwa kujaza kabla kupata lottery Visa inataka ujaze passport number je passport watatoa?
 
Fomu kujaza kabla kupata inataka ujaze passport number passport watatoa?
Passport hawatatoa kisa kuna lottery visa, uhamiaji kuna upuuzi mwingi mno na kama hicho kingekuwa kigezo basi kila 18+ mwenye elimu ya high school angekuwa ashaikamata kwa kisingizio cha kuomba lottery
 
Ushapata hiyo lottery au unamaanisha tangazo tu la hiyo bahati nasibu?
Jamaa watataka barua ya mualiko na sio tangazo la fursa, ila kanyooshe mkono wako mkuu utaipata kirahisi tu.
Mwisho wa kuingia hiyo lottery kwa 2021 ni September 30.

Hivyo huwezi kuanza taratibu za kutaka passport sasa hivi wakati hata lottery hujashinda.

Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi ni kwamba unaposhinda lottery ndo wabeba documents zote kuomba passport UHAMIAJI ukiwa na vielelezo vyote, kisha wenda US embassy kuomba visa ya kuingia US, ukiwa na vielelezo vyote ikiwemo confirmation ya Green card.

Hii nimeona baadhi ya closed friends wakihangaikia haya makitu.

Hivyo basi, passport waomba uhamiaji ukiwa na vielelezo vyote ikiwemo email ya wewe kupata green card.

UHAMIAJi hawawezi kukunyima passport ukiwa na vielelezo vyote hivyo.
 
Hawa Maafsa wa hiyo idara wanaamini kuwa wako kwa ajili ya Raia wanaohamia hapa au kuja kufanya kazi hapa ila sio Raia wetu ambao wanataka kutoka kwenda kutafuta maisha Nje
 
Ndio tumefika huko? Sitaki kuamini! Lakini haitashangaza ndani ya utawala huu hili kutokea.
Kimsingi sheria ya uhamiaji ilikuwa hivyo siku zote toka nchi ipate uhuru/ Nyerere system aka Ujamaa/bin ukomunist. Ila kwa sababu siku za nyuma shughuli hizo ziliwezekana kupitia Hongo ndio maana sheria hizi hazikujulikana.

Kimsingi sheria zetu nyingi ni za wakati wa ujima ni lazima zibadilishwe. Mpaka tuna bunge la kijani tupu, sahau mabadiliko hayo. Bado tutasubiri sana!

Kifupi sijakueleza sheria za Ardhi zilivyo hovyo, uchaguzi, elimu, ajira n.k. Kimsingi kila moja kati ya hayo ni mpaka yakuguse ndio joto utalihisi ukali wake. Alamsik.
 
Hapa ndipo tatizo kubwa la double work both kwa mteja na uhamiaji ambayo ni unneccessary ni kuongeza tu bureaucracy

Digital System ya uhamiaji ya kuomba passport ilitakiwa kupunguza kazi na bureacracy ila imeongeza kazi sababu zamani.ilikuwa manual unapeleka huo mzigo wote manual unapitiwa unapewa passport.Sasa hivi ni combination of both digital na manual mtu apitie digital halafu apitie tena manual hard copy documents!!! any way that is not my big concern.Concern yangu hilo la issue ya visa ya USA ondoeni kwenye dawati lenu waachieni ubalozi wa USA watoa hiyo Lottery Visa .Nyie toeni tu passport hayo ya Lottery Visa sijui nini waachieni ubalozi wa Marekani.Document za mambo ya Visa msi include kwenye sharti la kumpa mtu passport nyie sio ofisi za ubalozi.Msijikweze kupitiliza na kujiongezea kazi bure bila sababu.Mfanyakazi wa immigration anarudi nyumbani ohhh leo nimechoka sana nilikuwa napitia makaratasi ya watu kuwa wanaenda nchi gani kufanya nini ili ni saini wapate passport aaaah nimechoka kama nini!!!! tired kwa kazi ambayo is non of your business!!! Ni ya balozi!!!

Wewe toa Passport ya visa requirenents waachie wengine ambao ni mabalozi wa nchi za nje
 
Ukweli ni kuwa swala la passport kwa Tz limewekwa kama jambo la ajabu sana,,, ila nchi za wenzetu ni kitu watu wanapewa kama ID tu... sio biG issue sana...

Tatizo wabongo wazamiaji sana,, wahuni wengi so wakitoa tu passport bila vikwazo kuna watu watazitumia ndivo sivyo...

JPM mitano tena... Alisikika Polepole akizungumza kutokea Chato.
 
Hua kuna sharti lingine linaitwa "show money"...yaani ili Uhamiaji waamin utakwenda ng'ambo na utarudi wanataka uwaoneshe fedha za kutosheleza safari. Hapo ndo kazi ilipo
Hilo swali ni la ubalozini unakoomba VISA sio la uhamiaji wanaotoa passport kuliuliza it is non of their business lakini kwa ubalozini liko Ok
 
Tatizo wabongo wazamiaji sana,, wahuni wengi so wakitoa tu passport bila vikwazo kuna watu watazitumia ndivo sivyo...
Omba sanmahani kwa wazamiaji tafadhali.Mtu hawezi zamia kama ana passport na upatikanaji wa passport ni rahisi!!! ukiwa mgumu ndipo nchi huzalisha wazamiaji wengi mfano ni Ethiopia na Tanzania
 
Sasa utaombaje passport kama huna matumizi nayo?

Si unakua na mpango wa safari ndio unatafuta passport!? Au nakosea ndugu zangu
Huo ni ujima, nchi za watu huko passport ni kitu muhimu kiasi kwamba kila mtu anayo,
Chukulia majanga yametokea kama mafuriko au vita hao wenye passport ndo watapata rescue kwanza kabla ya wengine,
Uhamiaji hawana budi kubadilika watoe passport kwa muhitaji, mwingine anataka ufadhili wa kimasomo hawezi kupata bila passport wenzetu wanaenda mbele sisi tunarudi nyuma
 
Watoe tu kama njugu Ili kukuza mapato
Kukuza mapato hilo ni namba moja lakini pili ninkuiondia Tanzania kwenye aibu ya kila siku kurudishiwa wahamiaji haramu nchi za watu wasiokuwa na passport kutokana na wao kushindwa kupata passport Tanzania kwa sababu ya ujeuri wa vigezo vigumu vya idara ya uhamiaji

Sasa hivi ushauri kwa serikali mhamiaji yeyote haramu akishikwa nje na hana passport na akisema tatizo vigezo vya kupsta passport vilimshinda vikiwemo barua ya mwaliko na anaenda fanya nini.Maafisa uhamiaji wawajibishwe ikiwemo kustaafishwa na kutumbuliwa wao ndio wanasababisha tatizo la wahamiaji haramu wasio na passport nchi za watu na kuipa nchi image mbaya kimataifa Sababu unakuta wamerudishwa nchini sio sababu wamefanya uhalifu kule ila ni kuwa hawakuwa na passport!!! Si kuwa walikaba mtu au kupora au kuua au ujambazi ndio maana huwa tu deported

Kitengo cha passport kinaharibu jina la Tanzania nje kwa kuzalisha wahamiaji haramu wasio na passport
 
Tatizo wabongo mkienda nje ya nchi hamrudi!!! Tena mnabadiri kabisa na ukoo!! Achilia mbali kuukana utanzania wako!!

Asa sisi bongo hawa watu tulio nao hawatoshi! Tutapata wapi kodi? Nguvu kazi bin watumwa?
Watu kuingia Tz ni rahisi sana kuliko watanzania kutoka humo nchini.

Nje kuna raha bana weee!! Hasa ukisha pata uraia wa nchi nyingine!!!?? Heee! Uko unakuja tena unasahau na kiswahili kabisaaa
Navowajua watu wa mbagala hawatakubali kurudi mbagala!!!piga ua...

Wakirudi Tz kwa bahati mbaya wanaona km watakataliwa kurudi tena nje ya nchi walizotoka!!!

Elimu nje ni rahisi sana.km Ukiomba Mungu akusaidie.ukiona mtu amerudi kukaa bongo kabisa na kusahau basi huyo...
Ameitwa kichawi au

ana nia ya uongozi ubunge au

Fursa ya mkopo wa kibiashara au

Baba zao wana mahela meengi na mali nyiingi km Ndesamburo!! Mbowe!!! Dr Manyonyi! Au

Kamata shavu uwaziri, Ameitwa na mshikaji.au katonywa labda!!
pia km akiukosa anarudi ulaya. Ndo jumla.

Au awe na tatizo la kiafya km pumu au mwili wake una allergy hapendi ubaridi baridi anakuwa km anaumwa vile..

Wajanja wooote km Iraq.Nigeria.ethiopiana nk wanakimbilia nje ya nchi zao tena kwa miguu bila pass!
wakienda ni mazimaaa kurudi labda uwaroge!!!
Wako tayari wafungwe nje! Waishi km wafungwa kuliko kukaa Bongo land huru. wewe! chunguza utaona ukweli huu!!!
 
Omba sanmahani kwa wazamiaji tafadhali.Mtu hawezi zamia kama ana passport na upatikanaji wa passport ni rahisi!!! ukiwa mgumu ndipo nchi huzalisha wazamiaji wengi mfano ni Ethiopia na Tanzania

Mkuu unajua vitu vingapi mtandaoni vinavohitaji passport namba?
 
Siruhusiwi kusema "I know how you feel", lakini uhamiaji nao wamekuwa kama TRA kusumbua wananchi.

Nafikiri wamemwelewa naibu waziri juzi amewapa somo kuhusu kughulikia maombi.

Hii nchi inahitaji "dose" kubwa ya kutibu magonjwa yaliyopo, urasimu, wizi, ubadhilifu na usumbufu kwa wananchi uso lazima.
 
Mkuu unajua vitu vingapi mtandaoni vinavohitaji passport namba?
Vingi tu mimi nimetoa vichache Passport is no.longer a travel document only kwenye utandawazi ni cheti cha NDA cha kimataifa hata kama mtu hasafiri

Ukikutana na mtu wa nje ndani ya Tanzania akikuomba kitambulusho kwa serious business deal hataki kitambuñisho Cha NIDA anataka paddpiry sababu passport inabeba information zote kuanzia za NIDA kwa hiyo iko more realiable kuliko kitambulisho cha NIDA na yaweza kuwa verified kwa finger prints anywhete in the world .TOFAUTI na kitambulisho cha NIDA ambacho mwisho wa kutambuliwa ni ndani ya Tanzania kwa watanzania tu walioko Tanzania sio wageni.

Kwenye utandawazi kitambulisho reliable ni pasdport tu

Hata ukutane na mzungu barabarani unasema tushirikiane business atakuuliza do ypu have a passport give me anatoa photocopy atakako verify anajua mwenyewe ndio baadaye anakurudia anakwambia ok let us talk business.
 
Back
Top Bottom