Serikali yangu ya CCM naipongeza kwa jitihada za kuimarisha usalama wa wananchi na mali zao
Hivi wewe una passport kweli ? Au wewe uraia wako ni humu Jf .....
Mradi wa Passports Mpya.
Mradi Vitambulisho vya kupigia kura vipya.
Mradi wa vitambulisho vya mkazi/uraia kupitia NIDA.
Halafu miradi yote hiyo ya mabillioni ya shillings hupamba moto pale tu uchaguzi unapokaribia,uchaguzi ukiisha kimyaaa!!!
CCM wanabaka uchumi wa Taifa hili kwa mbinu nyingi sana,zabuni ya hiyo miradi yote itapitia tu mikononi mwa makampuni ya kihindi lakini kati kati yenye venture na kampuni za makada wa CCM,ni aina nyingine tu ya EPA!!!
Mnasema ni mawakala wenu ndiyo wanafanya udanganyifu....wakati huo huo mnasema ninyi hamuhusiki...(Au mmi kwenye red ndiyo sijaelewa?)
Wengine wanapotaka pasipoti hawafiki huku, wanaishia kwa wale mawakala wetu, wanadanganywa kule, kule mtu anamwambia nipe labda laki tatu, nitakutafutia utapata, kitu ambacho hana uwezo nacho.
Matokeo yake wanakuja kulalamika kuwa wameibiwa, na hii ni kutokana na watu kutaka mambo ya haraka, na imani walizo nazo kuwa wakija huku ni lazima watoe rushwa, hiyo kwetu haipo.....
Chanzo: Nipashe
Sababu za mabadiliko last time ilikuwa kuendana na mfumo wa kimataifa passport iwe readable kwenye database kimataifa, zoezi hilo lilifanyika kwa ufasaha na kwa ufanisi na sinazomeka po pote duniani. Hili la sasa halina uzito wa kutosha vinginevyo kuna ajenda nyuma ya pazia isiyowekwa wazi hadharani.
Mkuu nakubalina na wewe.
Kwakifupi, sababu kuu alizotoa:-
· Hali yaudanganyifu katika kuwasilisha vitu vinavyohitajika wakati wa kupata hati
· Matumizi mabayaya hati
· Watu kutumiamawakala (vishoka) kuwatafutia pasi.
Sasa kubadilisha pasi itakuwaje suluhisho la hayo matatizo yaliyotajwa hapo juu?
Wanachotakiwa kufanya ni kuendeleakutoa elimu kwa watumiaji kuhusu matumizi sahihi ya pasi, na kuhakikisha kuwavishoka na wafanyakazi wasio waaminifu wanakamatwa na kuchukuliwa hatua kali zakisheria.
Kubadili pasi kutokana na hizo sababu walizotoa ni matumizi mabaya ya pesa zetu za kodi.
Bi Burhani anasema, watu wanawatumia vishoka waliopo wizarani. Hee, kumbe anajua kuna vishoka! sasa suluhu ni kubadili hati au kutokemeza vishoka anaowajua.Mbona hizo sababu ni za ovyo .Sasa ukibadili ndio utazuia wizi?Nilidhani kuna maboresho
Tena zoezi hilo ni la kijuha na ni matumizi mabovu ya kodi zetu.Hizo sababu hazitoshelezi serikali kutumia kodi tetu kubadili passport.
Kuna mawili Kati ya haya;
Idara ya uhamiaji imejaa mbumbumbu
Au kuna ajenda ya siri ambayo itaishia kwenye ufisadi
Huku ni kutengeneza ulaji tu, sbabu hazitoshelezi. Hii awamu itatumaliza kabla haijatoka
Nakubaliana nawe hoja ya kubadili hati za kusafiria haina uzito. Jambo la msingi linalotakiwa kufanyika ni kuziba na kuwachukulia hatua wale wanaotifua zoezi kwanda kwa utaratibu unaotakiwa. Na wanaofanya hayo wanayolalamikia ni wao wenyewe na ofisi husika.
Huna tofauti na huyuSerikali yangu ya CCM naipongeza kwa jitihada za kuimarisha usalama wa wananchi na mali zao