Uhamiaji kubadilisha tena hati za kusafiria

Hizo sababu hazitoshelezi serikali kutumia kodi tetu kubadili passport.
Kuna mawili Kati ya haya;
Idara ya uhamiaji imejaa mbumbumbu
Au kuna ajenda ya siri ambayo itaishia kwenye ufisadi
 
Serikali yangu ya CCM naipongeza kwa jitihada za kuimarisha usalama wa wananchi na mali zao

Huyu mpuuzi hajui chochote anapongeza ujinga hajawahi kwenda hata kenya.

Sisi tuliozoae kusafiri kila Mara kwenye mataifa makubwa tunaona ni upuuzi tu wa kupata hela Za campaign mwakani
 
Mradi wa Passports Mpya.

Mradi Vitambulisho vya kupigia kura vipya.

Mradi wa vitambulisho vya mkazi/uraia kupitia NIDA.

Halafu miradi yote hiyo ya mabillioni ya shillings hupamba moto pale tu uchaguzi unapokaribia,uchaguzi ukiisha kimyaaa!!!

CCM wanabaka uchumi wa Taifa hili kwa mbinu nyingi sana,zabuni ya hiyo miradi yote itapitia tu mikononi mwa makampuni ya kihindi lakini kati kati yenye venture na kampuni za makada wa CCM,ni aina nyingine tu ya EPA!!!

Bravo MoudyBoka...
 
Kubadilisha passport kwa sababu zilizotolewa si suluhisho.Tunajua kuwa kuna sababu za msingi na za kimataifa kupelekea kwenye e-passport na maamuzi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutekeleza matakwa hayo. Hii ndiyo ingetolewa kama sababu kuu, lakini siyo hiyo iliyoandikwa.
 
Sasa hili balaa hebu tuwekeni sawa sisi tunaobeba box huku itakuaje maana tupo baadhi tunatumia passport za kitanzania.
 
Mbona hizo sababu ni za ovyo .Sasa ukibadili ndio utazuia wizi?Nilidhani kuna maboresho
 
CCM imeamua kukusanya pesa za kampeni kwa hiyo ngojeeni muone yatakayo tokea .Maana CCM bila kuhonga hakuna kitu , matokeo ni hayo sasa siku mambo mapya .Kwa nini mwaka huu na ghafla hivi ?

Kuna ukweli katika maelezo yako. I concur
 
Serikali itueleze namna passport mpya zitakavyozuia vishoka! Kwani serikali haijui kuwa vishoka ni hao hao watumishi wa uhamiaji?! Isitoshe mbona hizo passport za vishoka zinasomeka bila taabu yo yote katika computer?
 
Hapa watu wanatafuta ulaji, tatizo halipo kwenye passport ila Uhamiaji maana wanauza passport kwa wale ambao si raia sasa hata mkitengeneza za chuma hazitofaa.
 
Membe.jpg
images
images


“Wengine wanapotaka pasipoti hawafiki huku,
wanaishia kwa wale mawakala wetu, wanadanganywa kule, kule mtu anamwambia nipe labda laki tatu, nitakutafutia utapata, kitu ambacho hana uwezo nacho.

Matokeo yake wanakuja kulalamika kuwa wameibiwa, na hii ni kutokana na watu kutaka mambo ya haraka, na imani walizo nazo kuwa wakija huku ni lazima watoe rushwa, hiyo kwetu haipo.”....

Chanzo: Nipashe
Mnasema ni mawakala wenu ndiyo wanafanya udanganyifu....wakati huo huo mnasema ninyi hamuhusiki...(Au mmi kwenye red ndiyo sijaelewa?)
 
Sababu za mabadiliko last time ilikuwa kuendana na mfumo wa kimataifa passport iwe readable kwenye database kimataifa, zoezi hilo lilifanyika kwa ufasaha na kwa ufanisi na sinazomeka po pote duniani. Hili la sasa halina uzito wa kutosha vinginevyo kuna ajenda nyuma ya pazia isiyowekwa wazi hadharani.

Mkuu nakubalina na wewe.
Kwakifupi, sababu kuu alizotoa:-
· Hali yaudanganyifu katika kuwasilisha vitu vinavyohitajika wakati wa kupata hati
· Matumizi mabayaya hati
· Watu kutumiamawakala (vishoka) kuwatafutia pasi.
Sasa kubadilisha pasi itakuwaje suluhisho la hayo matatizo yaliyotajwa hapo juu?

Wanachotakiwa kufanya ni kuendeleakutoa elimu kwa watumiaji kuhusu matumizi sahihi ya pasi, na kuhakikisha kuwavishoka na wafanyakazi wasio waaminifu wanakamatwa na kuchukuliwa hatua kali zakisheria.

Kubadili pasi kutokana na hizo sababu walizotoa ni matumizi mabaya ya pesa zetu za kodi.
 
Mkuu nakubalina na wewe.
Kwakifupi, sababu kuu alizotoa:-
· Hali yaudanganyifu katika kuwasilisha vitu vinavyohitajika wakati wa kupata hati
· Matumizi mabayaya hati
· Watu kutumiamawakala (vishoka) kuwatafutia pasi.
Sasa kubadilisha pasi itakuwaje suluhisho la hayo matatizo yaliyotajwa hapo juu?

Wanachotakiwa kufanya ni kuendeleakutoa elimu kwa watumiaji kuhusu matumizi sahihi ya pasi, na kuhakikisha kuwavishoka na wafanyakazi wasio waaminifu wanakamatwa na kuchukuliwa hatua kali zakisheria.

Kubadili pasi kutokana na hizo sababu walizotoa ni matumizi mabaya ya pesa zetu za kodi.

Nakubaliana nawe hoja ya kubadili hati za kusafiria haina uzito. Jambo la msingi linalotakiwa kufanyika ni kuziba na kuwachukulia hatua wale wanaotifua zoezi kwanda kwa utaratibu unaotakiwa. Na wanaofanya hayo wanayolalamikia ni wao wenyewe na ofisi husika.
 
Mbona hizo sababu ni za ovyo .Sasa ukibadili ndio utazuia wizi?Nilidhani kuna maboresho
Bi Burhani anasema, watu wanawatumia vishoka waliopo wizarani. Hee, kumbe anajua kuna vishoka! sasa suluhu ni kubadili hati au kutokemeza vishoka anaowajua.

Kwa wenzetu ukiibiwa passport unakuwa under scrutiny. Ikikamatwa mahali na wewe unahusika. Kama imetumika katika uhalifu nawe ni sehemu ya uhalifu. Bi Burhani hajaeleza ngapi zimekamatwa na wahusika wamechukuliwa hatua gani.

Hakuna lolote la maana alilosema bi bURHANI.
 
Hizo sababu hazitoshelezi serikali kutumia kodi tetu kubadili passport.
Kuna mawili Kati ya haya;
Idara ya uhamiaji imejaa mbumbumbu
Au kuna ajenda ya siri ambayo itaishia kwenye ufisadi
Tena zoezi hilo ni la kijuha na ni matumizi mabovu ya kodi zetu.
Anaeleza shida ni MAWAKALA WAO kuwalaghai wananchi, hivyo wanapaswa kuwashughulikia hao na sio kuwasumbua wale ambao wana pass. Hata hivyo hayo matumizi yasiyofaa wanataka kutuambia watadhibiti nia na sababu za watanzania kusafiri?
 
Nakubaliana nawe hoja ya kubadili hati za kusafiria haina uzito. Jambo la msingi linalotakiwa kufanyika ni kuziba na kuwachukulia hatua wale wanaotifua zoezi kwanda kwa utaratibu unaotakiwa. Na wanaofanya hayo wanayolalamikia ni wao wenyewe na ofisi husika.

naona wametoa sababu za kitoto tu

passport ni haki ya raia yeyote wa tanzania na sio favor kwa wale wanaisafiri tu

wanannchi wanatakiwa wapewe elimu jinsi ya kuomba na matumizi ya hati za kusafiria

kutumia agents a.k.a vishoka ni uchaguzi wa mtu hata marekani wanaruhusu mradi mfuate sheria

mtu habanwi jinsi gani atumie passport yake nradi havunji sheria za nchi ... kama kaipoteza si anatakiwa areport police na uhamiaji mara moja ili passport hiyo iwe reported dunia nzima na kuondolewa kwenye system. hizi passports tulizo nazo zinasomwa na mashine dunia nzima kama kuna udanganyifu au wizi umefanyika huwezi itumia

point muhimu kwenye hoja yake ni udanganyifu katika maombi ya passport ... hili si tatizo la waombaji awe mwananchi mwenyewe au kishoka ... tatizo hili ni la kiutendaji ndani ya idara ya uhamiaji yenyewe, wanatakiwa kuchukua hatua kali kwa mfanyakazi yeyote wa uhamiaji atakatoa passport kwa mwombaji bilia kutimiza vigezo. hatua kali isiwe kufukuzwa kazi au faini bali wafungwe jela maana ni kuuza uraia wa tanzania kwa asiye raia wa tanzania

kutokana na uzembe wao inatakiwa watoe hizo passport mpya free of charge (wanaweza fanya hili na kuweka cha juu kwenye gharama ili kupata hela ya uchaguzi). kwa serikali ya sasa ukiona mradi unabuniwa haraka na hela inatoka haraka ujue asilimia kubwa kuna ufisadi maana iko miradi mingi ya muda mrefu ambayo haijapata fedha za kutosha
 
Tume ya uchaguzi nayo imetangaza kufuta vitambulisho vya kula na kutengeneza vipya.haya na hawa uhamiaji nao wameona wanapitwa na ulaji nao wameamua kubadili pasiport kwa sababu za kizembe sana ambazo hata mtoto wa primary anashangaa.bado nida nao hawajamaliza kazi yao!!!jaman ivi hii miradi mbna haieleweki???
 
Back
Top Bottom