Uhalisia wa maisha unazidi kuonekana

Uhalisia wa maisha unazidi kuonekana

Bengal Sanke

Senior Member
Joined
May 16, 2011
Posts
193
Reaction score
78
Mfumuko wa bei unazidi kudhibitiwa, bei za viwanja zimeshuka, mashamba ya kukodi yameshuka bei, kodi za nyumba zimeshuka, vinywaji kwa wanywaji bei zimeshuka (Ingawa inategemeana na wapi unataka kupata kinywaji) Kiukweli taratibu tunarudi kwenye hali halisi ya maisha.
Watu wa kipato cha chini walikuwa wanapelekeshwa sana, kufikiria kuwa na kibanda chako ilikuwa ni ndoto maana viwanja kwa mtu mwaminifu kabisa katika shughuri zake vilikuwa havishikiki

Ni maumivu makali sana kwa wapiga dili, mission town, matapeli, wezi wa maofisini maana walikuwa wanapeta tu. Sijasikia wabunge wanaulizia kuongezewa marupurupu kama ilivyokuwa siku za nyuma.
Tofauti ya asiye nacho na aliye nacho ilikuwa inaongezeka kwa kasi mbaya sana

Hongera sana Mheshimiwa Rais na cabinet yako
 
Watu tunasimamishwa kazi kwenye makampuni we unasema uchumi unakaa sawa kweli? Au unaungana na mchumi mwenzio anayesema bidhaa kupanda bei ndiyo uchumi imara
 
Kodi za nyumba zimeshuka wapi!??

Yani akili yako wewe kama uncle tu...

Kwamba sasahivi mshahara unatoka kila tar 21 hivyo basi hali ya watumishi iko bora kuliko hapo nyuma..!!!??
Sijui ni tusi gani zuri la kuweka hapa.....

Mishahara ni ileile aliyotuacha nayo JK....hivyo basi kama sasahivi haitoshi ..tulikuwa wapiga dili....

MUNGU KIMBIZA SIKU HARAKA.
 
Ndio ile kauli ya JK ....watu wana maisha mazuri hapa bongo kisa foleni za magari ni ndefu saana.

Lakini hawajui kuwa miundo mbinu tunayotumia ni ile ile ya mwaka 1961 wakati tunapata uhuru. .na wakati huo population ya Dar ilikuwa haizidi elfu 50. ..
Lakini leo Dar ina watu almost 5M
 
Wana kazi kweli hawa watu...
 
Back
Top Bottom