Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,926
- 4,110
Ukiangalia mwenendo wa kiuchumi duniani utagundua hali ya maisha kwa sasa ni mbaya. Si Marekani,China,Ujerumani au Uingereza kote kimeumana. Bei kubwa ya mafuta na gesi,chakula,ukame na uhaba wa maji safi, na"Rent" yote haya yamepelekea kupandisha sana gharama za maisha.
Leo Marekani miji kama ya Florida na Califonia kuna idadi kubwa ya Homeless people kutokana na watu kushindwa kumudu kodi ya nyumba(rent). Uingereza kuna mgomo wa wafanyakazi wa reli wakidai nyongeza ya mishahara ili kukabiliana na ukali wa maisha.
Nimekaa na kutafakari nikagundua sababu zinazosababisha dunia kuingia kwenye huu ugumu wa maisha.
1. Nchi kuwekeza pesa nyingi kwenye miundo mbinu ya kisasa. Siku hizi serikali za nchi nyingi duniani zimewekeza mabilioni ya dola kwenye miundombinu mipya ya kisasa km bandari,reli,viwanja vya ndege,barabara n.k na hivyo kuwasababishia wananchi mzigo mkubwa wa kodi.
2. Nchi kubwa kuendekeza vita vya kijinga na kutafta ubabe usio na maana. Kuna muda najiuliza hii vita ya Urusi na Ukraine ilikuwa na sababu gani za msingi km sio ubabe wa Urusi na NATO. Angalia ilivyoharibu hali ya uchumi wa dunia.Mbolea,Chakula,mafuta gesi vyote havishikiki.
3. Nchi kubwa kufanya uwekezaji mkubwa(mega investments) kwenye sayansi na technologia.
Kutokana na ushindani mkubwa uliopo baina ya Urusi,Marekani,China na washirika wao mabilioni ya pesa yamewekezwa kwenye sayansi na technology ili kila upande uwe juu ya mwingine. Kuna ushindani mkubwa wa silaha,anga za juu,mawasiliano n.k.
Marekani kwa mfano wametengeneza Telescope kubwa ya kutazama anga za juu itwayo James Webb Telescope(JWT) ambayo hadi inakamilika imegharimu dola bil.10 zaidi yaTrillion 20 za Kitanzania. Hapo unazungumzia karibu theluthi mbili ya bajeti yetu ya mwaka mzima. Vipi km pesa hii ingepelekwa kwenye kununua chakula na kuboresha huduma za maji ingeokoa watu wangapi duniani?
4.Mabadiliko ya tabia ya nchi. Hapa tunarudi palepale kwenye Ubabe wa kijinga. Nchi zinazoongoza kwa uchafuzi na uharibifu wa mazingira duniani kila mmoja hayuko tayari kupoteza. Ndio maana kila wakikubaliana kutia saini mkataba wa kupunguza gesi chafu kesho unasikia yule kagoma.
Wiki kadhaa zilizopita Ulaya wamekumbwa na joto na ukame mkali la hadi nyuzi joto 40 sababu kuu ni mabadiliko ya tabia ya nchi. Dunia inaangamizwa na maslahi ya wachache.
Kwa kifupi ugumu huu wa maisha kwa kiasi kikubwa umesababishwa na ubabe na ubinafsi wa mataifa makubwa uliopitiliza na ndo chanzo cha maumivu haya yote.
Nawasilisha.