Uhalali wa CCM kumiliki viwanja vya michezo

Uhalali wa CCM kumiliki viwanja vya michezo

Izato

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2019
Posts
5,357
Reaction score
11,504
Muda umewadia sasa kwa chama tawala kuvirudisha viwanja vyote vya michezo ilivyojimilikisha, ili viwe chini ya serikali. Ni ukweli usiopingika ya kwamba utaratibu uliotumika katika kuvimiliki haukuwa mzuri hata kidogo, na unaacha maswali mengi sana juu uhalali wa CCM wa kuvimiliki kama mali binafsi, huku kimsingi ukweli ni kuwa hivi ni mali ya umma.

Viwanja hivi, mathalani Kirumba - Mwanza, Sokoine- Mbeya, Samora - Iringa, Mkwakwani - Tanga, Sheikh Amri Abeid - Arusha, Ali Hassan Mwinyi - Tabora, n.k. vyote vilijengwa kupitia nguvu za wananchi wenyewe, katika maeneo ya serikali yaliyotengwa mahususi kwa ajili hiyo, lakini tu katika kipindi cha utawala wa chama kimoja cha kidola. Kwa hiyo hakuna hoja yoyote ile ya msingi ya CCM ya kuzidi kung'ang'ania kuvimiliki kama mali binafsi katika mazingira ya sasa ya uwepo wa vyama vingi.

Ukiachilia mbali suala la uhalali wa kuvimiliki, lakini jambo lingine ni dhahiri pia kuwa CCM imeshindwa kuviendeleza ili vikidhi mahitaji ya sasa ya maendeleo ya vijana kwa michezo mbalimbali. Viwanja vyote vya kisasa huwa na miundombinu bora ambayo huchochea maendeleo ya michezo yote kwa ujumla, na pia ndiyo kichocheo kingine cha kuzalisha ajira nyingi kwa vijana katika soko la ndani na hata lile la kimataifa.

Kwa sasa hali ya viwanja hivi ni mbaya na hairidhishi hata kidogo kutokana na ufinyu wa bajeti wa kutenga fedha za kuviendeleza, ama pia mapato kiduchu yanayopatikana ili kuweza kuviboresha ili viwe na muonekano wa kisasa sambamba na miundombinu bora na ya kisasa. Jambo ambalo litakuwa ni rahisi kulifanyika endapo vitakuwa chini ya manispaa za miji ama majiji.

Uongozi wa CCM Taifa uwiwe kufanya maamuzi yenye tija kwa Taifa letu, wapate busara ya kuona kuna kila aina ya haja, na pia ni takwa la wakati la kuvirudisha viwanja hivi viwe ni mali ya wananchi wote chini serikalini. Ni vyema njia za kistaarabu zikatumika kwa sasa kuvirudisha kwa hiyari kuliko kusubiri aibu ya kuja kunyang'anywa kwa nguvu siku za mbeleni, ambazo kwa akili ya kawaida kabisa zinaonyesha kuwa wala hazipo mbali kutoka hivi sasa.

Ndiyo! Ajenda ya kuwa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi ni maana sana, lakini vyama vya upinzani pia vinapaswa pia kupaza sauti zao juu ikiwa ajenda nyingine pia inayopaswa kupelekwa kwa wananchi kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi yetu. Na mwisho ni vyema michakato ya kufungua shauri la kisheria ili kupata tafsiri, na hata kuhoji uhalali ma utaratibu uliotumika kwa CCM kujimilikisha baadhi ya mali zake ikiwemo hivi viwanja katika kipindi cha kuanzishwa kwa utawala wa vyama vingi.
 
Muda umewadia sasa kwa chama tawala kuvirudisha viwanja vyote vya michezo ilivyojimilikisha, ili viwe chini ya serikali. Ni ukweli usiopingika ya kwamba utaratibu uliotumika katika kuvimiliki haukuwa mzuri hata kidogo, na unaacha maswali mengi sana juu uhalali wa CCM wa kuvimiliki kama mali binafsi, huku kimsingi ukweli ni kuwa hivi ni mali ya umma.
Naunga mkono hoja, hili JPM alilianza na tukapongeza humu!. Kwa Uamuzi Huu, Pongezi Sana Rais Wetu Magufuli, Utabarikiwa na Mungu, na Taifa Pia Litabarikiwa! pia hili la CCM kutoot mali halali za Watanzania wote kujifanya ni mali zake na kuzitumia kujihalalisha kutawala milele Tanzania, pia niliwahi kulizungumzia! Wenye Matumaini na Upinzani Kushika Dola!, Sahauni! CCM Inajiandaa Kuua Kabisa na Kuuzika Jumla !.

P
 
Tuliochangia ni sisi ambao bado tuko CCM
Bwashee unajua jambo la umiliki wa mali huleta taharuki kubwa hata katika ngazi za familia. Pale inapotokea kaka mkubwa anapindisha sheria na kujitwaalia malii za familia kama zake binafsi na kujinufaisha yeye mwenyewe.

Madogo hujisikia vibaya sana huku wakiwa hawana kitu chochote, kaka mkubwa anaendelea kula anasa, kuwasimanga na kuwalaumu kuwa ni wavivu wa kufiri na kufanya kazi, wamekosa weledi na maarifa, umaskni waliokuwa nao ni wakujitakia wenyewe. Anawapa ushauri kuwa mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe
 
Viwanja vyote vyenyewe wamewapangisha watu wa gereji,maduka nk
Watoto sahv hawana sehemu za kwenda kucheza,ndomana wanaishia kucheza vichochoroni mwishowe kubakana na kulawatiana tu huko

Ova
 
Muda umewadia sasa kwa chama tawala kuvirudisha viwanja vyote vya michezo ilivyojimilikisha, ili viwe chini ya serikali. Ni ukweli usiopingika ya kwamba utaratibu uliotumika katika kuvimiliki haukuwa mzuri hata kidogo, na unaacha maswali mengi sana juu uhalali wa CCM wa kuvimiliki kama mali binafsi, huku kimsingi ukweli ni kuwa hivi ni mali ya umma.
Yaani hakuna akili ya kipumbavu kubwa kama kujimilikisha mali halali za Umma, haiji akili aina hio ya upumbavu, hata makaburu yalifanya hivyo kwenye ardhi kule South Africa
 
Nimesikia hotuba ya waziri wa michezo kuwa watakarabati viwanja vvote vya ligi kuu ili kufikia viwango vya kimataifa ili kutumika kwenye AFCON je ikifanyika hivyo kwa bajeti ya Serikali itakuwaje ngoja tuone reaction ya Bunge. Au utakuwa mwanzo wa kuikabidhi serikali viwanja hivyo vya mpira. Tuvumilie tuone mwelekeo wa serikali.
 
Walishatenga fedha za serikali kukarabati hivyo viwanja vya CCM. Bunge haliwezi kuhoji uhalali wa jambo hilo maana ni CCM wote. Lakini tumehoji sana uhalali wa jambo hilo. CCM haiwezi kuachia hivyo viwanja ikiwa madarakani maana inaona aibu kuporwa mali za urithi wanazotambia.
 
Muda umewadia sasa kwa chama tawala kuvirudisha viwanja vyote vya michezo ilivyojimilikisha, ili viwe chini ya serikali. Ni ukweli usiopingika ya kwamba utaratibu uliotumika katika kuvimiliki haukuwa mzuri hata kidogo, na unaacha maswali mengi sana juu uhalali wa CCM wa kuvimiliki kama mali binafsi, huku kimsingi ukweli ni kuwa hivi ni mali ya umma.
Ni wizi mtupu! Ni wakati sasa wa kurudisha kila kitu CCM walichojimiliikisha kinyemela, kuanzia majengo, taasisi za elimu hadi jeshi na mahakama.
 
Biafra pale enzi zetu tumecheza sana mpira lakini sahv uwanja umejaa watu wa garage na wafanyabiashara wengine
Kizaz cha sasa watoto hawana pakwenda kucheza au kupumzika
Watoto wanaishia uchororoni na huko
Wanajiingiza kwenye mambo siyo

Ova
 
ccm turudishieni viwanja vyetu. Too much is harmful. Kila kitu mnajimilikisha! Kwani hii nchi ni ya baba yenu, au ni ya Watanzania?
 
Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta uliopo Arusha haukujengwa na CCM wala nguvu za umma.

Uwanja huu ulijengwa na Mkoloni mwingereza anayeitwa Middleton.Uwanja huu ulikuwa mpaka na taa na mechi za usiku zilichezwa bila matatizo.

Middleton alipoondoka aliukabidhi kwa Town Council ya Arusha wakati huo.Waliuendesha mpaka mwaka 1977 ulipochukuliwa na CCM na wakaufanyia ukarabati kwa kuongeza majukwaa.
 
Mkuu nakushukuru mno kwa hii elimu kwangu kuhusiana na historia ya uwanja huu. Lakini ukweli bado unabakia kuwa bado kuna utata kuhusu umiliki wake na CCM. Ilikuwa ni mithili ya kufanya "looting" kwa wananchi wasiokuwa na uwezo wa kujitetea.
 
Back
Top Bottom