Hii nchi kuna mambo mengi hufanyika bila kufikiria mbele. Leo tunakimbizwakimbizwa kwa ajili ya kitambulisho cha NIDA. Lakini kwa mujibu wa sheria ya utambulisho wa uraia, kadi/namba ya NIDA ndio kithibitisho pekee halali cha uraia wa mtanzania; yaani aliyesajiliwa NIDA ndo anatambulika kisheria kuwa ni raia wa Tanzania.
Wakati NIDA hutumia alama za vidole (fingerprint) katika kusajili raia, juzi tu hapa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) imetanganza kufanya maandalizi ya kuanzisha kanzidata ya taifa ya vinasaba (National Centre for Human DNA).
Kanzidata hii itatumika katika utambuzi wa watu/raia na kwamaana hiyo kanzidata hii itaunganishwa na za mamlaka zingine hasa zile za NIDA kuboresha utambuzi wa raia.
Biometria ya alama za vidole (fingerprint) inayotumiwa na NIDA ina mapungufu ukilinganisha na ile ya vinasaba (DNA profile) Mathalani, tofauti na DNA profile, fingerprint haiwezi kuonesha uhusiano (unasaba) wa ndugu wa karibu (closely related individuals).
Zaidi, fingerprint haiwezi kutumia sampuli ya mwili ulioharibika kubaini utambulisho wa mwenye huo mwili au ndugu yake wa karibu.
Ingawa fingerprint ni biometria ya haraka, isiyo na gharama kubwa na haihitaji mtaalamu katika ukusanyaji wake, haikupaswa kutumiwa na NIDA kutokana na udhaifu wake kama ulivyooneshwa hapo juu na badala yake mamalaka hiyo ingetumia DNA profiles za watu zitazoandaliwa na GCLA.
Hii ni kwasababu moja ya masharti ya NIDA ni muombaji wa usajili kutoa uthibitisho wa "makaratasi" kuonesha uraia au asil ya wazazi wake. Ifahamike kuwa "makaratasi" yanaweza kuwa na taarifa za uongo hata kama zinatolewa na mamlaka halali kama vile RITA au Mahakama/Wakili.
Wasiwasi uliopo ni kwamba hapo baadae kutakuwa na usumbufu kwa raia kwasababu kanzidata ya DNA profiles zitakazozoandaliwa na GCLA zinaweza kukinzana na taarifa za uhusiano (nasaba) za mzazi na mwanawe zinazokusanywa leo na NIDA kwa kutumia ushahidi wa "makaratasi".
Je, ikitokea DNA profile ya raia X hairandani na ya mzazi wake (raia Y) aliyemtaja kwenye taarifa zake zilizowasilishwa NIDA itakuwaje?
Zoezi la uhakiki wa uraia litatuhusu hapo baadae na huu ni usumbufu.