Uhakiki wa uraia haukwepeki hapo baadae kwa wale wanaosajiliwa sasa na NIDA

X-bar

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
1,002
1,146
Hii nchi kuna mambo mengi hufanyika bila kufikiria mbele. Leo tunakimbizwakimbizwa kwa ajili ya kitambulisho cha NIDA. Lakini kwa mujibu wa sheria ya utambulisho wa uraia, kadi/namba ya NIDA ndio kithibitisho pekee halali cha uraia wa mtanzania; yaani aliyesajiliwa NIDA ndo anatambulika kisheria kuwa ni raia wa Tanzania.

Wakati NIDA hutumia alama za vidole (fingerprint) katika kusajili raia, juzi tu hapa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) imetanganza kufanya maandalizi ya kuanzisha kanzidata ya taifa ya vinasaba (National Centre for Human DNA).

Kanzidata hii itatumika katika utambuzi wa watu/raia na kwamaana hiyo kanzidata hii itaunganishwa na za mamlaka zingine hasa zile za NIDA kuboresha utambuzi wa raia.

Biometria ya alama za vidole (fingerprint) inayotumiwa na NIDA ina mapungufu ukilinganisha na ile ya vinasaba (DNA profile) Mathalani, tofauti na DNA profile, fingerprint haiwezi kuonesha uhusiano (unasaba) wa ndugu wa karibu (closely related individuals).

Zaidi, fingerprint haiwezi kutumia sampuli ya mwili ulioharibika kubaini utambulisho wa mwenye huo mwili au ndugu yake wa karibu.

Ingawa fingerprint ni biometria ya haraka, isiyo na gharama kubwa na haihitaji mtaalamu katika ukusanyaji wake, haikupaswa kutumiwa na NIDA kutokana na udhaifu wake kama ulivyooneshwa hapo juu na badala yake mamalaka hiyo ingetumia DNA profiles za watu zitazoandaliwa na GCLA.

Hii ni kwasababu moja ya masharti ya NIDA ni muombaji wa usajili kutoa uthibitisho wa "makaratasi" kuonesha uraia au asil ya wazazi wake. Ifahamike kuwa "makaratasi" yanaweza kuwa na taarifa za uongo hata kama zinatolewa na mamlaka halali kama vile RITA au Mahakama/Wakili.

Wasiwasi uliopo ni kwamba hapo baadae kutakuwa na usumbufu kwa raia kwasababu kanzidata ya DNA profiles zitakazozoandaliwa na GCLA zinaweza kukinzana na taarifa za uhusiano (nasaba) za mzazi na mwanawe zinazokusanywa leo na NIDA kwa kutumia ushahidi wa "makaratasi".

Je, ikitokea DNA profile ya raia X hairandani na ya mzazi wake (raia Y) aliyemtaja kwenye taarifa zake zilizowasilishwa NIDA itakuwaje?

Zoezi la uhakiki wa uraia litatuhusu hapo baadae na huu ni usumbufu.
 
Point yako haina mashiko na sidhani kama dna inaweza kutumika katika kumtambua raia wa tanzania ila inaweza kutumika kiwatambua ndugu

Labda hapo baadae details za dna zitiwe ktk micro chip ya kitambulisho ili itumike kwa mambo ya kusolve uhalifu

Sidhani kama kuna nchi duniani inayotumia dna ili kuwatambua raia wake
 
wakijichanganya wakaanza kusajili watu kwa DNA tutarajie ndoa nyingi kuvunjika na vitendo vya kujiua na kuuana kuongezeka kwa kasi sana maana kuna mtu amesomesha watoto zaidi ya 3 shule za gharama kwelikweli halafu eti umwambie hao watoto sio wa kwake lazima tu afanye kitu na hicho kitu ni kati ya kuua au kujiua au vyote kwa pamoja yaani kuua na kisha kujiua
 
Wenzetu wana creat ajira kwa raia wake sisi tupo busy kufunga laini za simu, kazi kwelikweli
 
Hii nchi kuna mambo mengi hufanyika bila kufikiria mbele. Leo tunakimbizwakimbizwa kwa ajili ya kitambulisho cha NIDA. Lakini kwa mujibu wa sheria ya utambulisho wa uraia, kadi/namba ya NIDA ndio kithibitisho pekee halali cha uraia wa mtanzania; yaani aliyesajiliwa NIDA ndo anatambulika kisheria kuwa ni raia wa Tanzania.

Wakati NIDA hutumia alama za vidole (fingerprint) katika kusajili raia, juzi tu hapa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) imetanganza kufanya maandalizi ya kuanzisha kanzidata ya taifa ya vinasaba (National Centre for Human DNA).

Kanzidata hii itatumika katika utambuzi wa watu/raia na kwamaana hiyo kanzidata hii itaunganishwa na za mamlaka zingine hasa zile za NIDA kuboresha utambuzi wa raia.

Biometria ya alama za vidole (fingerprint) inayotumiwa na NIDA ina mapungufu ukilinganisha na ile ya vinasaba (DNA profile) Mathalani, tofauti na DNA profile, fingerprint haiwezi kuonesha uhusiano (unasaba) wa ndugu wa karibu (closely related individuals).

Zaidi, fingerprint haiwezi kutumia sampuli ya mwili ulioharibika kubaini utambulisho wa mwenye huo mwili au ndugu yake wa karibu.

Ingawa fingerprint ni biometria ya haraka, isiyo na gharama kubwa na haihitaji mtaalamu katika ukusanyaji wake, haikupaswa kutumiwa na NIDA kutokana na udhaifu wake kama ulivyooneshwa hapo juu na badala yake mamalaka hiyo ingetumia DNA profiles za watu zitazoandaliwa na GCLA.

Hii ni kwasababu moja ya masharti ya NIDA ni muombaji wa usajili kutoa uthibitisho wa "makaratasi" kuonesha uraia au asil ya wazazi wake. Ifahamike kuwa "makaratasi" yanaweza kuwa na taarifa za uongo hata kama zinatolewa na mamlaka halali kama vile RITA au Mahakama/Wakili.

Wasiwasi uliopo ni kwamba hapo baadae kutakuwa na usumbufu kwa raia kwasababu kanzidata ya DNA profiles zitakazozoandaliwa na GCLA zinaweza kukinzana na taarifa za uhusiano (nasaba) za mzazi na mwanawe zinazokusanywa leo na NIDA kwa kutumia ushahidi wa "makaratasi".

Je, ikitokea DNA profile ya raia X hairandani na ya mzazi wake (raia Y) aliyemtaja kwenye taarifa zake zilizowasilishwa NIDA itakuwaje?

Zoezi la uhakiki wa uraia litatuhusu hapo baadae na huu ni usumbufu.
Kwahiyo hii inji watu wataishi kwa kula hizo kanzudata!
Tushakuwa kama mifugo ya kuhesabiwa kila siku!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii mambo ya usaijli wa simu, moja ya hasara zake ndio hizo kujipenyeza kwa mamluki.

Ule uharaka unaweza waingiza baadhi ya wasio kuwa na sifa.

Naamini Taasisi husika ilizingatia vigezo wakati pia ikilinda umuhimu wa mawasiliano.
 
Point yako haina mashiko na sidhani kama dna inaweza kutumika katika kumtambua raia wa tanzania ila inaweza kutumika kiwatambua ndugu

Labda hapo baadae details za dna zitiwe ktk micro chip ya kitambulisho ili itumike kwa mambo ya kusolve uhalifu

Sidhani kama kuna nchi duniani inayotumia dna ili kuwatambua raia wake
Unapokosoa wazo basi jaribu kuwa na hoja inayoeleweka. Yaani unatambua na kukili kuwa DNA inatumika katika kumtambua mtu na vizazi vyake lakini bado unabisha kutumika katika utambuzi wa uraia wake. Cha ajabu unabisha bila kufafanua ni kwanini haiwezekani.

Lakini kusema tu kwamba Tanzania haiwezi kutumia teknolojia ya vinasaba eti kwa vile tu hakuna nchi yoyote dunuiani inayotumia teknolojia hiyo si hoja kwa vile kila nchi ina utaratibu wake.

Hivi unaweza kufafanua ubaya/udhaifu wa matumizi ya DNA katika mambo ya uraia ili tujifunze ni kwanini haitumiki hivyo? Au unataka kutuambia Tanzania haiwezi kuanzisha utaratibu au matumizi ya kitu fulani hadi itokee kuwa kuna nchi nyingine duniani inafanya hivyo?

Unakosoa wazo langu na wakati huohuo unataja wazo la "microchip". Hivi unaweza kueleza ni nini hiyo microchip, inatumikaje na katika nchi gani? Je, unatofautishaje matumizi ya microchip na kitambulisho cha uraia? Au unataka kusema microchip ni "idea" yako tu?
 
Tanzania mtu yeyote wakati wowote isipokuwa waimba pambio kwa wenye mamlaka, unaweza kuambiwa siyo raia hata kama una lundo la makaratasi na vitambulisho.

Lwajabe, Kakobe, Jenerali Ulimwengu, Kabendera wote waliambiwa siyo watanzania.

Tena hadi JIWE ambaye chimbuko lake lina UTATA na yeye anahoji watu URAIA ???!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom