Wakazi wa Dar na Mbeya waliopewa Namba za NIDA kuanza kupewa Vitambulisho (Kadi) Desemba 12, 2203

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
20231211_201326.jpg
20231211_201320.jpg

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inatarajia kuanza ugawaji wa Vitambulisho (Kadi) kwa Wananchi waliojisajili na kupewa Namba za Utambulisho (NIN) katika Mikoa ya Dar na Mbeya hapo Desemba 12, 2023.

Taarifa iliyotolewa na NIDA imeeleza kuwa zoezi hilo litafanyika katika Ofisi za Serikali za Mitaa za Wilaya zote za Mikoa hiyo kwa kipindi cha siku 14 kuanzia tarehe tajwa.

Hatua ya NIDA inafuatia Mjadala uliofanywa na JamiiForums Septemba 7, 2023 ambapo Wananchi walihoji juu ya kusuasua kwa Utoaji Vitambulisho licha ya wengine kujiandikisha kwa zaidi ya miaka 5.
 
Wa kwanza kucomment. Huo mwaka 22023 ndio mwaka gani? Hawa ndio wasomi wetu na UVCCM.
 
Hatua ya NIDA inafuatia Mjadala uliofanywa na JamiiForums Septemba 7, 2023 ambapo Wananchi walihoji juu ya kusuasua kwa Utoaji Vitambulisho licha ya wengine kujiandikisha kwa zaidi ya miaka 5.
Utendaji kazi wa aina hii hauwezi kamwe kutufikisha popote kama taifa.

Huu ni mfano mbovu kabisa wa jinsi serikali inavyofanya kazi zake.
Hata kama kulikuwepo na sababu maalum zilizo sababisha ucheleweshaji wa namna hi, hizo sababu zingetolewa mara tu zilipojitokeza, ili watu wajue.
Serikali itapanga vipi kufanya jambo, halafu katikati ya utekelezaji kutelekeza kazi bila ya maelezo yoyote?
 
Back
Top Bottom