Uhai wa binadamu unaanza wakati gani?

Uhai wa binadamu unaanza wakati gani?

na ndio mana ukitumia baadhi ya njia za uzazi wa mpango kama madawa,vipandikizi unakua UMEUA kwa sababu njia hizo hazizuii mbegu na yai kukutana ila zinazuia yai lililorutibishwa kuendelea kukua,mana yake ni kuharibu mimba iloyotungwa au kuzuia already FERTILIZED EGG(EMBRYO) isijipandikize IMPLANTATION. amabyo ni sawa na kuua tu.

2.ABORTION kutoa mimba iliyokwisha kutungwa nayo ni sawa na KUUA PIA.

TUTADAIWA HIZI ROHO ZA MIMBA TUNAZOZIHARIBU NI DHAMBI ZA KU UWA...wengi wetu huku WALISHAUA.
Ujauzito ukiwa tumboni hauhesabiki ni mtu, ndio maana mimba au ujauzito ukiharibika huwezi sema umefiwa na mtu ukaweka msiba na matanga.

Hata ajali ikitokea mama mjamzito akafariki na ujauzito wake haiwezi kutangazwa wamefariki watu wawili.
 
01. SWALI Ujauzito ukiwa tumboni hauhesabiki ni mtu?,

02. **SWALI**ndio maana mimba au ujauzito ukiharibika huwezi sema umefiwa na mtu ?

3.SWali la 3 ukaweka msiba na matanga kwa mimba iliyoharibika.??
 
01. SWALI Ujauzito ukiwa tumboni hauhesabiki ni mtu?,

02. SWALI ndio maana mimba au ujauzito ukiharibika huwezi sema umefiwa na mtu ?

03. SWALI ukaweka msiba na matanga kwa mimba iliyoharibika.??
 
Kisayansi na kimatibabu

jibu la swali kuhusu lini maisha yanaanza ??

linategemea kama unaangalia mwanzo wa kiumbe cha kipekee kibiolojia au ufafanuzi wa kitabibu wa mwanzo wa ujauzito.Hakuna makubaliano ya pamoja katika nyanja zote, kwani mifumo ya kibiolojia, kitabibu, na kisheria inaangalia hatua hizi tofauti.1. Fertilization (Urutubishaji) —

Mtazamo wa Kibiolojia

kiumbe kipya na cha kipekee cha mwanadamu kinaanza kuwepo wakati wa fertilization.Mchakato: Mbegu ya kiume inapoungana na yai la kike, vinatengeneza seli moja inayoitwa zygote.
Vinasaba (DNA): Zygote inakuwa na seti kamili na ya kipekee ya DNA ya mwanadamu ambayo haijawahi kuwepo hapo kabla, na ndiyo inayoongoza ukuaji wake wote
.
Hoja:
Kwa sababu seli hii iko hai, ni ya mwanadamu, na inajiongoza yenyewe kukua kuwa binadamu kamili, wanabiolojia wengi wanahesabu hatua hii kama mwanzo wa maisha ya kiumbe binafsi

.2. Implantation (Kupandikizwa) — Mtazamo wa Kitatibu na UjauzitoMashirika makubwa ya matibabu duniani yanafasiri kuwa mwanzo rasmi wa ujauzito (pregnancy) unaanza wakati wa implantation, na si wakati wa urutubishaji.Mchakato: Baada ya fertilization, seli zinazoendelea kujigawa (blastocyst) husafiri kwenye mirija ya uzazi na kujishikiza kwenye ukuta wa mji wa mimba, hatua inayotokea siku 6 hadi 9 baadaye.

Hoja:
Karibu asilimia 50 ya mayai yaliyolutubishwa hushindwa kujishikiza na hutoka yenyewe mwilini bila mwanamke kujua. Sayansi ya tiba inapima ujauzito kuanzia implantation kwa sababu ndio wakati kiinitete (embryo) kinapoungana na mwili wa mama ili kupata virutubisho vya kuishi.3. Mawimbi ya Ubongo na Uwezo wa Kuishi

(Mtazamo wa Kinyurolojia)Baadhi ya wanasayansi na wataalamu wa maadili ya viumbe (bioethicists) huangalia hatua maalum za ukuaji wakati wa ujauzito:Gastrulation (Siku ya 14): Hii ni hatua ambayo kiinitete hakiwezi tena kujigawa kutengeneza mapacha wanaofanana. Wataalamu wengine wanadai utambulisho wa mtu mmoja mmoja unakamilika hapa.Mawimbi ya Ubongo (Wiki ya 24-28):

Mitazamo mingine inasema maisha huanza pale ubongo unapokuwa na mtandao wa neva unaowezesha utambuzi (consciousness) na uwezo wa kuhisi, hatua inayoendana na uwezo wa mtoto kuishi nje ya mfuko wa uzazi (viability).
 
Nchini Tanzania, kutoa mimba ni kosa la jinai chini ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code, Cap. 16).Mwanamke anayetoa mimba mwenyewe au mtu anayemsaidia anaweza kuhukumiwa kifungo cha miaka saba jela, wakati daktari au mtu anayefanya kitendo hicho anaweza kufungwa hadi miaka 14 jela, isipokuwa tu kama kimefanyika kuokoa maisha ya mama.Sheria na Adhabb KuuSheria Kuu: Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 (Kifungu cha 150 hadi 152).Adhabu kwa Mwanamke: Kifungo cha hadi miaka 7 jela kwa kujaribu au kutoa mimba mwenyewe.Adhabu kwa Mtoa Huduma: Kifungo cha hadi miaka 14 jela kwa mtu anayetoa au kusababisha mimba itoke kinyume cha sheria.Upekee na VighairiSheria inaruhusu utoaji wa mimba chini ya masharti maalum (Kifungu cha 230-234) pale tu ambapo daktari bingwa anathibitisha kuwa kuendelea na ujauzito kunahatarisha maisha au afya ya mama
 
Eeh mkuu hii ni ngoma kweli! Hata mimi nimesikia hivyo, lakini hiyo ya kumwaga nje umeua ni kali bana. Hivi sasa hata madaktari wanasema kuna njia nyingi za kupanga uzazi, si lazima uwe mkorofi hivyo. Lakini kwa ufupi, uhai unaanza kwenye yai na mbegu, ndio maana watu wanasema mimba ni zawadi. safi sana
 
Halafu unakaa wapi baada ya kuungana !
Unakaa tumboni miezi 9 (ni kama mbinguni waliyosema wamisionari) kila kitu unahudumiwa. Ukizaliwa ni kama unaingia motoni, taabu zinaanza, kula mwenyewe, kujisaidia, kupumua na mgonjwa. Mwisho ni kifo.
 
Baadhi ya sifa za kiumbe hai ni zifuatazo
1. Kinaweza kukua
2. Kinaweza kula
3. Kinaweza kujongea
4. Kinaweza kutoa taka mwili
Uhai wa binadamu unaanza pale anapokuwa na sifa hizo,so mimba ikitungwa tu tayari binadamu kawa hai maana ana uwezo wa kufanya yote hayo akiwa huko huko tumboni.
 
Inategemeana na familia utakayoibukia..
 
Uhai unaanzia kwenye yai na mbegu za kiume.

Ni kinyume na sheria kumwaga nje ya uke wakati wa kujamiiana. Mbegu zinatakiwa zimwagiwe ndani ya uke.

Ukimwaga nje umeua. 🙂

Usiniulize chochote kuhusu hilo..Narudia sheria ya Bwana kwa wayahudi
Kama ni hivo mkuu I'm MASSIVE MENACE 😅
 
Uhai unaanzia kwenye yai na mbegu za kiume.

Ni kinyume na sheria kumwaga nje ya uke wakati wa kujamiiana. Mbegu zinatakiwa zimwagiwe ndani ya uke.

Ukimwaga nje umeua. 🙂

Usiniulize chochote kuhusu hilo..Narudia sheria ya Bwana kwa wayahudi
Ukimwaga nje haujaua kwa sababu nje unamwaga sperms
Sperms pekee bila kukutana na mbegu za kike sio mtoto.
 
Ukimwaga nje haujaua kwa sababu nje unamwaga sperms
Sperms pekee bila kukutana na mbegu za kike sio mtoto.
Mwanzo 38 : 8 - 10

Ila mimi nasoma sana sheria za Wayahidi kutoka kwa Bwana. Ingawa kanisa limezibadilish kufanya sheria za kanisa na kuzipunguza

Ukiacha onani aligoma kumpatia ndugu yake uzao, ilikuwa ni koda kubwa sana kumwaga nje

Ndio maana nikasema hapo juu nisiulizwe, hiyp ilikuws Amri za Mungu ambazo Mussa alizipokea mlima sinai

Hizi amri alizovunja Musa zilikuw mia sita kumi na tatu. Moja wapo usikojoe nje🙂

Ubishani wa Yai na kuku nani limeanza, msingi wake ni Mungu kaanza. Ndio shetani anadhani kaanza yeye
Hivyo Mungu emeweka uhai kwenye mbegu na mayai, ni jambo kubwa zaidi navoweza kuliwakilisha kwako.

Nachojua ni amri mengine najuaje ndugu yangu msingi wqke ni nini?
 
Baadhi ya sifa za kiumbe hai ni zifuatazo
1. Kinaweza kukua
2. Kinaweza kula
3. Kinaweza kujongea
4. Kinaweza kutoa taka mwili
Uhai wa binadamu unaanza pale anapokuwa na sifa hizo,so mimba ikitungwa tu tayari binadamu kawa hai maana ana uwezo wa kufanya yote hayo akiwa huko huko tumboni.
Asante mkuu!
 
SIfa
1. Anaweza kukua. Fetus grows in the womb
2. Fetus eat off her mothers
3. Mtoto tumboni anacheza
4. Mtoto tumboni anakunya. Akizaliwa anatoka na mavi yake

Labda utoe mfano mwingine ila hivi vyote mtoto anaanza kuvifanya tumboni
 
Back
Top Bottom