Uhai wa binadamu unaanza wakati gani?

Uhai wa binadamu unaanza wakati gani?

Unataka kusemaje? Kuwa akibakwa sio kiumbe cha Mungu?

Ni jambo la kusikitisha
Kwanza una uthibitisho mungu yupo?
Halafu kama kubaka ni kitendo kiovu kwa nini anaruhusu ubakaji na mimba zinazotokana na ubakaji kutungwa??
 
Hata atom zenye energy zina uhai..

Tatizo binadamu anahisi consciousness iko kwenye ubongo
 
Uhai ni illusion...

When you die unarudi kwenye source..

Unarudi kwenye sehemu uliyo tokea..

Energy only changes form
 
Wakuu....

Uhai wa binadamu unaanza wakati gani, akiwa tumboni. Na unakaa sehemu gani ya mwili baada ya kuanza!

Cc. Mshana Jr
Jagina and others
Kutoka kwa Abu 'Abdir-Rahman Abdullah ibn Mas'ud (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema: "Alituhadithia Mtume wa Mwenyezi Mungu,Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), naye ni mkweli mwenye kusadikiwa:"

"Hakika mmoja wenu hukusanywa umbo lake katika tumbo la mama yake kwa siku arobaini akiwa ni tone la manii (Nutfah), kisha huwa pande la damu (´Alaqah) kwa mfano wa siku hizo (40), kisha huwa bonge la nyama (Mudghah) kwa mfano wa siku hizo (40). Kisha Mwenyezi Mungu humtuma Malaika kwake, naye humpulizia roho ndani yake, na anaamrishwa kuandika mambo manne: Riziki yake, ajali yake (muda wa kufa), vitendo vyake, na kama atakuwa mtu wa mashaka (motoni) au wa furaha (peponi)..." [Bukhar na Muslim]

Hadithi hii inabainisha safari ya ukuaji wa mtoto tumboni katika vipindi vitatu vikuu vya siku 40 kila kimoja kabla ya kupewa roho:
    • Siku 1 hadi 40:
    • Mtoto anakuwa katika hali ya tone la manii lililorutubishwa (Nutfah).
    • Siku 41 hadi 80: Anabadilika na kuwa pande la damu linaloning'inia (´Alaqah).
    • Siku 81 hadi 120: Anakuwa bonge la nyama lililoanza kushonwa umbo (Mudghah).
    • Siku ya 120 (Mwezi wa 4): Malaika anakuja kumpulizia roho na kuandika majaaliwa yake yote.
    • Mambo Manne Yanayoandikwa Wakati wa Kupewa Roho
    Malaika anapofika kuweka roho, anaandika mambo yafuatayo ambayo yatatawala maisha yote ya kiumbe hicho:
      • Riziki: Kiasi cha mali, chakula, na neema atakazopata duniani.
      • Umri (Ajali): Siku na sekunde kamili atakayokufa.
      • Amali: Matendo yote atakayoyafanya (mema na mabaya).
      • Mwisho Wake: Hatima yake kama atafuzu kuingia Peponi au atakuwa wa Motoni.
 
Kutoka kwa Abu 'Abdir-Rahman Abdullah ibn Mas'ud (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema: "Alituhadithia Mtume wa Mwenyezi Mungu,Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), naye ni mkweli mwenye kusadikiwa:"

Hadithi hii inabainisha safari ya ukuaji wa mtoto tumboni katika vipindi vitatu vikuu vya siku 40 kila kimoja kabla ya kupewa roho:
    • Siku 1 hadi 40:
    • Mtoto anakuwa katika hali ya tone la manii lililorutubishwa (Nutfah).
    • Siku 41 hadi 80: Anabadilika na kuwa pande la damu linaloning'inia (´Alaqah).
    • Siku 81 hadi 120: Anakuwa bonge la nyama lililoanza kushonwa umbo (Mudghah).
    • Siku ya 120 (Mwezi wa 4): Malaika anakuja kumpulizia roho na kuandika majaaliwa yake yote.
    • Mambo Manne Yanayoandikwa Wakati wa Kupewa Roho
    Malaika anapofika kuweka roho, anaandika mambo yafuatayo ambayo yatatawala maisha yote ya kiumbe hicho:
      • Riziki: Kiasi cha mali, chakula, na neema atakazopata duniani.
      • Umri (Ajali): Siku na sekunde kamili atakayokufa.
      • Amali: Matendo yote atakayoyafanya (mema na mabaya).
      • Mwisho Wake: Hatima yake kama atafuzu kuingia Peponi au atakuwa wa Motoni.
Achana na hadithi, jikite kwenye Sayansi.
 
Achana na hadithi, jikite kwenye Sayansi.
kaulize Wanasayansi kuhusu elimu ya Embriyology halafu rudi kuyasoma hayo maneno ya Mtume Muhammad (pbuh) halafu jiulize alijuaje hizo details katika karne ya 7 wakati hakukuwa na vipimo vyovyote vya kisayansi kuhusiana na hizo details.
 
Mara tu utungisho unapofanyika tayari mtu huwa nafsi hai. Ndiyo maana huruhusiwi kutoka mimba hata kama ni ya wiki 1
 
Asante... mkuu Mkono Mmoja
swali... huyo mtoto akitolewa kama kiumbe ambacho may be kina siku 80 hatima yake inakuaje?
 
Mara tu utungisho unapofanyika tayari mtu huwa nafsi hai. Ndiyo maana huruhusiwi kutoka mimba hata kama ni ya wiki 1
Safi, mkuu umefika! hichi kiumbe kikitolewa tumboni bado niki zygote hatima yake ni nini kwa MUNGU.
 
MUNGU MUUMBAJI ANASEMA HIVI

Quran 22:5-10

"Enyi watu! Ikiwa nyinyi mna shaka ya kufufuliwa basi kwa hakika Sisi tulikuumbeni kutokana na udongo, kisha kutokana na manii, kisha kutokana na kipande cha damu ilio gandana, kisha kutokana na kipande cha nyama chenye umbo na kisicho kuwa na umbo, ili tukubainishieni. Nasi tunakiweka katika matumbo ya uzazi tunacho kitaka mpaka muda ulio wekwa. Kisha tunakutoeni kwa hali ya mtoto mchanga, kisha mfikie kutimia akili. Na wapo katika nyinyi wanao kufa, na wapo katika nyinyi wanao rudishwa kwenye umri wa unyonge kabisa, hata mtu awe hajui kitu baada ya kuwa anakijua. Na unaiona ardhi imetulia kimya, lakini tunapo yateremsha maji juu yake husisimka na kututumka, na kumea kila namna ya mimea mizuri.

Hayo ni kwa sababu hakika Mwenyezi Mungu ndiye Haki, na kwamba hakika Yeye ndiye mwenye kuhuisha wafu, na kwamba hakika Yeye ni Muweza wa kila kitu.

Na kwamba hakika Saa itakuja hapana shaka kwa hilo, na kwamba hakika Mwenyezi Mungu atawafufua walio makaburini.

Na katika watu wapo wanao bishana juu ya Mwenyezi Mungu bila ya ilimu, wala uwongofu, wala Kitabu chenye nuru.

Anaye geuza shingo yake ili kupoteza watu waache Njia ya Mwenyezi Mungu. Duniani atapata hizaya, na Siku ya Kiyama tutamwonjesha adhabu ya kuungua

(Ataambiwa): Hayo ni kwa sababu ya iliyo tanguliza mikono yako. Na hakika Mwenyezi Mungu si dhaalimu kwa waja."
 
Kwanza una uthibitisho mungu yupo?
Halafu kama kubaka ni kitendo kiovu kwa nini anaruhusu ubakaji na mimba zinazotokana na ubakaji kutungwa??
Ndio Mungu yupo
kubaka ni kitendo kiovu sana

Mwili wako, akili yako, utashi wako unamilikiwa na nani? Ndio cha haya mambo yote unayaona yanaendelea duniani

Ni rahisi sana kupeleka machukizo yetu kwa Mungu. Hata mimi nishafanya hivyo mara kibao tu

Ukweli hautabadilika. You belong to him una haki ya kulalamika but uhalisia wetu dunia hii unamilikiwa na mwovu
Ndio maana kila tunayoyawaza yana ubaya

Kisha tukichuma yanayopandwa na ubaya tunaenda kumlaumu Yeye

We are not worthy to question.
 
Back
Top Bottom