Uhaba wa DOLA (U.S.D) Tanzania na ukimya wa Serikali

Zillion

JF-Expert Member
May 15, 2017
1,358
1,807
Kumekuwa na uhaba mkubwa wa fedha za kigeni hapa Tanzania hasa USD ambayo ndio hutumika sana kwa malipo kwa biashara za kimataifa.

Pamoja na kupanda kwa dola na kushuka kwa shilingi kutoka 2375 mpaka 2405 bado imekuwa shida sana kupatikana.

Kwanza ilianza mabenki kuweka ukomo wa kununua dola mpaka 5000 USD pekee. Na sasa wameweka ukomo wa 1000 USD pekee.

Maduka ya kubadilisha fedha za kigeni hakuna dola, Benki hazina dola, wafanyabiashara hawana dola Serikali iko kimya na hakuna hatua za dharura zinazochukulia kunusuru hali hii mbaya kiuchumi.

Sasahivi ukihitaji dola 30,000 inabidi uzunguke kwenye mabenki karibu mwezi mzima ili kuzipata
Hali hii imekuwa changamoto sana kwa wafanyabiashara (Waagizaji)

Nauliza hii nchi tuna Serikali?!

==
Pia soma, Kufuatia upungufu wa dola, BoT yatoa maelekezo ya kudhibiti Viwango Vya Miamala
 
Tanzania ina-import mpaka mpaka Kelo kuliko ku-export na Forex reserve ya hii nchi ni ndogo Sana, kuboost hayo mahitaji serikali inabidi ikope tena. Nina uhakika ni BOT ndiyo inayorestrict kiwango cha kuuza dola.

Kilimo ndio kinachangia fedha za kigeni nyingi nyuma ya dhahabu ndio maana serikali inakumbana na ugumu kuzuia chakula kuuzwa nje.
 
Hii kitu kwa mara ya kwanza nliisikia kwenye YouTube account ya Sky
Alitoa ufafanuzi wa kinachoendelea Duniani juu ya Dola na sio hapa Tanzania tuu hata mataifa kama china uturuk n.k ukitaka kununua vitu sahv wanataka utumie hela zao
Wanasema huo ni mpango wa kuondoa nguvu ya Dola Duniani
Wajuzi watakuja kutupa info zaidi
 
Sasa nchi yako bado ina import mpaka foodstuff, hapo lazima dola iadimike tu
Ku import vitu vingi kuliko ku export ni tatizo namba moja lakini..

Shida kubwa iko upande wa serikali yetu, wamekosa ubunifu kabisa
Nashauri yafuatayo

1. Serikali lazima iwekeze kwenye madini iwe na migodi yake yenyewe
Yaani watanzania tuchimbe na kuuza dhahabu, gesi, chuma nk
Lakini kufanikisha hili ni lazima iwekeze kwenye utafiti wa kutosha nasisitiza
UTAFITI WA KUTOSHA.
Hii itasaidia kuingiza fedha nyingi za kigeni kwenye nchi yetu hasa uuzaji wa dhahabu.

2. Serikali iboreshe bandari ya Dar es salaam
Kwa kununua vifaa vya kisasa na kufanya kazi 24hrs lakini pia itengenezwe bandari kavu kubwa kabisa Morogoro ili mizigo inapotoka bandarini ipelekwe Morogoro wahusika wa mikoa ya kanda ya ziwa kati na nje ya nchi watachukua mizigo hapo. Hii itaongeza ufanisi wa bandari na kuwavutia wateja zaidi.

3.Serikali ni lazima iwekeze kwenye kilimo na viwanda ili kupunguza uagizaji wa bidhaa nje ya nchi, kwanza kutoa ruzuku kwenye pembejeo zakilimo na kuandaa mazingira wezeshi kwa wazawa kufungua viwanda vya bidhaa zinazozalisha kwa wingi nchini mfano mkonge, pamba, alizeti, chikichi na karafuu.

Tukifanya hivyo tutaongeza uzalishaji, tutapata fedha nyingi za kigeni na tutaongeza mzunguko wa biashara na fedha nchini.
 
Hii kitu kwa mara ya kwanza nliisikia kwenye YouTube account ya Sky
Alitoa ufafanuzi wa kinachoendelea Duniani juu ya Dola na sio hapa Tanzania tuu hata mataifa kama china uturuk n.k ukitaka kununua vitu sahv wanataka utumie hela zao
Wanasema huo ni mpango wa kuondoa nguvu ya Dola Duniani
Wajuzi watakuja kutupa info zaidi
Umechanganya vitu viwili mkuu.

Tunazungumzia matumizi ya Dola kwenye manunuzi ya bidhaa kutoka nje ya nchi importation na sio manunuzi ya ndani
Ni sawa kuzuia matumizi ya dola kwa manunuzi na malipo ndani ya nchi lakini huwezi kufanya manunuzi ya nje kwa kutumia Tsh.

Mfanya biashara akitoka Tanzania kwenda Uturuki kununua nguo atakwenda na dola kwakua ndio pesa unayoweza kuibadili na kupata fedha nchi yoyote duniani kwa urahisi.
Matumizi ya Dola hayaepukiki.
 
Hii kitu kwa mara ya kwanza nliisikia kwenye YouTube account ya Sky
Alitoa ufafanuzi wa kinachoendelea Duniani juu ya Dola na sio hapa Tanzania tuu hata mataifa kama china uturuk n.k ukitaka kununua vitu sahv wanataka utumie hela zao
Wanasema huo ni mpango wa kuondoa nguvu ya Dola Duniani
Wajuzi watakuja kutupa info zaidi
Naweza nikaita hii ni propaganda, si china wala uturuki inayoweza zuia matumizi ya Dola hata North Korea, yaani unajaribu kusema kuwa ukienda na Dola kwenye hizo nchi ukichenji benki zitakataa?

Kilichopo Tanzania kuna upungufu WA foreign reserve fuatilia data za BOT utaona.

Hifadhi ya fedha za kigeni Tanzania Kwa sasa inatosheleza miezi minne Tu kipindi cha wakati 2022 ilikuwa miezi mitano mpaka sita(ripoti ya mwezi April 2023)
 
Hao waliokuelekeza ni waongo maana wao bado wana dollar nyingi sana.
Ungetoa maelezo kwanini Dollar imepungua Tz na sio story za kutumia Yuan
 
Naweza nikaita hii ni propaganda, si china wala uturuki inayoweza zuia matumizi ya Dola hata North Korea, yaani unajaribu kusema kuwa ukienda na Dola kwenye hizo nchi ukichenji benki zitakataa?

Kilichopo Tanzania kuna upungufu WA foreign reserve fuatilia data za BOT utaona.

Hifadhi ya fedha za kigeni Tanzania Kwa sasa inatosheleza miezi minne Tu kipindi cha wakati 2022 ilikuwa miezi mitano mpaka sita(ripoti ya mwezi April 2023)
Kwa ufupi Dollar nyingi zitakuja endapo tutakopa pesa zaidi au tusubirie msimu wa watalii
 
Daaah eti hali ni mbaya sana.kwani bibi yng kule masoko inamsIdiaje iyo dola? Mahindi,mtama,dagaa ananunua kwa dola.mpk useme ivyo.
 
Daaah eti hali ni mbaya sana.kwani bibi yng kule masoko inamsIdiaje iyo dola? Mahindi,mtama,dagaa ananunua kwa dola.mpk useme ivyo.
Ngoja nikusaidie mkuu,

Bibi yako unayemwongelea nina imani anavaa nguo, hizo nguo zinatoka China nk
Unahitaji dola kuzinunua na kuzileta hapa ili bibi
anunue na azivae.

Bibi yako akiumwa anatumia dawa lakini hatuna viwanda vingi vya dawa, zinaagizwa nje
Ili bibi azipate ni lazima ziagizwe nje kwa dola.

Umesema bibi yako anahitaji mahindi
Ili upate mahindi unahitaji mbolea
Serikali yako inaagiza mbolea nyingi nje ya nchi kwa kutumia dola.

Bibi yako anasafiri sio?
Magari, pikipiki nk yanatumia mafuta lakini hatuchimbi mafuta, serikali inatumia fedha nyingi sana (dola) kuagiza mafuta ili bibi yako apande gari kwenda sokoni kununua mahitaji uliyoorodhesha.
Yapo mengi sana lakini nadhani nimetumia lugha rahisi na utakuwa umenielewa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom