Ugonjwa wa Rubella ni Hatari zaidi Kuliko Ebola

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
51,360
22,658
Chanjo ni kuanzia tarehe 18 hadi 24 mwezi wa kumi.

Hospitali za serikali na private bure

pelekeni watoto na watu wazima pia

ugonjwa mbaya sana uko Mtwara na watoto wanakufa mbaya .. Wameamua kuchanja na watu wazima!
 
Chanjo tar 18/24 oct

hosp za serikali na privatebbure

pelekeni wattoto .na watuwazima pia


ugonjwa mbaya.sana uko.mtwara na watoto wanakufa mbaya ..wameamua kuchanja na watu wazima

mkuu hii habari inaonekana ni muhimu sana, tafadhali toa maelezo ya kina, ili na sisi tuwaelimishe wenzetu

unaambukizaje, dalili zake ni zipi, tuchukue tahadhari zipi, nk
 
Kuanzia tarehe 18 hadi 24 mwezi oktoba 2014, wizara ya afya na ustawi wa jamii inaendesha kampeni shirikishi ya chanjo ya surua na rubella katika mikoa yote 27 ya bara na visiwani. Chanjo ya surua rubella itatolewa kwa watoto kuanzia umriwa miezi 9 hadi chini ya miaka 15. Sambamba na utoaji wa chanjo, pia kutatolewa matone ya vitamin A kwa watoto wa umri wa miezi 6 hadi chini ya miaka 5, dawa za mebendaole za kutibu minyoo kwa watoto umri wa mwaka mmoja hadi chini ya miaka 5 na dawa za albendazole na ivermectin za kutibu mabusha, matende na minyoo tumbo kwa watu wa umri wa miaka 5 na kuendelea.
 
mkuu hii habari inaonekana ni muhimu sana, tafadhali toa maelezo ya kina, ili na sisi tuwaelimishe wenzetu

unaambukizaje, dalili zake ni zipi, tuchukue tahadhari zipi, nk

Sendoro:
Chanjo ya Surua Rubella itakayotolewa ina kinga dhidi ya ugnjwa wa surua na rubella. Surua na rubella husababishwa virus na huenezwa kwa njia ya hewa. Dalili zinafanana japo za rubella ni "mild", ambzo kati ya siku 8-21 za maambukizo mtoto atakuwa na dalii za joto kupanda, vipele vidogovidogo kuanzia usoni hadi miguui, na machokuwa mekundu.
Madhara ya Rubella kwa mama mjamzito asiye na kinga ni kuzaa mtoto njiti, kuzaa mtoto mwenye tundu katika moyo, au kuzaa mtoto mwenye mtindio wa ubongo.
Chanjo ya Rubella haijawhi kutolewa nchini na kampeni hii ndio itakuwa mara ya kwanza.
 
nadhani ulitaka kusema "ugonjwa wa rubella" (sio rubera);a.k.a german measles

thx dk wanse

msaada pls kuna wanaoitaji maelezo kidogo ya huu ugonjwa ..mi niliona kwa tv na kutumiwa msg na aar nikachanje watoto na sisi pia embu tussaidie zaidi
 
sendoro:
Chanjo ya surua rubella itakayotolewa ina kinga dhidi ya ugnjwa wa surua na rubella. Surua na rubella husababishwa virus na huenezwa kwa njia ya hewa. Dalili zinafanana japo za rubella ni "mild", ambzo kati ya siku 8-21 za maambukizo mtoto atakuwa na dalii za joto kupanda, vipele vidogovidogo kuanzia usoni hadi miguui, na machokuwa mekundu.
Madhara ya rubella kwa mama mjamzito asiye na kinga ni kuzaa mtoto njiti, kuzaa mtoto mwenye tundu katika moyo, au kuzaa mtoto mwenye mtindio wa ubongo.
Chanjo ya rubella haijawhi kutolewa nchini na kampeni hii ndio itakuwa mara ya kwanza.

wapwa twendeni kuchanjwa mi ntakuwa aar moroco saa tatu asbh na vikinda vyangu mungu akinipa nguvu
 
yani sinaga imani kabisa na hzo chanjo as long as zinatengenezwa na wazungu ambao ndo inawezekana wameyengeneza huo ugonjwa,, Mungu atuepushe tu
 
Wito kwenu kushiriki kikamilifu katika kampeni shirikishi ya Surua Rubella ambayo itatoa


  • Chanjo ya Surua Rubella kwa watoto wote walio katika umri wa miezi 9 mpaka chini ya miaka 15
  • Vidonge vya vitamin A kwa watoto wote wenye umri wa miezi 6 mpaka 59
  • Dawa za minyoo aina ya Mebendazole kwa watoto wote wenye umri wa miezi 12 hadi 59
  • Dawa ya Ivermectin na Albendazole zinazokinga Usubi, Minyoo ya Tumbo, Matende na Mabusha kwa umri wa miaka 5 na kuendelea kwa mikoa ya: Dar-es-salaam, Njombe, Iringa, Mbeya, Ruvuma, Morogoro, Tanga, Tabora, Katavi, Rukwa, Mtwara, Lindi, Pwani, Manyara, Singida, Dodoma.

LINI?

  • Kampeni itafanyika kitaifa kuanzia tarehe 18 hadi 24 Oktoba, 2014

Vituo vya kampeni

  • kliniki za huduma za afya ya uzazi na mtoto
  • Mashuleni
  • Stendi za mabasi
  • Stesheni za treni
  • Ofisi za Serikali za mitaa na
  • Sehemu yoyote inayoonekana na kufikika kwa urahisi na jamii na yenye nafasi ya kutosha kwa ajili ya mkusanyiko wa watu

Kama una maswali ruksa kuuliza.....


 
Zaidi ya watoto milioni moja na laki mbili kuanza kupewa chanjo ya surua mkoani Mbeya.
11(1).jpg

Zaidi ya watoto milioni moja na laki mbili wenye umri wa chini ya miaka mitano wanatarajiwa kupewa chanjo ya ugonjwa wa surua na rubella mkoani mbeya katika kipindi cha siku saba kuanzia jumamosi ya wiki hii.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa mbeya, Abbas Hussein Kandoro, mkuu wa wilaya ya mbeya, Prof. Norman Sigalla King amesema kuwa chanjo hiyo ambayo itaambatana na utoaji wa chanjo ya magonjwa ya usubi, mabusha na matende kwa watu wazima itaanza kutolewa jumamosi ijayo ya oktoba 18 na itaendelea hadi oktoba 24, mwaka huu, huku akiwataka wazazi kujitokeza kwa wingi kupeleka watoto wao na watu wazima kwenda kwenye vituo vya afya kupata chanjo hiyo.

Kwa upande wake mratibu wa chanjo mkoa wa mbeya,Japhet Mhaye amesema kuwa chanjo hiyo ni salama na imethibitishwa na shirika la afya duniani, hivyo hakuna sababu ya wazazi na watu wengine kuogopa kwenda kupata chanjo hiyo.

Ikiwa chanjo hiyo itatolewa kwa ufanisi ambao umekusudiwa, zaidi ya watu milioni mbili na laki nne wanatarajiwa kunufaika na kampeni hiyo. Mia
 
Chanjo ni kuanzia tarehe 18 hadi 24 mwezi wa kumi.

Hospitali za serikali na private bure

pelekeni watoto na watu wazima pia

ugonjwa mbaya sana uko Mtwara na watoto wanakufa mbaya .. Wameamua kuchanja na watu wazima!

Chanzo cha Ugonjwa wa Rubella ni nini? Na wapi Asili Yake?
 
Obama tusamehe,tumekukosea nini? Hiyo NWO inalenga kutuangamiza sisi wa afrika? Mie sichomi hiyo sindano na wala sihitajia,mababu zetu mbona hawakuumwa hilo gonjwa? Chris Brown shukrani kwa kuwaumbua wazungu.
 
Obama tusamehe,tumekukosea nini? Hiyo NWO inalenga kutuangamiza sisi wa afrika? Mie sichomi hiyo sindano na wala sihitajia,mababu zetu mbona hawakuumwa hilo gonjwa? Chris Brown shukrani kwa kuwaumbua wazungu.

Mkuu nidadavulie kidogo kuhusu Brown,
By The Way Sitachoma hizo sindano, kama magonjwa ya kutengeneza yameshatosha....
 
Mkuu nidadavulie kidogo kuhusu Brown,
By The Way Sitachoma hizo sindano, kama magonjwa ya kutengeneza yameshatosha....

Brown alitoa twiti kuhusu ebola alisema ni njia ya kupunguza population afrika ila wazungu wakammaindi maana aliongea ukweli magonjwa mengi hayo ni yakutengenezwa na hata hizi chanjo tunazowachoma hawa watoto itakuja kuwaghalimu sana usoni maana watakuja kuwa majoka ya kibisa na wanawake watakuwa hawana mayai kabisa.
 
Mkuu GAUTAMA Brown alitweet kwamba Ebola imetengenezwa ili ku control human population especially in Africa ingawaje wazungu walimgeuka na kumuita kwamba ni drug addicted na matusi mengine yaliyoratibiwa na BBC,CNN, SKY NEWS etc but kuna ukweli ndani yake ukitrace vizuri ugonjwa wenyewe. Wazungu wameamua kutumaliza na hamna wa kututetea viongozi wetu wameshasaini mikataba kwa kuongwa suti tuu . May God forbid this not happen.
Mkuu nidadavulie kidogo kuhusu Brown,
By The Way Sitachoma hizo sindano, kama magonjwa ya kutengeneza yameshatosha....
 
Last edited by a moderator:
Aisee acheni watuue tu kwasababu tumezidi kuwa mazuzu mburula na maamuma waliokubuhu. Tunajichibua tufanane kama wao na waohawapendi. Tunarogana kwa chuki ilmradi umuone mwenzako kafa anateseka ndio furaha. Acha watuue nyambaff zetu! !!
 
Kwa huu mpango wao hao Wazungu wamefanikiwa, sana ikiwa kama utakataa halafu unasema ugonjwa uko Mtwara umeuwa watu wengi sana.

Hapo hakuna namna lazima Watu wote wanywe dawa, Duh yaani hii kali pia ni huzuni hakuna pa kujitetea.
Ona sasa Ebola wanazuia kwenda Ulaya ili tufe
 
Back
Top Bottom