Dkt. Eva Wakuganda: Watoto Wanne kati ya 1,000 wanaozaliwa wanakuwa na matatizo ya Moyo

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Katika kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo inatarajiwa kuadhimishwa Machi 8, 2024, Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Dar Group iliyopo TAZARA Wilaya ya Temeke wanatarajia kutoa huduma kutoa Huduma za Tiba Mkoba(Outreach Service) kwa kufanya kambi maalumu ya upimaji na matibabu ya mogonjwa ya moyo kwa Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa jirani.

Kaimu Mkurugenzi wa JKCI- Dar Group Hospital, Iddi Lemmah amesema kuwa upimaji huo unatarajiwa kufanyika kwa watoto na Watu wazima kwa siku mbili kuanzia tarehe 2-3/03/2024 kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa 10 jioni katika hospitali ya JKCI Dar Group.

Ameeleza pia katika kambi hiyo kutakuwepo na wataalamu wa lishe ambao watatoa elimu ya lishe bora ambayo itawapa wananchi uelewa na kufuata mtindo bora wa maisha na kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo ambayo yanaweza kuepukika kwa kufuata ushauri wa kitaalumu.

Kaimu Mkurugenzi huyo ametoa rai kwa kuwataka wananchi kutumia fursa hiyo kupima afya zao kufahamu kama wana matatizo ili ikigundulika waanze matibabu mapema kuwaepusha na madhara zaidi.

Aidha, kwa upande wa Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa Watoto, ambaye ni Kaimu Mkuu wa Huduma za Tiba za Hospitali ya Dar Group, Dkt. Eva Wakuganda amesema sababu iliyochangia kuweka msukumo wa kusogeza huduma hizo ni wahusika wengi wenye matatizo ya moyo kushindwa kufika kwa wakati hospitalini.
photo_2024-03-02_09-29-56.jpg

photo_2024-03-02_09-29-55.jpg
"Tumeamua kuweka kambi hii kwa sababu matatizo mengi ya watoto na Watu wazima tumekuwa tukiwaona wagonjwa wakiwa wamechelewa."

Ameongeza kuwa kulingana na changamoto hiyo inaonesha kati ya watoto 1,000 wanaozaliwa kati yao watoto wasiopungua wanne wanakuwa na matatizo ya moyo, ambapo amesema kwa mwenendo huo inaonesha jambo hilo ni tatizo na kuwa hata baadhi ya watoto wenyewe matatizo hayo kumekuwepo na changamoto ya kuwapokea kwa wakati kwa sababu mbalimbali ikiwemo umbali pamoja na gharama.

Amesema kuwa kwa kuliona hilo Taasisi ya Moyo kupitia 'Tiba Mkoba' wameamua kuwasogezea wananchi huduma hizo.

"Wananchi wengi wanaweza kuwa na magonjwa hayo (magonjwa ya moyo) lakini wasifahamu kwa sababu magonjwa mengi yanaweza kuwa kimya kwa muda mpaka mgonjwa anakuja kufika hospitali anakuwa ameisha umwa sana kiasi kwamba matibabu yake yakuwa yameshakuwa na mambo mengi"

Sanjali na hayo Dkt. Eva ameeleza dalili mbalimbali za magonjwa ya moyo kwa watoto, ambazo ni pamoja na mtoto kuanza kuwa na mwonekano wa rangi ya bluu kwenye sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo kwenye midomo na kucha, changamoto ya upumuaji, kushindwa kuongezeka uzito, mapigo ya moyo kwenda mbio, mtoto kushindwa kula au akila anachoka na kutoka sana jasho.

Ameongeza kuwa matatizo hayo yanaweza kusababishwa na masuala mbalimbali ikiwemo, Mama mjamzito kuwa na kisukari, matumizi ya pombe kupindukia, uvutaji wa bangi pamoja na sababu nyingine ikiwemo kurithi, na kujifungua umri ukiwa umeenda.

Amesisitiza ni muhimu wananchi kufika eneo husika kunufaika na huduma hiyo itakayotolewa bure bila malipo.

Naye, Debora Mkemwa ambaye ni Mwakilishi wa Wanawake, JKCI - Dar Group amesema kuwa mpango huo kwa awamu hii umekuja kipindi ambacho yanaelekea maadhimisho ya siku ya Wanawake hivyo JKCI imeona umuhimu wa kuwahamashisha Wanawake kushiriki katika kufanikisha huduma hii kwa kuhamashisha familia zao ikiwemo watoto wao ili waweze kunufaika na huduma hiyo.

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom