Ugonjwa wa kifafa: Chanzo, Dalili, Huduma kwa Mgonjwa na Ushauri wa Matibabu

Mkuu snochet wewe huwa husomi thread za humu jamvini mpaka umkute mtu anaye uguwa ugonjwa fulani ndio uje hapa kuuliza maswali tafuta humu humu ndani ya JF. utapata jibu lako wewe uliza kila swali utapata jibu humuhumu ndani haya endelea kusoma hapa chini.

Kifafa ni ugonjwa wa ubongo.

Ubongo wa binadamu una mabilioni ya seli za neva.Zinashirikiana na kila moja kupitia chaji ndogo ndogo za umeme ambazo huwaka na kuzima.Wakati baadhi ya ama hizi seli zote kwa ghafla huanza kuwaka kwa pamoja, wimbi la nguvu za umeme hupita kwenye ubongo na husababisha kifafa ama kuzirai.

Kuzirai kwa ghafla huathiri vile ubongo hufanya kazi.Kunaweza kumsababisha mtu kupata mabadiliko ya ghafla katika fahamu, mwendo ama hisia.

Mshtuko wa moyo mmoja haumanishi ya kwamba mtoto ana kifafa.Kuzirai mara moja kunaweza kutokea kwa sababu tofauti k.m homa, jeraha la kichwa, kiwango cha chini cha sukari katika damu na kadhalika.

Kifafa ni jina la kuzirai kwa ghafla kunapotokea zaidi ya mara moja bila ya sababu ya kutibiwa inayojulikana.

Katika sehemu hii jifundishe zaidi kuhusu huu ugonjwa.


Dalili na ishara za kifafa Nitajuaje ikiwa niimeathiriwa na kifafa?

Kuna aina nyingi za kuzirai na mara kwa mara sio mgonjwa ambaye huona ishara za kifafa ilhali ni wale wanaomzunguka. Kuzirai kwingine hutokea kama kupotea kwa fahamu (ugonjwa wa kifafa usio mkali).

Hapa, mgonjwa (ambaye huwa ni mtoto) hupoteza makini kwa dakika kadhaa. Wakati huu, hawaitikii jina lao na hawawezi kusikia ama kuelewa chochote. Ni walimu ama wazazi ambao wataona ya

kwamba mtoto anazubaa. Wanapopataa nafuu, hawafahamu chochote kisicho cha kawaida kimefanyika. Watoto kama hawa huwa hawafanyi vizuri katika masomo kwa sababu kumakinika kwao huathiriwa.

Kuzirai kwingine hujumuisha kutingika ambako hakuwezi kudhibitiwa ama msukumano wa sehemu moja ama zaidi za mwili. Wakati huu, mtu hawezi kuzuia kutingika huku. Kutingika huku huanza kwenyewe na huisha baada ya mda fulani. Mgonjwa anaweza kujihisi akiwa mnyonge ama hana hisia katika sehemu hiyo ya mwili kwa mda baada ya kuzirai.

Aina nyingine ya kuzirai ni wakati mtu anapoanguka chini na kuanza kutetemeka katika mwili wake kwa kipindi fulani na kisha analala usingizi mzito (anapoteza fahamu). Aina hii ya kifafa inaogofya kutazama. Watu huwa hawana fahamu ya vitendo vyao na saa zingine wanapoamka hawawezi kukumbuka kile ambacho kimetoka kufanyika. Ni wale tu ambao walikuwepo wanaweza kuelezea ni nini kimetoka kufanyika.

Katika aina zingine za kifafa, mtu hupoteza udhibiti wa misuuli yake na huangusha kile walichokuwa wamekishikilia, hujikwa wanapojaribu kutembea ama huanguka chini wasiweze kujizuia ama kujilinda.

Kwa mukhtasari, wakati mtu anapothiriwa na kutetemeka kusikoweza kudhibitiwa kwa sehemu moja ama zaidi ya mwili wake ama anaanguka chini na kupoteza fahamu, hii inaweza kuwa dalili ya kifafa na ni muhimu kutafuta ushauri wa dakitari haraka iwezekanavyo.

Je kila mtu anayeathiriwa na kifafa anapaswa kupelekwa hospitalini?

La. Sio kila mtu anayeathirika na kifafa anapaswa kupatiwa huduma ya matibabu. Mtu mwenye kifafa ambaye yuko chini ya matibabu labda hahitaji kupelekwa hospitalini mara moja. Kuna visa vingine ambavyo ni muhimu kumpeleka mtu hospitalini kama dharura.


Kuzirai mara ya kwanza. Ikiwa mtu anafahamika ya kwamba huwa hana kifafa na kishe azirai, mtu huyu anahitaji kumuona dakitari mara moja.
  • Ikiwa kuzirai kumekaa zaidi ya dakika 5, mpeleke mgonjwa hospitalini.Hili huwa nadra lakini lifanyikapo huwa hatari sana na ni lazima umkimbize mgonjwa hospitalini hata ikiwa bado yuko katika hali hiyo ili kuokoa maisha yake.
  • Ikiwa kupumua hakurudii hali ya kawaida baada ya kuzirai.
  • Ikiwa kuzirai kutaisha na kujirudia tena mara hiyo hiyo Kabla ya mgonjwa kupata nafuu. Nitaendelea hii Topic ................. Habari zaidi kuhusu kifafa bonyeza hapa https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/156786-kifafa-ni-nini.html
 
Last edited by a moderator:
Baada ya miaka 3 ya ndoa, imegundulika kuwa mke wangu ana kifafa, nasikia kifafa ni hatari sana kwa wanawake, naomba kujua kuna tiba ya kifafa? kama hakuna natakiwa kufanya nini kuhusu ndoa yangu changa?

Ushauri pleaseee.
 
Baada ya miaka 3 ya ndoa, imegundulika kuwa mke wangu ana KIFAFA, nasikia kifafa ni hatari sana kwa wanawake, naomba kujua kuna tiba ya kifafa? kama hakuna natakiwa kufanya nini kuhusu ndoa yangu changa? Ushauri plzeeeeee

Mpende mkeo kama ulivyokula kiapo.
 
Kifafa ni nini?

Kifafa ni ugonjwa wa ubongo.

Ubongo wa binadamu una mabilioni ya seli za neva.Zinashirikiana na kila moja kupitia chaji ndogo ndogo za umeme ambazo huwaka na kuzima.Wakati baadhi ya ama hizi seli zote kwa ghafla huanza kuwaka kwa pamoja, wimbi la nguvu za umeme hupita kwenye ubongo na husababisha kifafa ama kuzirai.

Kuzirai kwa ghafla huathiri vile ubongo hufanya kazi.Kunaweza kumsababisha mtu kupata mabadiliko ya ghafla katika fahamu, mwendo ama hisia.

Mshtuko wa moyo mmoja haumanishi ya kwamba mtoto ana kifafa.Kuzirai mara moja kunaweza kutokea kwa sababu tofauti k.m homa, jeraha la kichwa, kiwango cha chini cha sukari katika damu na kadhalika.

Kifafa ni jina la kuzirai kwa ghafla kunapotokea zaidi ya mara moja bila ya sababu ya kutibiwa inayojulikana.

Katika sehemu hii jifundishe zaidi kuhusu huu ugonjwa.


Dalili na ishara za kifafa

Nitajuaje ikiwa niimeathiriwa na kifafa?
Kuna aina nyingi za kuzirai na mara kwa mara sio mgonjwa ambaye huona ishara za kifafa ilhali ni wale wanaomzunguka. Kuzirai kwingine hutokea kama kupotea kwa fahamu (ugonjwa wa kifafa usio mkali). Hapa, mgonjwa (ambaye huwa ni mtoto) hupoteza makini kwa dakika kadhaa. Wakati huu, hawaitikii jina lao na hawawezi kusikia ama kuelewa chochote. Ni walimu ama wazazi ambao wataona ya kwamba mtoto anazubaa. Wanapopataa nafuu, hawafahamu chochote kisicho cha kawaida kimefanyika. Watoto kama hawa huwa hawafanyi vizuri katika masomo kwa sababu kumakinika kwao huathiriwa.

Kuzirai kwingine hujumuisha kutingika ambako hakuwezi kudhibitiwa ama msukumano wa sehemu moja ama zaidi za mwili. Wakati huu, mtu hawezi kuzuia kutingika huku. Kutingika huku huanza kwenyewe na huisha baada ya mda fulani. Mgonjwa anaweza kujihisi akiwa mnyonge ama hana hisia katika sehemu hiyo ya mwili kwa mda baada ya kuzirai.

Aina nyingine ya kuzirai ni wakati mtu anapoanguka chini na kuanza kutetemeka katika mwili wake kwa kipindi fulani na kisha analala usingizi mzito (anapoteza fahamu). Aina hii ya kifafa inaogofya kutazama. Watu huwa hawana fahamu ya vitendo vyao na saa zingine wanapoamka hawawezi kukumbuka kile ambacho kimetoka kufanyika. Ni wale tu ambao walikuwepo wanaweza kuelezea ni nini kimetoka kufanyika.

Katika aina zingine za kifafa, mtu hupoteza udhibiti wa misuuli yake na huangusha kile walichokuwa wamekishikilia, hujikwa wanapojaribu kutembea ama huanguka chini wasiweze kujizuia ama kujilinda.

Kwa mukhtasari, wakati mtu anapothiriwa na kutetemeka kusikoweza kudhibitiwa kwa sehemu moja ama zaidi ya mwili wake ama anaanguka chini na kupoteza fahamu, hii inaweza kuwa dalili ya kifafa na ni muhimu kutafuta ushauri wa dakitari haraka iwezekanavyo.

Je kila mtu anayeathiriwa na kifafa anapaswa kupelekwa hospitalini?

La. Sio kila mtu anayeathirika na kifafa anapaswa kupatiwa huduma ya matibabu. Mtu mwenye kifafa ambaye yuko chini ya matibabu labda hahitaji kupelekwa hospitalini mara moja. Kuna visa vingine ambavyo ni muhimu kumpeleka mtu hospitalini kama dharura.

  • Kuzirai mara ya kwanza. Ikiwa mtu anafahamika ya kwamba huwa hana kifafa na kishe azirai, mtu huyu anahitaji kumuona dakitari mara moja.
  • Ikiwa kuzirai kumekaa zaidi ya dakika 5, mpeleke mgonjwa hospitalini.Hili huwa nadra lakini lifanyikapo huwa hatari sana na ni lazima umkimbize mgonjwa hospitalini hata ikiwa bado yuko katika hali hiyo ili kuokoa maisha yake.
  • Ikiwa kupumua hakurudii hali ya kawaida baada ya kuzirai.
  • Ikiwa kuzirai kutaisha na kujirudia tena mara hiyo hiyo Kabla ya mgonjwa kupata nafuu.

Je, kuna tiba ya kifafa?

Mara nyingi kile kinachosababisha kifafa hakijulikani, ugonjwa huu hauna tiba inayotambulika. Wakati mtu anapoathiriwa na kuzirai kwa sababu ya hali zingine kama vile uvimbe kwenye ubongo ,ugonjwa wa figo au ugonjwa wa ini unaweza kuwa na nafasi ya tiba ikiwa hali hiyo nyingine imetibiwa. Katika visa vingine, hata hivyo kuzirai huendelea hata kama ikiwa hali hiyo nyingine imeshughulikiwa.

Ugonjwa wa kifafa unaweza kudhibitiwa kwa kutumia madawa na kufuata matibabu ya mara kwa mara. Ugonjwa wa kifafa uliodhibitiwa vizuri hupunguza idadi ya visa vya kuzirai vinavyomkumba mtu na wakati mwingi mgonjwa hazirai kwa mda mrefu. Hali hii haitibiwi na mgonjwa anaweza kurejelea kuzirai wakati wowote. Dawa hutumiwa KUDHIBITI kuzirai lakini sio kutibu.
 
Jinsi nyingine za kudhibiti kifafa

Kando na madawa, ni nini kingine ambacho kinaweza kunisaidia ikiwa niko na kifafa?

Imeonekana ya kwamba kuna vitu ambavyo vinaweza kusababisha mshtuko kwa mtu aliye na kifafa ikiwa hata

amedhibitiwa na matibabu. Kukosa usingizi wa kutosha (mtu mzima anahitaji angalau masaa 8 ilhali mtoto anahitaji

angalau masaa 9
) kunaweza kusababisha mshtuko wa kifafa. Mfadhaiko mwingi utokanao na matatizo unaweza pia

kusababisha shambulizi. Homa katika watoto imejulikana kuongeza nafasi ya kutokea kwa mshtuko wa kifafa. Taa

zinazomemeteka kama vile kioo cha runinga na mataa ya disko yanaweza kusababisha mshtuko wa kifafa katika watu

wengine. Kupumua kwa nguvu wakati unapumzika kumetambuka kusababisha mshtuko. Hutokea mara kwa mara katika

watoto wakati wako kwenye hali ya kuogopesha sana ama hofu kubwa. Ukiwa unaweza kuepuka haya, unaweza
kujisaidia kuepuka kushikwa na mshtuko wa kifafa.


Kwa nini haupaswi kumwekea mtu kitu mdomoni anaposhikwa na mshtuko wa kifafa?

Kwa mda mrefu iliaminika ya kwamba wakati mtu ameshikwa na kifafa, mgonjwa anaweza kumeza ama hata kunyongwa na ulimi wake na kwa hivyo kusababisha kifo. Hivi sasa hali imebadilika na inaeleweka ya kwamba hakuna haja ya kuweka kitu chochote kwenye mdomo wa mgonjwa anaposhikwa na kifafa. Hili linaweza kusababisha madhara zaidi.

Wakati wa kifafa kuna mshtuko wa ghafla wa misuli.Mikono, miguu na sehemu zingine za mwili huwa na mwendo wa kujirudia rudia ambao ni vigumu kuukabili kwa kutumia nguvu haswa ikiwa mgonjwa ni mkubwa kwa umbo. Kama sehemu ya tendo la misuli, mgonjwa husaga meno yake kwa sababu ya tendo la nguuvu katika taya. Jaribio lolote la kuweka kitu kwenye mdomo linaweza kusababisha kuvunjika kwa meno ya mgonjwa, kunyongwa na kile kilichowekwa mdomoni ama mgonjwa kumuuma vibaya mhudumu wake.

Kwa hivyo fahamu: USIWEKE kitu katika mdomo wa mgonjwa anaposhikwa na mshtuko wa kifafa.

Kwa nini wagonjwa wa kifafa hawawezi kugawana madawa yao?

Madawa ya kifafa hufanya kazi ya kukomesha shughuli zisizo za kawaida kwenye ubongo. Kuna aina nyingi za kuzirai katika kifafa na hizi zote huitikia kwa njia tofauti kwa madawa tofauti. Hii ndio sababu ya kwanza kwa nini haufai kugawa dawa za kifafa. Dawa ambazo hudhibiti aina moja ya kifafa zinaweza kukosa athari kwa aina nyingine ya kifafa.

Pili, watu tofauti wanahitaji vipimo tofauti vya dawa iliyotolewa kudhibiti kifafa. Ugonjwa wa kifafa unamaanisha ya kwamba ubongo wa mtu unaweza kufyatuka kwa njia isiyo ya kawaida. Watu tofauti hupata kifafa katika viwango tofauti vya mchangamsho wa ubongo. Watu wengine huchangamshwa kwa urahisi na kuzirai ilhali wengine hawachangamshwi kwa urahisi. Kipimo cha dawa kinachotumiwa kumdhibiti mtu ambaye huzirai kwa urahisi ni tofauti na kile cha yule ambaye hazirai kwa urahisi.

Tatu, sio vizuri kugawana madawa ambayo yametolewa kufuatia maagizo ya dakitari. Maagizo ya dakitari hutoa dawa kwa mtu mmoja kwa kipindi maalumu cha wakati. Kwa kugawana madawa, mtu ambaye alipewa maagizo ya dakitari ataishiwa na dawa kabla ya ahadi ya kuonana na dakitari inayofuatia. Wanweza kuzirai kwa urahisi kwa sababu hawako kwenye matibabu. Sio salama kwa mtu mwenye kifafa kugawa dawa zake.

Matatizo yaweza tokezea wakati wa matibabu?

Je kuna jambo ambalo linaweza kuenda mrama nikiwa bado kwenye matibabu?


Athari ya matibabu ni hisia ya kusinzia na kutokuwa mwepesi ambako hutoweka baada ya mda. Baadhi ya madawa yanaweza kumfanya mgonjwa aongeze uzito. Athari mbaya zaidi ambayo inaweza kutokea ni kwenye ini. Hili ni jambo la kawaida wakati mgonjwa anatumia madawa kadhaa ili adhibiti kifafa.


Unapoanza matibabu, athari yake kwa kifafa huwa siio ya papo kwa hapo. Inachukua angalau mwezi mmoja kuona athari yoyote ya kudumu na mtu anahitajiwa kuwa mvumilivu. Katika visa vichache, visa vya kuzirai vinaweza kuongezeka unapowekwa kwenye matibabu kabla kuzirai hakujapungua.


Ni kipi kipimo cha dawa za kutibu kifafa?

Kipimo cha dawa ni kile ambacho kitatibu kitadhibiti ama kitatibu hali hii bila ya kusababisha mathara mabaya ya kando. Hii hutofautiana kutoka kwa matibabu hadi matibabu na hali hadi hali. Dawa zingine kama Panadol zina kiwango chake rasmi; watu wazima humeza vidonge 2 kila masaa 6-8. Hali zingine kama malaria isiyo kali zina kiwango cha dawa kinachopeanwa katika kiwango cha kipimo cha dawa kama watu wazima humeza vidonge 2 vya Camoquine mara moja kwa siku 3.

Hesabu ya kiwango cha kipimo cha dawa hutegemea uzani wa mgonjwa ama umri wake. Kila aina ya dawa ina kipimo kwa uzani ama umri wa mgonjwa uliopeanwa.

Katika visa vingine vya kifafa, kiwango cha dawa hakiwezi kuhesabika kwa urahisi. Matibabu yanayotolewa ili kudhibiti kifafa huathiriwa kwa urahisi na vipimo vya dawa na hufanya kazi katika kadiri ndogo. Dawa kidogo kwenye damu ama dawa nyingi kwenye damu na udhibiti wa kifafa hupotezwa. Kwa hivyo kila dawa inaweza tu kutumiwa katika kadiri iliyotolewa ya kipimo cha dawa. Ikiwa kuzirai hakuwezi kudhibitiwa katika kadiri hii,dawa ya pili na saa zingine dawa ya tatu inaweza kuongezwa. Hii nyongeza ya madawa hujiathiri na kipimo cha kila dawa kinahitaji kuhesabiwa mara tena ili kila dawa ikuwe katika kiwango kinachofaa katika damu.

Kufanya mambo kuwa magumu zaidi, kutokea kwa kifafa hakuwezi kutabirika katika watu tofauti. Kuna wale ambao ugonjwa wao wa kifafa unaweza kudhibitiwa kwa urahisi ilhali wengine wanahitaji matibabu 2-3 ili kupunguza visa vya kuzirai bila ya kuvimaliza kabisa. Kwa wagonjwa 2 wenye umri sawa na uzani sawa, matibabu ya kipekee yanaweza kutolewa katika vipimo tofauti ili kudhibiti kuzirai kwao.

Ni kwa mda upi ambao mtu aliyeathiriwa na kifafa anapaswa kutumia dawa?

Mtu aliyeathiriwa na kifafa anapaswa kutumia madawa aliyopewa hadi ashauriwe vingine. Kwa kutegemea wingi wa kutokea kwa visa vya kifafa, wagonjwa wanaweza kutumia dawa kwa maisha yao yote.Katika watoto,hata hivyo mambo yanabadilika. Kitambo, ilichukuliwa ya kwamba mtoto mwenye kifafa angehitajika kutumia madawa kwa miaka mingi ya maisha yake. Lakini hali sio hivyo tena. Ikiwa mtoto anatumia madawa kwa njia inayofaa na kwa wakati bila ya kukosa hata kipimo.cha dawa na anabakia bila kifafa kwa angalau miaka 2, basi dakitari anaweza kufikiria kusimamisha utumizi wa madawa. Ni dakitari pekee yake anayeweza kutoa ushauri kuhusu kusimamaisha matumizi ya madawa ya kifafa baada ya kumfuatilia mgonjwa kwa kipindi fulani cha mda. Ni muhimu maamuzi haya yafanywe na dakitari, kwa sababu mwanzo utumizi wa madawa umeanza haufai kukatizwa kwa ghafla. Badala yake dakitari atapunguza kipimo cha dawa pole pole hadi matumizi ya dawa umesitishwa. Ukisitisha dawa kwa ghafla, kuna madhara ya kando kama kumwa na tumbo, kutapika na kutomakinika na kuzirai kunaweza kujirudia.

Kwa hivyo, jambo muhimu ni kuzungumza na dakitari wako kuhusu kusimamisha matibabu. Ikiwa mtoto hajafuzu kwa ajili ya kusitishwa matibabu kwa sasa, na kisha aendele kutokana na ushauri wa dakitari. Ikiwa mtoto atafuzu, basi hili linafaa kufanywa kwa utaratibu. Wakati kipimo cha dawa kinapunguzwa, ni muhimu kukumbuka ya kwamba mtoto anaweza kushikwa na kifafa. Waweke wakiwa salama na waangalie kwa karibu hadi dawa zote zimesitishwa kabisa na kila kitu kiko salama.
 
Ni nini ninachopaswa kufanya ikiwa mtu atashikwa na mshtuko wa kifafa?

Wakati mwingi, huduma ya kwanza ina maana ya kumfanya mtu awe salama wakati mshtuko wa kifafa unapotokea. Kwa bahati nzuri, mshtuko huwa mfupi na huisha baada ya dakika kadhaa.

Hatua ya kwanza katika kujitayarisha kwa ajili ya kifafa ni kufahamu kitu cha kufanya wakati ugonjwa huu unapotokea. Hii ni muhimu ikiwa unamchunga mgonjwa wa kifafa lakini pia kwa kila mtu. Ugonjwa wa kifafa unaweza kuanza katika umri wowote na kila mtu anahitaji kufahamu nini cha kufanya wakati mtu karibu nao anaathiriwa na kifafa.

Huduma ya Kwanza

  • Kuwa mtulivu na usiogope. Kifafa humuogopesha mtazamaji. Huchukua dakika chache na kwa kawaida huhitaji matibabu.Kumbuka ya kwamba mtu aliyeshikwa na kifafa huwa hafamu vitendo vyake na anaweza au asiweze kukusikia.
  • Walinde dhidi ya majeraha wakati wanaposhikwa na kifafa.Ikiwa inahitajika mweke chini kwa njia iliyo taratibu.
  • Sogeza vitu vigumu, vitu vyenye ncha kali na vilivyo moto na linda kichwa na mwili wa mgonjwa dhidi ya jeraha.
  • Usiweke chochote mdomoni ama ujaribu kubanua meno.
  • Mtu hayuko katika hatari ya kumeza ulimi wake
  • Usijaribu kuzuia mwendo wao kwa kutumia nguvu.Hili linaweza kusababisha majeraha kwa mgonjwa na pia yule anayejaribu kuwasaidia.
  • Popote inapowezekana, jaribu kumlaza mtoto katika sehemu iliyo laini na wageuze upande mmoja.
  • Weka kitu tambarare na laini chini ya kichwa chake ili asijiumize.
  • Fungua nguo zilizombana haswa kwenye shingo kama tai, skafu na kadhalika
  • Usiweke chochote mdomoni.
  • Nakili mda ambao mshtuko umechukua.
  • Jaribu kutazama mwondoko ambao mtu hufanya wakati ameshikwa na kifafa.
  • Wakati mkutuo unaanza kupungua, hakikisha ya kwamba kupumua kumerudia hali yake ya kawaida.
  • Baada ya kifafa, mvingirishe mtu ili alalie upande mmoja.Hili hufanya mate kutoka mdomoni na kuhakikisha ya kwamba hanyongwi. Ikiwa kuna matapishi, mweke mtu kwa upande mmoja na safisha mdomo wake kwa kidole.
  • Usijaribu kumpatia dawa ama uoevu hadi aamke
  • Waondolee hofu, zungumza nao kwa upole na wasaidie kupata nafuu pole pole.
  • Usimwache mtu pekee yake hadi apate nafuu.
Ni nini ninachopaswa kufanya ikiwa nadhani nimeathiriwa na kifafa?

Ni muhimu kukumbuka ya kwamba kifafa ni hali ambayo inaweza kudhibitiwa. Sio kitu cha kuona haya. Sio laana ama ulemavu. Ni hali inayohitaji matibabu na kufuatiliwa kama hali zingine kama shinikizo la juu la damu, kisukari, pumu na kadhalika

Ikiwa unadhani ya kwamba umeathiriwa na ugonjwa wa kifafa ama ikiwa umewahi kuanguka chini na kuzimia ni muhimu kutafuta usaidizi wa dakitari aliye karibu. Ikiwa inawezekana andamana na mtu aliyekuwa nawe wakati ikifanyika ili waeleze kile walichokiona. Hili litasaidia dakitari kufanya ubainifu sahihi.

Ni sehemu gani ya ubongo huathiriwa na kifafa?

Ubongo ni ogani iliyo na sehemu nyingi (sehemu ya mwili) ambazo hudhibiti mwili wote. Sehemu tofauti za ubongo hudhibiti sehemu tofauti za mwili na kazi tofauti kwenye mwili. Kuna sehemu ya ubongo ambayo hudhibiti misuli ya mkono; sehemu tofauti itadhibiti kuhisi uchungu wa mkono huo huo na sehemu tofauti ya ubongo itaratibu sauti ya kupiga mayowe wakati mkono huo unahisi uchungiu ama uko kwenye hatari. Hizi sehemu zimeunganishwa na seli za ubongo (nyuroni). Muungano huu ndio ule unaoturuhusu kufanya kazi kama mtu mmoja kwa njia ya kupatana kwa misuli.

Kifafa ni shughuli isiyo ya kawaida kwenye ubongo. Sehemu yoyote ya ubongo inaweza kupatwa na jambo hili lisilo la kawaida. Kwa sababu sehemu tofauti za ubongo hudhibiti sehemu tofauti za mwili, hii ndiiyo sababu mtukutiko wa maungo katika kifafa ni tofauti kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine ama pia kutoka kwa kuzirai huku na kule. Ikiwa kuna shughuli isiyo ya kawaida kwenye ubongo katika sehemu ya ubongo inayoathiri misuli ya mikono na miguu, kutakuweko msukumano mwingi katika hizo sehemu za mwili.

Shughuli hii isiyo ya kawaida kwenye ubongo inaweza kufanyika tu katika sehemu moja ya ubongo ama inaweza kusambaa katika muungano ili kuhusisha ubongo wote.Kuzimia ambako husababishwa na shughuli ya sehemu moja ya ubongo ndio kule tunakokuita kuzirai kusio kamili. Kuzirai kunakosababishwa na shughuli ya ubongo wote ndio kule tunakokuita ugonjwa wa kifafa ulio mbaya ama kuzimia kamili.

Kwa jumla tunaweza kusema ya kwamba ikiwa sehemu ndogo ya ubongo itaathirika basi mtukutiko wa maungo utakao onekana utakuwa mdogo. Ikiwa sehemu kubwa ya ubongo itaathirika basi mtukutiko wa maungo utakao onekana utakuwa mkubwa. Kuzirahi kusio kamili kutaathiri sehemu ndogo ya ubongo kuliko kuzimia kuliko kamili.


Ni vipi naweza kujilinda mimi mwenyewe na familia yangu dhidi ya kifafa?

Njia moja muhimu ya kuwalinda watoto dhidi ya hatari ya kifafa ni kuhakikisha ya kwamba wanapata chanjo zao kwa wakati unaofaa. BCGkwa mfano humlinda dhidi ya kifua kikuu. Ugonjwa wa kifua kikuu umekuwa ugonjwa wa kawaida hivi leo na unapoathiri mtoto mdogo ambaye hajapata chanjo, hatari ya kupata ugonjwa homa ya uti wa mgongo (meningitis) huongezeka. Homa ya uti wa mgongo itamweka mtoto kwenye hatari kubwa ya kupata kifafa. Chanjo zingine maalumu kwa aina tofauti za homa ya uti wa mgongo zinapatikana hospitalini lakini kwa ada.

Homa ni kitu kinachoongezea hatari ya kupatwa na mshtuko ilhali inaweza kudhibitiwa vyema. Mtoto ambaye homa yake inaruhusiwa kupanda juu yuko katika hatari ya kupatwa na mshtuko. Ni muhimu kwa homa kudhibitiwa vizuri pindi tu inapoanza. Udhibiiti wa homa unajumuisha; kutumia dawa kama Panado (paracetamol) ama Brufen(Ibuprofen), mtoe mtoto nguo kisha umpanguze na kitambaa kilicholoweshwa ndani ya maji yenye joto la kadri na la muhimu zaidi ni kutafuta msaada wa matibabu.

Ulinzi dhidi ya jeraha, haswa jeraha kwenye kichwa ambayo ndiyo sababu nyingine ya kifafa. Ulinzi hutokana na kuhakikisha ya kwamba watoto hawezi kuanguka kwa urahisi kutoka katika sehemu iliyo juu, usimamizi unaofaa wanapocheza na kuweka mbali vitu ambavyo vinaweza kuwaletea madhara wanapocheza. Unaposafiri kwenye gari, ni muhimu kutumia mishipi ya usalama ili kupunguza hatari ya kujeruhiwa ikiwa kutatokea ajali. Jeraha la kichwa ndilo jeraha ambalo hutokea mara kwa mara kukitokea ajali.
 
Ni wapi naweza kuenda ikiwa sitapata usaidizi?

Kuzirai ambako hakuwezi kudhibitiwa kunaweza kuwa hatari kwa mgonjwa.Huwa hakuwezi kubashiriwa na unaweza kufanyika wakati mgonjwa yuko karibu na moto, anaendesha gari ana jaribu kuvuka barabara, anaogelea ama anafanya kazi akiwa juu (k.m juu ya paa la nyumba). Katika hali hii, kuzirai kutamweka mtu katika hatari kubwa kwani anaweza kuchomeka, kupatwa na ajali, kuzama ama kuanguka na kuumia. Hii ni sababu moja muhimu ambayo inahitaji kifafa kudhibitiwa.

Pili, ugonjwa wa kifafa unaweza kutokea mara kwa mara ukiwa hautadhibitiwa. Kuzimia kunaweza kutokea mara kwa mara na kuonekana ni kama unaendelea. Hii ni dharura ya kimatibabu ambayo inaweza kusababisha kifo katika mda mfupi. Kwa hivyo ikiwa mgonjwa ataathiriwa na kifafa kwa zaidi ya dakika 5, mpeleke katika hospitali iliyo karibu haraka iwezekanavyo kwa sababu kuzimia hakuwezi kuisha bila ya dawa.

Nitapata usaidizi wapi?

Hospitali iliyo karibu nawe itakutolea usaidizi. Watakuwa na dakitari ambaye atakuchunguza na atakushauri kuhusu uchunguzi wowote ama matibabu ambayo unaweza kuhitaji kutumia.
Pia unaweza kuwasiliana na shirika linalowashughulikia walio na kifafa nchini Tanzania.

Tambua uwongo unaozungumziwa kuhusu Kifafa

Kifafa ni aina ya ulemavu kwani huathiri utenda kazi wa ubongo

Ulemavu ulielezewa vizuri na Shirika la Afya Duniani mnamo mwaka wa 1976. Unatofautisha dhana tatu ambazo hutumiwa sana na unadhihirisha baina ya kudhoofika, ulemavu na upungufu.

Kudhoofika
ni upungufu wowote ama hali ya akili isiyo ya kawaida (saikolojia), utenda kazi wa mwili (fiziolojia) ama muundo wa mwili wa binadamu (anatomia) ama utenda kazi; Ulemavu ni kikwazo ama kukosa uwezo (unaotokana na upungufu) wa kufanya shughuli kwa njia inayochukuliwa kuwa ya kawaida kwa binadamu; Upungufu ni kasoro inayotokea kwa mtu kwa sababu ya kudhoofika ama ulemavu ambao huzuia kutimilika kwa wajibu unaochukuliwa kuwa wa kawaida (kwa kutegemea umri, jinsia na mambo ya ushirikiano wa jamii na utamaduni) kwa mtu huyo.

Kifafa ni matokeo ya utenda kazi wa ubongo usio wa kawaida ama kudhoofika kwa utenda kazi wa ubongo.Huathiri utenda kazi wa ubongo kwa kuendelea na kuwacha. Kuna hali zingine ambazo huwa na athari inayoendelea na ya mda mrefu. Hizi hali hutokea kama kutoona vizuri, kutowiiana vizuri,kuongea pole pole,kutoweza kumakinika na kusahausahau. Hali hizi huitwa ulemavu ama taahira ya akili.

Ugonjwa wa kifafa unaweza kumshika mtu mwenye hali/ulemavu mwingine. Unaweza pia kutokea tu wenyewe. Mgonjwa wa kifafa ambaye yuko chini ya matibabu na anafuatiliwa mara kwa mara anaweza kutimiza majukumu yake kama mtu yeyote mwingine. Katika hali hii hadhaniwi kuwa na ulemavu wowote. Ikiwa kuzirai kunakosababishwa na kifafa kumeongezeka na kunamzuia mtu kufanya kazi yake ya kawaida, basi hili huchukuliwa kuwa ulemavu.

Kifafa hutokea kwa sababu ya kupagawa na mapepo

MziziMkavu
 
DAWA YA MARADHI YA MARADHI YA KIFAFA:


Kila Tiba kati ya zifuatazo ni yenye kujitegemea.Chagua iliyo rahisi kwako.Isipokufaa ndipo uchague nyengine


TIBA 1:
Chukua udi swalib (udi sulb) kijiko kimoja cha chai (5ml),chukua na kijiko kimoja cha chakula (10ml) cha mbegu za habbat Sawda.
Twanga pamoja halafu changanya na Asali safi ya nyuki kijiko kimoja (10ml).
Tumia mchanganyiko huu kutwa mara tatu (1×3) kwa muda wa miezi mitatu hata mwaka mmoja (miezi 3-miezi12).

TIBA 2:
Kunywa maji yaliyochemshwa na Harmal.Kisha baada ya kunywa ujipake kifuani Mafuta ya Habat Sawda na unywe kijiko kimoja (10ml) cha mafuta hayo.

Tumia Dawa kisha uje unipe Feedback.By MziziMkavu.
 
DAWA YA MARADHI YA MARADHI YA KIFAFA:

Kila Tiba kati ya zifuatazo ni yenye kujitegemea.Chagua iliyo rahisi kwako.Isipokufaa ndipo uchague nyengine
TIBA 1:
Chukua udi swalib (udi sulb) kijiko kimoja cha chai (5ml),chukua na kijiko kimoja cha chakula (10ml) cha mbegu za habbat Sawda.
Twanga pamoja halafu changanya na Asali safi ya nyuki kijiko kimoja (10ml).
Tumia mchanganyiko huu kutwa mara tatu (1×3) kwa muda wa miezi mitatu hata mwaka mmoja (miezi 3-miezi12).

TIBA 2:
Kunywa maji yaliyochemshwa na Harmal.Kisha baada ya kunywa ujipake kifuani Mafuta ya Habat Sawda na unywe kijiko kimoja (10ml) cha mafuta hayo.

Tumia Dawa kisha uje unipe Feedback.By MziziMkavu.

Mkuu Asante sana, Ubarikiwe. Je dawa hizi zinapatikana wapi?
 
Asante mkuu. Kuna mtu alikuwa anashida hii na mkewe. Bahati mbaya sikumbuki ni nani. Nna maswali mawili na mshangao.mmoja.

Mshangao: kumbe udi unaweza kuliwa?

Maswali :
ati phernababitone ni dawa ya kifafa? Kwa sababu nilidhani ni kwa.ajili ya pumu tu.

Pili, myu mwenye kifafa mwanamke, hawezi kubeba mimba chini ya uangalizi wa katibu? Tulikuwa na house maid mwenye kifafa, alipewa dawa na tulikaa nae kwa miaka 5 bila kuanguka. Na kilichomuondoa ilikuwa mimba.
 
Asante mkuu. Kuna mtu alikuwa anashida hii na mkewe. Bahati mbaya sikumbuki ni nani. Nna maswali mawili na mshangao.mmoja.

Mshangao: kumbe udi unaweza kuliwa?

Maswali :
ati phernababitone ni dawa ya kifafa? Kwa sababu nilidhani ni kwa.ajili ya pumu tu.

Pili, myu mwenye kifafa mwanamke, hawezi kubeba mimba chini ya uangalizi wa katibu? Tulikuwa na house maid mwenye kifafa, alipewa dawa na tulikaa nae kwa miaka 5 bila kuanguka. Na kilichomuondoa ilikuwa mimba.
bibie King'asti Sio Udi wa kawaida huo ni udi wa Dawa unaitwa kwa jina ( Chukua udi swalib (udi sulb) Hii Dawa
Sio huo Udi unaofikiria wewe wanaojifukiza wanawake kwenye nguo zao huu Udi ni wadawa.
 
Last edited by a moderator:
bibie King'asti Sio Udi wa kawaida huo ni udi wa Dawa unaitwa kwa jina ( Chukua udi swalib (udi sulb) Hii Dawa Sio huo Udi unaofikiria wewe wanaojifukiza wanawake kwenye nguo zao huu Udi ni wadawa.
Ohoo, asante kwa kunielimisha. Nakiri sijui aina za udi. Naomba tafadhali unijibu masuali yangu mawili nipate kuelimika.
 
Habari wanaJF,

Nina rafiki yangu wa karibu anaumwa ugonjwa wa kuanguka, yaani kifafa kwa muda mrefu sasa ameangaika hospitalini mpaka kwa wanganga wa kienyeji na kutumia dawa mbalimbali bila mafanikio.

Tafadhali mwenye kujua lolote kuhisiana na tiba naomba anijuze ili tumsaidie ndugu yetu huyu jamani. maoni, mawazo, ushauri na lolote ujualo unakaribishwa.

Asante sana
 
Back
Top Bottom