Ugonjwa wa Corona tumekuwa kituko cha kutolewa mifano

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,823
35,829
Moja kwa moja kwenye mada. Waswahili wanasema asiyejua maana haambiwi maana.

Kwamba haka kaugonjwa ni ka upepo tu katapita. Na kwa kuwa sisi tu wacha Mungu sana sijui kuliko nani, basi sisi tumemwachia yeye.

Vipi mambo yakienda ndivyo sivyo (katu hatuombei hivyo), je tutasema Mungu katususa?

Why This Controversial Kenyan-American Professor is very Unhappy With President Magufuli

Kwa kuwa fair tu tunapaswa sana kujitathmini.

Kama tunadhani tuko sawa basi tuna matatizo (incurable) ambayo labda ni makubwa zaidi kuliko hata Corona yenyewe.

Kama ni hivi tunaelekea kwenye kutakana kuachia ngazi.

It can't be like this.
 
Iwapo kiongozi wa juu kabisa ameamini hivyo..yawezekana akawa sahihi au asiwe sahihi maana kila jambo lifanywalo kwa Imani lina matokeo yake either positive or negative..yote yanawezekana maana hata huyo professor anaweza asiwe sahihi pia kwa kumkosoa mwenye Imani
 
Magufuli amuulize yule mchungaji wa South Korea aliyewadanganya waumini wake wenye maambukizi waendelee kuja kanisani eti Yesu atawaponya. Matokeo yake wakawa cluster ya Corona Virus. Mungu ametupa maarifa tuyatumie. Huwezi mfuata Simba aliye na njaa ukitegemea Yesu atakuokoa. Huko ni kumjaribu Mungu.
 
Kusema kweli Magufuli ana sentensi na kauli tata mno!

Hata kumtetea haiwezekani kabisa!

Yeye anasema ni msema kweli!

Mtu kuwa muwazi na mkweli juu ya unayoyafikiri ni sawa pia!

Ndio uhuru wa kutoa mawazo huo! Japo mawazo TATA.
 
Hiyo korona imekula vichwa vingapi mpaka sasa hapa kwetu wakuu!
Wengine tuko Mchambawima - Wesha - Pemba huku!
 
Hiyo korona imekula vichwa vingapi mpaka sasa hapa kwetu wakuu!
Wengine tuko Mchambawima - Wesha - Pemba huku!

Unadhani kote unakoua kwa kasi unayoisikia ilikuwa hivyo hivyo tangia mwezi wa kwanza tangu ugonjwa kuingia?

1. Congo walioanza na mgonjwa 1, wakawa 3, 9, 18 sasa 33. Vifo 1 sasa 2.

2. Kenya nako hivyo hivyo ilianza 1 sasa wako kwenye 18 wamesha pita humo kwenye 3, 9 pia.

Haka ka kujipa moyo, Mungu atunusuru kaendelee.
 
Moja kwa moja kwenye mada. Waswahili wanasema asiyejua maana haambiwi maana.

Kwamba haka kaugonjwa ni ka upepo tu katapita. Na kwa kuwa sisi tu wacha Mungu sana sijui kuliko nani, basi sisi tumemwachia yeye.

Vipi mambo yakienda ndivyo sivyo (katu hatuombei hivyo), je tutasema Mungu katususa?

Why This Controversial Kenyan-American Professor is very Unhappy With President Magufuli

Kwa kuwa fair tu tunapaswa sana kujitathmini.

Kama tunadhani tuko sawa basi tuna matatizo (incurable) ambayo labda ni makubwa zaidi kuliko hata Corona yenyewe.

Kama ni hivi tunaelekea kwenye kutakana kuachia ngazi.

It can't be like this.
Tuna viongozi wabovu sana Africa.
 
Back
Top Bottom