Kwenu marais wetu Wastaafu, Mwinyi, Mkapa na rais Kikwete.
Kwa heshima na taadhima inafikirisha kuwaandikia waraka huu baada ya kuwa kwa dhati kabisa, njia nyingi zimejaribiwa kushauri, kuhimiza, kuomba, kuisihi nk ili kuwepo mtizamo tofauti kuhusiana na ugonjwa huu.
Nchi hii ni yetu sote kiasi kuwa kwa yeyote yule, awe mkubwa au mdogo kunyamaza kimya tu wakati ni wazi kuwa labda tunakoelekea sasa siko, siyo jambo ambalo tunaweza kulichagua kama moja ya uwezekano tena.
Waheshimiwa katika nyakati tofauti mmewahi kupokea hatamu za serikali na kuiongoza nchi hii pendwa kama watakavyo kuja na kutoka wengine kwa njia za amani. Siyo siri kuwa kama marais wastaafu nafasi yenu ya kulitumikia taifa hili ingalipo. Ni wazi kuwa, katu marehemu baba wa taifa (rip) asingelikubali kuliacha taifa hili ambalo limekuwa la kupigiwa mfano siku zote kuangamia.
Waheshimiwa, msiliache taifa hili kuangamia na ugonjwa huu huku mkiangalia tu. Mnayo nafasi ya kuliunganisha taifa hili kuwa moja ili kwa pamoja tukaishinda Corona kwa salama.
Shime waheshimiwa msilinyime taifa hili hekima wala busara zenu, ambazo kwa hakika zinahitajika sana kwa sasa labda kuliko kipindi kingine chochote kilichowahi kupita.
Kwa umoja wenu kama wananchi wa nchi hii au katika nafasi zenu ka mtanzania mmoja mmoja mnayo nafasi ya kushauriana na mheshimiwa rais kwa niaba yetu sisi wananchi.
Umoja wetu utokanao na kushawishiana kwa nguvu za hoja si hoja za nguvu utatuvusha katika vita hivi.
Kama watanzania tunastahili kuushinda ugonjwa huu kama jambo la dharura kweli kweli vinginevyo kama ilivyo wazi, maisha ya wengi wetu yako hatarini mno.
Mungu ibariki Tanzania. Mungu tujalie salama tunavyomuunga kupambana na ugonjwa huu.
Nawasilisha.