Mabibi na mabwana moja kwa moja kwenye mada ili kumfunga paka huyu kengele.
Tunayoyashudia sasa hivi mipakani ni wazi kuwa yataendelea kwa muda mrefu tu na bila ya kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Ni wazi kuwa Tanzania kwa kukataa kuwemo katika protokali za pamoja kuhusiana na ugonjwa huu katika EAC au katika zile za dunia kupitia WHO, hakuna namna yoyote ambayo sisi tunaweza kuwa na mashirikiano au maingiliano na wengine pasipokuwa na migongano.
Tanzania imekuwa ikipotosha kauli na misimamo inayotolewa WHO ambayo kwa hakika imekuwa ikizingatiwa na mataifa takribani yote duniani. Mfano:
1. WHO inatambua ugonjwa huu kuwa ni janga la kimataifa. Kuwa ugonjwa huu ni hatari, unauwa, hauna dawa wala chanjo ya kujikinga nao.
Tanzania badala yake inatambua kuwa huu ugonjwa ni kaupepo tu ambako katapita. Tanzania pia inauona huu ugonjwa kuwa ni vita vya kiuchumi vya mabeberu dhidi yake. Tanzania inatambua kuwa tiba ya ugonjwa huu ipo. Ya kwamba nyungu ya kujifukiza, mitishamba na maombezi vinatambulika rasmi kama suluhu yake kamili.
2. WHO inatambua kuwa ugonjwa huu ungalipo na kuwa kama hatua stahiki za kuudhibiti hakuna, basi utaendelea kusambaa na hali kuwa hata mbaya zaidi.
Hata hivyo WHO inatambua ugonjwa huu utakuwapo kwa muda mrefu na kama jitihada sahihi za kuudhibiti zikiwapo, basi tunaweza kuendelea na maisha hata kama ugonjwa ungalipo hadi pale tiba au chanjo vitakapogunduliwa.
Tanzania kwa upande wake inaamini kuwa ugonjwa huu umeshakwisha hali hakuna hatua zozote zilizochukuliwa au zinazochukuliwa kuumaliza au kuuzuia kuendelea kusambaa. Msisitizo umekuwa zaidi kwenye kulinda uchumi, yaani kwenye kuwataka watu wake kuchapa kazi tu. Ya kuwa corona ni kaugonjwa kadogo tu kanakopita.
Katika EAC wanayatambua yote haya mawili tokea WHO vilivyo, isipokuwa kwa Tanzania tu.
Nchi nyingine zote katika EAC zinatambua umuhimu wa kuwaweka wananchi wao salama dhidi ya ugonjwa huu hata kama ni kwa kuuweka uchumi wa nchi zao hatarini.
Nchi nyingine zote katika EAC haziko tayari kusubiria wananchi wao kufa kwa Corona, bali wako tayari kufa wakati wakipambana nayo.
Nchi nyingine zote katika EAC ziko tayari kuishi na Corona iliyodhibitiwa. Katika hili, nchi hizo haziko tayari kuruhusu mgeni yeyote kuingia katika nchi zao bila ya wao kujiridhisha kwanza kuhusiana hali yake ya Corona ikoje.
Ukiangalia mfululizo wa protocols hizi ni wazi kuwa hapa pana "mwana mkaidi ambaye huyo yeye kufaidi ni mpaka siku ya Iddi!"
Tanzania tunapaswa tujitathmini. Hayupo mchawi bali ni sisi wenyewe. Tumekuwa kama watoto watukutu.
Wala tusimsubiri mno wa kuja kutufunga paka sisi kengele! Mbona sasa tunapitiliza mno?
Choko choko zote hizi huko mipakani, ni wazi kuwa washari ni sisi.
Kama sisi tumeamua kuishi na Corona tukiichukulia poa tusilazimishe hilo na kwa wengine pia.
Kama hatukubali raia wetu waendao kwa wenzetu kupata ruhusa za kuingia kwa kufuata masharti yaliyoko huko, basi na tuifunge tu hii mipaka. Vinginevyo migogoro hii isiyokuwa na tija itaendelea huku mkiwahimiza waathirika wa mitafaruku hii kuwalipa nyie kodi na vitisho vya mafaini juu.
Kwani hamzioni biashara za watu zinavyodorora huko mipakani? Kwani mnadhani wafanyabiashara hao watatoa wapi pesa za kuwalipa nyie kodi tena kwa wakati na kwa shuruti zenu?