Ugomvi katika mahusiano ni afya

Ugomvi katika mahusiano ni afya

Himidini

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Posts
5,534
Reaction score
4,193
Ukimuuliza binti yeyote akutajie mambo 10 asiyopenda kusikia au kuyaona katika ndoa yake, mojawapo litakuwa ni ugomvi. Ugomvi unaumiza, kiakili na kimwili. Ugomvi si ustaarabu, zaidi sana ugomvi si haki !! Kuna ugomvi wa hoja, kuna ugomvi wa ngumi mbili tatu mambo yawe sawa, kuna ugomvi wa ukimya! Vyovyote uwavyo, ugomvi si neno jema, halina ladha kwa wapendanao!!!
....
Kama ulikuwa ukifikiria kuwa ugomvi katika mahusiano ni jambo baya basi umekosea sana! Kama ukikutana na wanandoa wakakuambia hawakuwahi kugombana au kutofautiana katika ndoa yao, ama wanakutania tu au wape pole! Ugomvi katika mahusiano una maana zifuatazo;
....
UGOMVI UNA MAANA MNAPENDANA
Wanasaikolojia Bruce na John katika kitabu chao cha Language of love, wanasema, kama wawili wanapendana kweli, lazima wagombane! Wanagombana kwa sababu kila mmoja anatetea sehemu ya pili isiende pengine, anailinda, anaionea wivu. Hivyo kugombana na pengine kugombezwa ni ushahidi kuwa ndani yenu mnahitajiana na mnapendana kwa hiari.
....
UGOMVI HUTIBU MATATIZO YA HISIA (HEALTHIER EMOTIONS)
Wanandoa/Wachumba wasiotofautiana na kugombana mara kadhaa basi ni wazi hisia za kimapenzi baina yao zinaumwa! Hapo kuna misongo ya mawazo, kuna kulimbikiza maudhi sio upole huo, kuna hasira inayosubiri kulipuka.. Upendo wenye afya huonekana kwa hisia za wazi.
....
KUGOMBANA NI KUONESHA KUJALI (CARE)
Hapa ntatofautiana wengi wanaofikiri kuwa kumjali mwenza ni kumtoa out, kumpa maua, kumnyoshea shati, kumpa zawadi, surprise n.k Kugombana ni zawadi ambayo wanandoa vijana wengi hawaijui uzuri wake. Kuwa na mahusiano yaliyopoa kabisa kuna gharama zake, wengi hushituka mambo yalishaharibika. Mwanasaikolojia George R. Bach na Peter Wyden katika kitabu chao cha 'How to fight fair in love' wanasema '...we have discovered that couples who fight together are couples who stay together- provided they know how to fight properly..."
....
Ugomvi wa wachumba huhusu zaidi mavazi, simu, mwonekano, hitaji la watoto,namna ya kutumia starehe n.k
Ugomvi wa wanandoa wengi huhusu zaidi pesa, watoto, wakwe, ndugu, majukumu, tendo la ndoa n.k
Ugomvi wa wanandoa wazee huhusu wajukuu, watoto wao wakubwa, ibaada n.k
....
TAHADHARI
Sijaruhusu kupigana makonde, unaweza kupigana na mwenza kwa kutumia akili nyingi pasipo kutumia nguvu nyingi. Ugomvi mzuri ni ule unaoleta suluhu mapema na usipigane kuwapa wengine faida.
Be brave!
 
uko sawa kabisa na ndio maana hata wahenga walisema wagombanao ndio wapatanao asante kwa somo murua mkuu Himidini.
 
Last edited by a moderator:
kweli kabisa aisee mimi na wife tunagombana mara kibao kwa maneno, minuno na ngumi lakini baadae huisha na tunaendelea kama kawaida
 
dah...siku ya tatu sasa wife kaninunia...na me nimeuchuna tu...cjui ka no afya...
 
Naunga mkono hoja. Kwa sababu mimi ni siku ya tatu sijaongea na wife lakini matumaini yangu baada ya week tutakuwa pamoja kujenga taifa. Thanks for inspirational.
 
Dah! jukwaa lingekuwa hivi tungepata elimu sana juu ya haya mahusiano,lakini nina swali kwa mtoa maada au kwa yeyote aliyeisoma maada husika Ugomvi wa kila siku nao huimarisha au hubomoa maana kuna wengine maugomvi hayaishi leo simu kesho hiki yaani unakuta hata majirani mnahusishwa kwa namna moja ama nyingine maana inakuwa kama kero vipi kwa wahusika huwa inaimarisha hii?
 
Ugonvyi si kitu cha kuendekeza maana wengine huwaachia makovu moyoni just imagine ugonvyi unatokea halafu mme anamtamkia "mwanamke yaani wewe mwanamke wa hovyo kwanza ulijipendekeza kwangu ndo nikakuoa wala sikuku penda".
Hata wakisamehana hayo maneno atayakumbuka hata baada ya siku nyingi.
 
Back
Top Bottom