Mwanamaji
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 2,896
- 4,495
Habari zenu wajumbe....
Kwa muda mrefu kidogo nimekua nikijiuliza hili swali.
Ni kwanini kuna mkanganyiko katika ugawaji wa masafa ya vituo vya redio ?
Nitaeleza kwa mifano ili hoja yangu ieleweke vema kwa namna hali ilivyo sasa hivi.
Kituo chetu cha redio (cha mfano) tutakiita ''Tikiti maji FM''.
Kwa namna hali ilivyo sasa, utaipata Tikiti FM kwa masafa yafuatayo katika mikoa tofauti tofauti....
Mbeya 89.9 MHz
Tanga 102.3 MHz
Iringa 85.7 MHz
Dar Es Salaam 97.5 MHz
Kigoma 101.4 MHz
Mtwara 92.1 MHz
N.k
Tatizo liko hapa:
Hii inatupa mkanganyiko sisi wapenzi wa redio hii (Tikiti Maji FM) pale tunaposafiri kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine. Itatulazimu kuanza kuhangaika kujua redio yetu pendwa (Tikiti maji FM) inapatikana kwenye frequency zipi katika mkoa huu ''mpya'' tulioutembelea, ili tuweze kuisikia.
Mawazo yangu:
Ninadhani ingekua ni vema zaidi haya masafa yagawanywe ''kitaifa'' ukizingatia kwamba mamlaka inayogawa masafa haya ni moja yaani (TCRA), hivyo hakutakua na mkanganyiko.
Hali iwe kama hivi:
88.1 MHz ni Tikiti Maji FM
89.8 MHz ni Mapapai FM
92.3 MHz ni Nanasi FM
95.6 MHz ni Nazi Mbovu FM
98.5 MHz ni Embe Dodo FM
102.7 MHz ni Nyanya Mbichi FM
107.2 MHz ni Pilipili Kichaa FM
N.k
Masafa tajwa hapo juu yawe ni kwa nchi nzima na si kimikoa.
Manufaa:
Hii itasaidia yafuatayo:
1. Kuondoa mkanganyiko na usumbufu usio wa lazima kwa walaji (wasikilizaji).
2. Itasidia kwenye ''branding'' ya vituo vya redio. Mtangazaji akisema ''unasikiliza 88.1'', msikilizaji anaelewa moja kwa moja kwamba kituo kinachozungumziwa hapa ni Tikiti Maji FM.
(Itakua tofauti na sasa, ambapo ni lazima mtangazaji huyo ni afafanue anaizungumzia 88.1 ''ya mkoa upi'')
Kwa kifupi ni kwamba masafa fulani yanakua ni ''brand and identity'' ya kituo cha fulani cha redio nchi nzima.
Majibu ya hoja ''zinazoweza'' kujitokeza kufuatia pendekezo hili:
1. Itakuwaje kwa redio ambazo hazisikiki nchi nzima ?
Jibu: Katika eneo ambalo redio husika haisikiki, frequency ''yake'' inabaki ''wazi'' (Hakuna mwingine atakayeitumia hadi pale ''mwenyewe'' atakapoanza kurusha matangazo kwenye eneo hilo).
2. Je hii haitapunguza mapato ya serikali kupitia tozo za kuomba masafa ?
Jibu: Hapana, mapato yatapatikana kwenye kuomba hayo masafa ya ''kitaifa'' pamoja na ''vibali'' vya kurusha matangazo kwenye mikoa tofauti tofauti.
3. Tuna vituo vya redio vingi sana nchini, je, tukitaka kila redio ihodhi masafa ''kitaifa'', tunayo ''akiba'' ya masafa ya kumgawia kila mmoja (kila redio) ?
Jibu: Tunaweza kutanua ''uwanda'' wa masafa kutoka (87 hadi 108) yaliyopo sasa (endapo hayatatosha) na kuongezea zaidi (kwa kadri teknolojia itakavyoturuhusu).
Naombeni kuwasilisha.
NB: Mimi si mtaalam wa mambo ya ''telecommunications'' hivyo kunaweza kukawa na mapungufu ya kiufundi katika wasilisho langu hapo juu (hasa jibu la swali la 3), hivyo naomba tuutumie uzi huu kuelimishana kama kuna waliobobea katika masuala haya.
Karibuni.