Uganda wanatumia dawa gani kutibu corona?

the muter

JF-Expert Member
Oct 31, 2012
1,314
1,746
Kwa nchi zote za Africa, Uganda ndio wapo vizuri sana katika kutibu corona. Je, wanatumia dawa gani? Kwanini tusicopy na kupaste kwetu?
Screenshot_20200423-103053.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni mwendo wa kujifukiza tu virusi kwisha

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kwa nchi zote za Africa, Uganda ndio wapo vizuri sana katika kutibu corona. Je, wanatumia dawa gani? Kwanini tusicopy na kupaste kwetu?View attachment 1427650

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio kitu Rais alichokua anasema jana. Hata hapa Tanzania kuna watu wanapona lakini takwimu hizo hazitolewi bali zinatolewa zile za maambukizi mapya na za vifo na kupelekea kutisha watu

Mimi najiuliza kina Mwana FA, Isabela na wengine kibao mbona hatuambiwi kuwa walipona? Naamini Rais anataarifa za kweli na za uhakika zaidi kutokana na kua na vyanzo tofauti vinavyompatia taarifa zingine zikiwa na za ki intelijensia. Vyanzo vyake vinasema watu zaidi ya 100 walishapona ugonjwa huo
 
Mh, mbona HIV wanapukutika/walipukutika mpaka leo?

You cant be a master of everything in this world. Wao wameamua kutumia dawa za kienyeji zile walizozoea. Nyinyi mnaosema let science lead, indeed, it leads you nowhere.
Science ni kitu endelevu. Hakina majawabu ya moja kwa moja kwenye kila kitu. Ndio maana US na Ulaya wanachabangwa kama hawana akili nzuri pamoja na science yao
 
Umesoma virology?
 
Ndio kitu Rais alichokua anasema jana. Hata hapa Tanzania kuna watu wanapona lakini takwimu hizo hazitolewi bali zinatolewa zile za maambukizi mapya na za vifo na kupelekea kutisha watu

Mimi najiuliza kina Mwana FA, Isabela na wengine kibao mbona hatuambiwi kuwa walipona? Naamini Rais anataarifa za kweli na za uhakika zaidi kutokana na kua na vyanzo tofauti vinavyompatia taarifa zingine zikiwa na za ki intelijensia. Vyanzo vyake vinasema watu zaidi ya 100 walishapona ugonjwa huo
Mbona wanaopona wanatangazwa ndugu!!
Ile idadi iliyotolewa mara ya mwisho kwa waliopona ndio sahihi
Hawawezi kujitungia ili waonekane wamfurahishe meco
Kama anaona wanafanya kazi ya kuwatisha raia, awafute kazi ateue tim mpya
 
Kwa nchi zote za Africa, Uganda ndio wapo vizuri sana katika kutibu corona. Je, wanatumia dawa gani? Kwanini tusicopy na kupaste kwetu?View attachment 1427650

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna dawa ya kutibu virusi vya Covid 19 popote ulimwenguni. Mtu yeyote atakayeambukizwa ama atapata dalili mfano mafua, homa na shida kupumua, wanachotibu mahospitalini ni hizo dalili, homa na mafua inashushwa kwa panadol au aspirin, kupumua ndiyo wanaweka mashine kusaidia kupona ni vita ya mwili wako na hao virusi kwa msaada wa hivyo wanavyokupa hospitali.
 
Wa
Mbona wanaopona wanatangazwa ndugu!!
Ile idadi iliyotolewa mara ya mwisho kwa waliopona ndio sahihi
Hawawezi kujitungia ili waonekane wamfurahishe meco
Kama anaona wanafanya kazi ya kuwatisha raia, awafute kazi ateue tim mpya
Waliopona wanatangazwa kwa idadi sahihi? Kwanini kuwe na taarifa zinazotofautiana? Kwa namna yeyote naamini taarifa ya Mkuu wa Nchi ndiyo sahihi
 
Back
Top Bottom