Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,557
- 21,512
Uganda: wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nkumba kilichopo mjini Entebbe, wamegoma kuingia madarasani, baada ya kutokuwepo kuku kwa siku tatu mfululizo.
Mgomo huo ulioanza leo, umeridhiwa na idadi kubwa ya wanafunzi. Mbali na kudai kutowepo kwa kitoweo cha nyama ya kuku, wanafunzi hao wanalalamikia upungufu wa uma za chakula, maziwa, ubovu wa chakula na kudai maji ya kunywa ya chupa yenye ubora. Ili kushinikiza zaidi kutekelezwa kwa madai hayo, uongozi wa wanafunzi hao uliandamana kuelekea ofisi ya makamu mkuu wa chuo ambako walifanya kikao.
Katika kikao hicho, wanafunzi hao walidai uongozi umepokea malalamiko Yao na kwamba yatafanyiwa kazi haraka. Hatua hii ya wanafunzi hao imeonekana kuwa tofauti kidogo na madai yaliyozoeleka kwa wanafunzi wa vyuo ambao mara nyingi hudai ubora wa masomo, upungufu wa wahadhiri, lakini sasa hawa wa Nkumba, wao wanalilia kuku kuwemo kwenye mlolongo wa vyakula vyao kila siku.