Ugali wa jana

Ugali wa jana

Ndugu wazalendo wenzangu, amani iwe kwetu sote na kwa familia zetu.

Mara nyingi sisi 🇹🇿 Watanzania hula ugali. Wasukuma hula ugali asubuhi, mchana, usiku na wakati mwingine usiku wa manane huamka na kuusonga Tena ule ulio mgumuuuu.

Ugali hupikwa kwa nafaka mbalimbali, mahindi, ulezi, uwele, mtama, muhogo na kule Mbeya Wanyakyusa hupika ugali wa ndizi.

Jamani mwenzenu naumia Sana nikitupa chakula, hasa nikitilia maananani Kuna mamilioni ya watu wanalala bila kula.

Naumia nikiwapa mifugo chakula kilichobaki, ndio maana chakula Cha mifugo siwezi kukila, iweje wao wale chakula changu?

Nawauliza wana JamiiForums nifanye Nini na ugali uliobaki jana usiku? Sitaki kuutupa walakuipa mifugo.

Naomba ujuzi na uzoefu wako
0769099203
Ulishe kwenye namba hii,plzzzz
 
Zamani marehemu Bibi alikuwa anauchoma ugali uliobaki kwenye Moto asubuhi Kisha anatukatia mapande mapande na tunamezea na maziwa fresh ya Moto ya mbuzi............. Ulikuwa mtamu sana....

Siku hizi ukienda majumbani mwa watu unashangaa sima nzima ipo jalalani.....vitoto vinakula tambi na chai au maandazi au vitumbua........... Mwili watatoa wapi.... Ukiniangalia Mimi sipigi chuma ila Nina uwezo wa kuzuia watu wanne wenye kilo hamsini hamsini.........

Kula sima isiyokobolewa kwa afya
 
Back
Top Bottom