Ugali wa jana

Ugali wa jana

Kuna familia niliwahi kwenda binti wa kazi anaambiwa mpakulie mgeni, binti akasema chakula kimeisha umebaki ugali wa kaka(shamba boy). Hadi leo sijaielewa ile kauli kwa kweli.

Mkuu ugali uliolala hua tuna uweka kwenye mfuko wa plastiki then tunaweka kwenye sufulia lenye maji tunachemsha fresh kabisa
 
Haya ngoja nikufundishe hau-uli wenyewe, ila una urudia kuupika unakata vipande vidogo×2 halafu unaweka kwenye sufuria mpaka uchemke baada ya hapo unakoroga uji unachanganya unasubiri uchemke then unaweka unga unasonga tayari ugali

*Hakikisha unakata vipande vidogo sana ili yasitokee yale mabuja
Dah! Umenikumbusha mbali. Hii mbinu hawa kina "Junior" hawawezi kuijua.
 
  • Thanks
Reactions: ABJ
Wasukuma hula ugali asubuhi, mchana, usiku na wakati mwingine usiku wa manane huamka na kuusonga Tena ule ulio mgumuuuu.
 
Ndugu wazalendo wenzangu, amani iwe kwetu sote na kwa familia zetu.

Mara nyingi sisi 🇹🇿 Watanzania hula ugali. Wasukuma hula ugali asubuhi, mchana, usiku na wakati mwingine usiku wa manane huamka na kuusonga Tena ule ulio mgumuuuu.

Ugali hupikwa kwa nafaka mbalimbali, mahindi, ulezi, uwele, mtama, muhogo na kule Mbeya Wanyakyusa hupika ugali wa ndizi.

Jamani mwenzenu naumia Sana nikitupa chakula, hasa nikitilia maananani Kuna mamilioni ya watu wanalala bila kula.

Naumia nikiwapa mifugo chakula kilichobaki, ndio maana chakula Cha mifugo siwezi kukila, iweje wao wale chakula changu?

Nawauliza wana JamiiForums nifanye Nini na ugali uliobaki jana usiku? Sitaki kuutupa walakuipa mifugo.

Naomba ujuzi na uzoefu wako
Mkuu Bujibuji ngoja nikupe njia ninayotumia mie kutotupa ugali. Hakikisha ugali unaobaki unauhifadhi kwenye friji ukiwa bonge Moja (unaweza kuuviriga kwa shepu unayotaka).
Asubuhi chukua Ugali ukate slesi jinsi unavyopenda, hizo slesi zinyunyizie chumvi na pilipili manga Kwa mbali. Andaa kikaango na mafuta (samli nzuri zaidi). Weka kwenye moto vikaange had viwe na rangi ya njano brown. Ipua weka mezani kula na familia. Lete mrejesho.
 
Nimeipenda hiii mbinu
 
Back
Top Bottom