Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,174
Ufuska, ulevi vyamkera Babu akemea Send to a friend Saturday, 28 May 2011 10:30
Mussa Juma, Samunge
MCHUNGAJI Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapila amekemea maovu anayodai kuwa yameibuka katika kijiji cha Samunge kutokana na ongezeko la watu walioweka makazi ya muda.
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum jana, Mwasapila alisema katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko la matendo ya ngono na ulevi, mambo ambayo yanaelekea kupunguza heshima ya tiba yake.
Tangu aanze kutoa tiba ya magonjwa sugu mwanzoni mwa mwaka huu, Mwasapila amekuwa akikemea maovu hayo ambayo ni pamoja na ngono, ulevi na wizi ili kulinda heshima ya tiba yake.
Lakini, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa vitendo vya ufuska vimekuwa vikifanywa katika mahema ambayo yanakodishwa kwa watu mbalimbali kwa gharama ya kati ya Sh5,000 hadi Sh20,000.
Huduma hiyo ya mahema inapatikana katika maeneo ambayo kuna migahawa na baa na hivyo baadhi ya wateja wakiwamo wagonjwa wamekuwa wakilala kwa kukodi kwa muda watakaohitaji kustarehe.
Uchunguzi katika baadhi ya mahema hayo umeonyesha kuwa huduma hiyo ya kupangisha imekuwa ikitolewa hadi nyakati za mchana kwa wenyeji, wakiwemo wafanyabiashara wengi wa vyakula na vinywaji, jambo ambalo limekuwa likiwasukuma pia kuyatumia kwa ufuska.
Baadhi ya wakazi wa Samunge, Joram Bugirwa na Peter Paulo waliieleza Mwananchi kuwa wageni wanaofika kijijini kwao ndio ambao wanaendesha vitendo hivyo na kuomba uiongozi wa serikali na Mchungaji Mwasapila kuwakemea.
"Kijiji chetu sasa kimeharibika sana, uhuni tu watoto wa kike wanaharibika kwani hawakuwahi kuona watu wengi hivi hapa na wanashawishika kufanya vitendo vibaya,"alieleza Peter.
Kwa upande wake, kaimu mwenyekiti wa kijiji hicho, Jonas Ngiroboi alikiri jana kupokea taarifa za kuwepo vitendo vya ufuska na kueleza kuwa tayari serikali ya kijiji inao mpango wa kuwaorodhesha wafanyabuiashara wote waliopo Samunge ili kujua kazi zao.
"Wapo wengi inawezekana wengine wamekuja kwa mambo yao tumeanza kufuatilia jambo hili kwani awali hata kodi walikuwa hawalipi sasa tunaweza utaratibu walipe kwa kijiji kutokana na kufanyabiashara hapa,"alisema Ngiroboi.
Mapema jana, Mchungaji Mwasapila aliamua kutolea kauli suala hilo akisema ameshangazwa na tabia ya baadhi ya watu kuanza kufanya ufuska wa kutisha na kuitia doa tiba yake.
"Asubuhi mipira ya kiume (kondomu) inaokotwa barabarani, muziki unapigwa hadi asubuhi na matendo mengine mabaya yanaonekana sasa.....hivi karibuni
Nitalisemea suala hili baada ya kukutana na watu wanaofanya biashara hapa,"alisema.
Katika siku za hivi karibuni baadhi ya watu wanaofika Samunge kwa ajili iya tiba wamewalalamikia baadhi ya wasaidizi wa mchungaji huyo kwa madai kuwa wamekuwa wakiendekeza ulevi.
Tiba ya mchungaji huyo imekigeuza kijiji hicho kuwa eneo la utalii hasa baada ya mamia ya wanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali nchini kuweka makazi ya muda kwa kujenga mahema, kuuza vyakua, vinywaji na maduka ya bidhaa mbalimbali.
Vifo vyafikia 101
Katika hatua nyingine, idadi ya watu waliofariki dunia katika kijiji hicho kuanzia Machi 13 hadi Mei 25 mwaka huu imefikia 101
Idadi hiyo imeongezeka juzi baada ya watu wengine watatu akiwemo raia wa Kenya kufariki.
Mganga mfawidhi wa zahanati ya Kata ya Samunge, Elias Lubida aliliambia gazeti hili kuwa wagonjwa hao wamekuwa wakifariki dunia kutokana na kufika mahali hapo wakiwa katika hali mbaya kiafya.
Aliwataja wagonjwa waliofariki wiki hii kuwa ni Ledama Maridani (70), mkazi wa Narok, Kenya, Lucia Mmasi (27) kutoka Hai mkoani Kilimanjaro na Nolekatu Mollel (3), mkazi wa Pinyinyi wilayani Ngorongoro.
"Tunaendelea kutoa wito watu wasilete huku wagonjwa mahututi ambao wanawatoa hospitali kwani miundombinu siyo mizuri na pia ni kuwatesa wagonjwa, ''alisema Lubida.
Mwenyekiti adaiwa kutoweka na vitendea kazi
Wakati huohuo, halmashauri ya kijiji cha Samunge imetoa siku tatu kwa mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho aliyeondolewa madarakani, Michael Lengume kukabidhi vitendea kazi.
Maamuzi hayo yalifikiwa juzi katika kikao kilichofanyika jioni chini ya kaimu mwenyekiti wa kijiji hicho, Jonas Ngiroboi na afisa mtendaji wa kata Michael Kimario.
Ngiroboi ambaye pia ni mwenyekiti wa kitongoji cha Samunge aliliambia gazeti hili kuwa wamempa siku tatu mwenyekiti huyo kukabidhi mali zaserikali na ofisi wakati suala lake linashughulikiwa na halmashauri ya wilaya hiyo.
''Tumepokea taarifa ya mapato na matumizi bado tunaifanyia kazi kwani kuna malipo ya watu ambayo yana utata, lakini tumeona kwanza tukabidhiwe ofisi ndipo kazi iendelee,''alisema Ngiroboi.
Hata hivyo, Lengume amekuwa akipinga kuondolewa kwake katika nafasi hiyo kwa maelezo kuwa taratibu hazikufuatwa ikiwepo kupewa muda wa kujibu tuhuma na kufafanya tuhuma nyingi hazina ukweli.
Foleni yapungua Samunge
Misafara ya magari jana imeendelea kupungua licha ya uwepo wa magari zaidi ya 150 yaliyopewa huduma jana yakiwepo mengi ya raia wa kigeni toka nchini Kenya, Uganda na Burundi.
Ataka urasimu wa vibali ukome
Katika hatua nyingine Mchungaji Mwasapila ametaka mamlaka zinazohusika na utoaji wa vibali kwa magari yanayopeleka wagonjwa Samunge kuacha urasimu ili kuwaondolea wagonjwa hao usumbufu usiokuwa wa lazima.Mchungaji huyo aliliambia gazeti hili kuwa amepata malalamiko mengi kutoka kwa wagonjwa kwamba utaratibu mzima wa upatikanaji wa vibali umetawaliwa na rushwa.
"Wawaachie watu waje kupata tiba kwa sasa hakuna haja ya kusumbua watu kwani tuna utaratibu mzuri wa kutoa dawa ambao unasababisha foleni kumalizika mapema," alisema Mwasapila.
Mchungaji huyo pia alieleza kuridhishwa na maafisa wa serikali wanaomsaidia kutoa huduma hapa Samunge kutokana na kupungua kwa kiasi kikubwa kwa foleni.