Ufunguzi wa Kituo cha TEHAMA - Zanzibar

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
737
476
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema ukamilikaji wa ujenzi wa minara 42 ya mawasiliano na vituo 11 vya Teknolojia, Habari, Mawasiliano (TEHAMA) imefungua ukarasa mpya wa mawasiliano Zanzibar.

Ameyasema hayo leo mara baada ya kufungua kituo Cha TEHAMA kilichojengwa kupitia mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) kilichopo Bwefum Mkoa wa Mjini Magharibi.

Pia, Rais Dk. Mwinyi amezindua mnara wa mawasiliano uliojengwa Kisakasaka wilaya ya Magharibi 'B'.

Rais Dk.Mwinyi amesema kukamilika kwa vituo hivyo vitasaidia kuchochea ukuaji wa matumizi ya TEHAMA ambayo wananchi wengi watatumia kwenye shughuli za kila siku.

Amesema kukamilika kwa ujenzi wa minara hiyo 42 itaondoa malalamiko ya wananchi katika ukosefu wa huduma ya mawasiliano pamoja na kuwepo kwa hali ya usalama na mali za wananchi pamoja na wageni wanaoingia Zanzibar.

26 Oktoba 2022

Zanzibar.
IMG-20221026-WA0087.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom