Ufugaji wa Kuku wa kisasa (Layers)

Mkuu muhinda...
Niendelee kukupa pongezi kwa hatua uliyochukua.

Kuhusu chanjo ya mareks, kidogo umenishtua. Ninachofahamu ni kwamba hii chanjo hutolewa kwa day old cheek (kifaranga cha siku 1), mara nyingi hutolewa na kampuni, hii ya kuwapa chanjo wakiwa wakubwa sijawahi kuisikia, labda unipe darasa kidogo.
Nami nina layers 400, wana mwezi wa 2 sasa, lakini hii stage niliiruka...
Marek vaccine ni only once tena ni siku ya kwanza wanapotolewa katika Hatchery....

Na ikitokea umechelewa kuwapa hiyo chanjo in day one then waweza wapa hata wakina na siku tatu but isizidi hapo chief....
 
Wakuu Vifaranga vya layers nitapata wapi wadau, nahitaji hii awamu wamezuia toka Kenya shida tupu
 
mkuu
muhinda. vipi mbona haukumalizia updates hadi wiki ya 96 kama ulivyoahidi. ingependeza sana kama ungemalizia.
 
UZI HUU UTAKUWA UPDATED KWA KILA HATUA NITAKAYOPITIA KAMA MFUGAJI. KARIBUNI


UPDATE 20TH FEB 2015

Habari za masiku wadau na heri ya mwaka mpya.
Napenda kuwaletea mrejesho kama nilivyoahidi.

Kwakweli changamoto nimekumbana nazo nyingi sana. Kama sio roho ngumu ningeacha kufuga.

Kuku wangu wana week 40 sasa na walianza kutaga at 18 weeks exactly.

Changamoto ya 1 ni magonjwa. Kuku wangu wameugua sana typhoid na mafua. So far wameshakufa over 100 layers.
Kitu nilichokosea ni kutowachanja typhoid na mafua. Sababu nilishauriwa kuwa typhoid is not common na kama wakipata inatibika. Kumbe wapi typhoid inatibika lakini inatabia ya kujirudia.

2. Joto pia liliua sana kuku. Kutokana kwamba niliwaweka juu sana karibu na bati. Sasa ivi nimewashusha na mambo yanaenda vizuri.

3. Soko la mayai lilisumbua sana. Wakati kuku walianza kutaga mwezi wa 10 bei ya mayai ilishuka sana na hata kuuza ilikuwa shida. Hapa watu waliuza sana kuku. Kwakweli nilipambana kufa na kupona nikafaulu kupata walau chakula cha kuku. At this point walikuwa wanakula 80, 000 per day. Iyo ni chakula tu. Mwezi wa kwanza soko lika improve ndio kidogo kafaida nikakaona.

So far napata tray 22 -25 per day. Faida kwa mwezi napata angalau 1.5m. Na hapa kuku wamekufa sana.

Nilichojifunza ni kwamba next time ntachukua mbegu tofauti. Maana inaelekea hawa nilionao either parent stock yao ilikuwa na matyphoid au ni mbegu tu ndio dhaifu kwa magonjwa.
Always hakikisha kuku wako wanapata chanjo zote. Utaserve hela nyingi sana kwenye madawa.

Nakaribisha maswali
------------------------

Mimi ni mdau mpya katika fani ya ufugaji. Baada ya kufanya utafiti kwa mda mrefu kupitia hapa JF na kwa wafugaji wazoefu nimeamua kuanza na kuku wa mayai yaani layers.

Kwanza kabisa nilianza kujenga banda kwa kufuata maelekezo ya wataalamu. yaani layers wanahitaji ventilation ya kutosha. banda la layers linashauriwa kujengwa kwa kupandisha tofali 2 then chicken wire mpaka juu. inashauriwa squire metre 1 kwa layers 5.

Sasa basi mi nimeanza na layers 1000. ivi ninavyoandika wamefikisha siku ya nne. kwakweli nashukuru Mungu so far wanaendelea vizuri na wamechangamka fresh tu.

Siku ya kwanza walipofika, niliwafikishia kwenye banda ambalo nililiandaa kwa kuweka chokaa kwenye sakafu, then maranda ambayo yamekauka vizuri na kuchujwa vumbi, juu ya maranda nilitandika magazeti. juu ya magazeti nilimwaga glucose ambayo walikuwa wakiidonoa wakati nawaandalia maji.

Pia niliweka majiko special ya mkaa kwa ajili ya kuwapatia joto la kutosha, kwa kiasi fulani na banda nimelizibaziba mpaka watakapofikisha week mbili ndio niwafungulie.

Pili nikawakorogea glucose gm 100 kwa lt 10 za maji ya uvuguvugu (hii unawapa bila chakula). maji ya uvuguvugu yanasaidia kulainisha utumbo wao kabla ya kuwapatia chakula kwa mara ya kwanza. baada ya masaa mawili niliwabadilishia maji na kuwawekea maji yenye vitamin na dawa kukausha vitovu, hapa niliwapa na chakula.

Dawa ya vitovu(Aliseril) watakunywa for 5 to7 days.

Hapo ndio nilipofikia tutaendelea kujulishana kadiri wanavyoendelea.

03/06/14 - Leo ni siku ya tano na vimeshakufa 3. Nimemconsult dr. Akaniambia ni tatizo la vitovu. Amenitoa hofu kwa kusema vifo kwa vifanga kwa idadi mpaka 10 kwa week ya kwanza ni vitu vya kawaida mradi isiwe rate ya kutisha. Despite all that vifaranga wanaendelea vizuri.

Jana tarehe 6/06/14 ambayo ilikuwa siku ya saba, nimewapa chanjo ya new castle ambayo procedure zake, niliwanyima maji for 2 hrs kabla ya kuwapa chanjo. lazima maji yachemshwe alafu yapoe. Then ktk lt 20 nilishauriwa kuweka vijiko 14 vya chakula vya maziwa ya unga baada ya nusu saa ndio unachanganya maji hayo na chanjo. Nikawapa kwa mda Wa masaa2.

Vifaranga vyangu vimetimiziza week 3 sasa. samahani siku update kwa mda kidogo, nilibanwa kidogo.
nilichojifunza kwenye chanjo ya kwanza kuku walidonoana sana. niliita mtaalamu akanieleza ni sababu ya stress ya kuwanyima maji for 2 hrs. alishauri next time niwanyime for 1 hr inatosha. nilifanya ivyo kwenye chanjo ya Gomboro na tatizo la kudonoana likatoweka. procedure za kuchanja Gomboro ni kama nilivyofanya kwenye New castle.

Siku ya 18 nilishauriwa niwachanje MAREX. huu ni ugonjwa unawapataga layers pale wanapoanza kutaga na ivyo kushindwa kutaga.. kwa kawaida wanatakiwa kupata hii chanjo na anayekuuzia. lakini kutokana na uaminifu mdogo wa baadhi ya makampuni inabidi kutake pre caution. hii wanachanjwa na Dr. kwa kuchomwa sindano ya shingoni.

Nimerudia chanjo ya new castle siku ya 21, procedure ni zilezile.. vifaranga vinakua vizuri. tuendelee kuelimishana.
Mradi unaendeleaje mkuu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom