Kuku wanauzwa

mr man city

JF-Expert Member
Apr 8, 2015
467
319
Nauza kuku aina ya SASSO. Wana wiki 11. Bado wiki 10 hadi 13 mitetea waanze kutaga.

-Jumla wapo 76. Wana uwiano sawa wa idadi..yani nusu kwa nusu na mitetea.

-majogoo unaweza kuyauza msimu wa sikukuu kwa kuwa tayari watakuwa na wiki 18 wanakuwa wakubwa kwaajili ya nyama na uache mitetea iendelee kutaga.
  • wana chanjo zote nne za awali(mareks,newcastle mara 2, gumboro mara 2, ndui)
  • niliwachukua wakiwa na umri wa siku moja kutoka Silverlands. Walikuwa 100 ila kutokana na uangalizi duni walifariki kutokana na baridi ile week ya kwanza.
-kwa sasa nawatoa hawa kwakuwa nina ramani nyingine na sitaweza kuwa na muda wa kuwahudumia, wanahitaji uangalizi angalau mara tatu kwa siku..chakula, maji vibadilishwe kila mara ili wasipate magonjwa ya kuharisha.

Bei ni 10000 kwa kuku mmoja na nawauza wote wapo 76. Laki 7 na elfu 60. ARUSHA

20231017_134949980.jpg
 
Bei imechangamka, bei imeweka pozi yaani bei imekunywa bia
Gharama za utunzaji wake ndio zinafanya wawe na bei pia. Jogoo akiwa na miezi mi5 anauzwa 25 hadi 30k.
Mtetea anataga kwa mwaka na nusu mfululizo. Na akishamaliza kutaga unamuuza kama nyama 15k. Hawatamii. Anataga pekee. Ila mayai yake unaweza kutotolesha kwa incubator. Kuku chotara ni ghali.saso au tanbro. Au aina yoyote ile
 
Back
Top Bottom