Ufugaji wa Kuku wa kisasa (Layers)

UZI HUU UTAKUWA UPDATED KWA KILA HATUA NITAKAYOPITIA KAMA MFUGAJI. KARIBUNI.

. banda la layers linashauriwa kujengwa kwa kupandisha tofali 2 then chicken wire mpaka juu.

Mkuu hongera sana. Ila huu ujenzi ni kwa maeneo ya joto. Ukifanya hivi Mbeya watakufa wote.
 
HP1 sawa kwa wale wa maeneo ya baridi wanaweza zingatia hapo. Ila kwenye joto ni muhimu sana kuacha nafasi ya hewa ya kutosha.
 
Last edited by a moderator:
kuna kuku nawauza wako kama 90 ni wa mayai nilianza kuwafuga mwaka jana mwezi wa 6 na walianza kutaga mwezi wa 12 mwaka jana, sababu ya kuuza ni kukosa usimamizi bora hivyo mradi una jiendesha kwa hasara wapo kibamba kwa mangi kwa anae hitaji please! bei mmoja 12,000/-
 
Mkuu.. muda si mrefu nataka nianze mradi wa kufuga kuku wa kienyeji... nisaidie kujua ni vitu gani natakiwa kuvitilia maanani ili kufanikiwa ?.... sina idea yoyote. muhinda
 
Last edited by a moderator:
Muhinda asante kwa uzi huu mzuri, hivi tray ya mayai bei ya jumla kwa sasa ni sh ngapi?

Bei bado haijatulia vizuri. Ila Tunauza mpaka 6000. Kuna wengine wanasema soko limeanza kusumbua tena so huenda yakashuka tena bei. Kuna mayai yanaingizwa toka nje ya nchi kinyemela ndio maana.
 
Mkuu.. muda si mrefu nataka nianze mradi wa kufuga kuku wa kienyeji... nisaidie kujua ni vitu gani natakiwa kuvitilia maanani ili kufanikiwa ?.... sina idea yoyote. muhinda

Kwa kweli sina uzoefu na kuku wa kienyeji. Mi nafuga wa kisasa.
 
Last edited by a moderator:
Asante kwa feedback, Mi nina mpango wa kuanza na broilers 100 then 300 kama kujifunza hivi kisha ntafuga layers nikipata experience.
 
UZI HUU UTAKUWA UPDATED KWA KILA HATUA NITAKAYOPITIA KAMA MFUGAJI. KARIBUNI.

UPDATE 20TH FEB 2015

Habari za masiku wadau na heri ya mwaka mpya.
Napenda kuwaletea mrejesho kama nilivyoahidi.

Kwakweli changamoto nimekumbana nazo nyingi sana. Kama sio roho ngumu ningeacha kufuga.

Kuku wangu wana week 40 sasa na walianza kutaga at 18 weeks exactly.

Changamoto ya 1 ni magonjwa. Kuku wangu wameugua sana typhoid na mafua. So far wameshakufa over 100 layers.
Kitu nilichokosea ni kutowachanja typhoid na mafua. Sababu nilishauriwa kuwa typhoid is not common na kama wakipata inatibika. Kumbe wapi typhoid inatibika lakini inatabia ya kujirudia.

2. Joto pia liliua sana kuku. Kutokana kwamba niliwaweka juu sana karibu na bati. Sasa ivi nimewashusha na mambo yanaenda vizuri.

3. Soko la mayai lilisumbua sana. Wakati kuku walianza kutaga mwezi wa 10 bei ya mayai ilishuka sana na hata kuuza ilikuwa shida. Hapa watu waliuza sana kuku. Kwakweli nilipambana kufa na kupona nikafaulu kupata walau chakula cha kuku. At this point walikuwa wanakula 80, 000 per day. Iyo ni chakula tu. Mwezi wa kwanza soko lika improve ndio kidogo kafaida nikakaona.

So far napata tray 22 -25 per day. Faida kwa mwezi napata angalau 1.5m. Na hapa kuku wamekufa sana.

Nilichojifunza ni kwamba next time ntachukua mbegu tofauti. Maana inaelekea hawa nilionao either parent stock yao ilikuwa na matyphoid au ni mbegu tu ndio dhaifu kwa magonjwa.
Always hakikisha kuku wako wanapata chanjo zote. Utaserve hela nyingi sana kwenye madawa.

Nakaribisha maswali
------------------------

Mimi ni mdau mpya katika fani ya ufugaji. Baada ya kufanya utafiti kwa mda mrefu kupitia hapa JF na kwa wafugaji wazoefu nimeamua kuanza na kuku wa mayai yaani layers.

Kwanza kabisa nilianza kujenga banda kwa kufuata maelekezo ya wataalamu. yaani layers wanahitaji ventilation ya kutosha. banda la layers linashauriwa kujengwa kwa kupandisha tofali 2 then chicken wire mpaka juu. inashauriwa squire metre 1 kwa layers 5.

sasa basi mi nimeanza na layers 1000. ivi ninavyoandika wamefikisha siku ya nne. kwakweli nashukuru Mungu so far wanaendelea vizuri na wamechangamka fresh tu.

Siku ya kwanza walipofika, niliwafikishia kwenye banda ambalo nililiandaa kwa kuweka chokaa kwenye sakafu, then maranda ambayo yamekauka vizuri na kuchujwa vumbi, juu ya maranda nilitandika magazeti. juu ya magazeti nilimwaga glucose ambayo walikuwa wakiidonoa wakati nawaandalia maji.

pia niliweka majiko special ya mkaa kwa ajili ya kuwapatia joto la kutosha, kwa kiasi fulani na banda nimelizibaziba mpaka watakapofikisha week mbili ndio niwafungulie.

pili nikawakorogea glucose gm 100 kwa lt 10 za maji ya uvuguvugu (hii unawapa bila chakula). maji ya uvuguvugu yanasaidia kulainisha utumbo wao kabla ya kuwapatia chakula kwa mara ya kwanza. baada ya masaa mawili niliwabadilishia maji na kuwawekea maji yenye vitamin na dawa kukausha vitovu, hapa niliwapa na chakula.

Dawa ya vitovu(Aliseril) watakunywa for 5 to7 days.

hapo ndio nilipofikia tutaendelea kujulishana kadiri wanavyoendelea.

03/06/14 - Leo ni siku ya tano na vimeshakufa 3. Nimemconsult dr. Akaniambia ni tatizo la vitovu. Amenitoa hofu kwa kusema vifo kwa vifanga kwa idadi mpaka 10 kwa week ya kwanza ni vitu vya kawaida mradi isiwe rate ya kutisha. Despite all that vifaranga wanaendelea vizuri.

Jana tarehe 6/06/14 ambayo ilikuwa siku ya saba, nimewapa chanjo ya new castle ambayo procedure zake, niliwanyima maji for 2 hrs kabla ya kuwapa chanjo. lazima maji yachemshwe alafu yapoe. Then ktk lt 20 nilishauriwa kuweka vijiko 14 vya chakula vya maziwa ya unga baada ya nusu saa ndio unachanganya maji hayo na chanjo. Nikawapa kwa mda Wa masaa2.

vifaranga vyangu vimetimiziza week 3 sasa. samahani siku update kwa mda kidogo, nilibanwa kidogo.
nilichojifunza kwenye chanjo ya kwanza kuku walidonoana sana. niliita mtaalamu akanieleza ni sababu ya stress ya kuwanyima maji for 2 hrs. alishauri next time niwanyime for 1 hr inatosha. nilifanya ivyo kwenye chanjo ya Gomboro na tatizo la kudonoana likatoweka. procedure za kuchanja Gomboro ni kama nilivyofanya kwenye New castle.

siku ya 18 nilishauriwa niwachanje MAREX. huu ni ugonjwa unawapataga layers pale wanapoanza kutaga na ivyo kushindwa kutaga.. kwa kawaida wanatakiwa kupata hii chanjo na anayekuuzia. lakini kutokana na uaminifu mdogo wa baadhi ya makampuni inabidi kutake pre caution. hii wanachanjwa na Dr. kwa kuchomwa sindano ya shingoni.

Nimerudia chanjo ya new castle siku ya 21, procedure ni zilezile.. vifaranga vinakua vizuri. tuendelee kuelimishana.


Layers DOC TZS 2200
Broiler DOC TZS 1400
Vijogoo (Male Layers-ISA) TZS 400

Contant me:0717332652
 
Naomba kuelimishwa. Kwa nini bei ya vijogoo inakuwa ndogo sana ukilinganisha na broiler?

Vijogoo ni by product,alafu cost ya kuvikuza ni ghali zaidi ya broiler,vinakula sanaa,na mpaka kuuzwa it's almost miezi 4 na nusu.Though it's more profitable than broiler
 
Vijogoo ni by product,alafu cost ya kuvikuza ni ghali zaidi ya broiler,vinakula sanaa,na mpaka kuuzwa it's almost miezi 4 na nusu.Though it's more profitable than broiler

Vijogoo vikikua vinauwezo wa kupanda matetea na kupata mayai?
 
Wewe ni jembe, kula "like". Una-inspire na wengine,
Swali langu ngoja nikimbilie moja kwa moja kwenye faida ulosema,
1. hiyo 1.5 ni faida baada ya kutoa gharama zote, chakula, dawa, kijana wa kazi n.k, yaani ndo pesa unayoiingiza wewe mfukoni wewe mwenyewe??
2. Ulianza na mtaji wa shilingi ngapi?
3. Soko la mayai unalipataje?
4. Je umefikiria pia ufugaji wa broilers? Una kauzoefu/ au ujuzi kidogo na hii?? Na pia kama mtu ambaye unafanya ufugaji, nina uhakika una wasiliana na wafugaji wengine wa poultry, kati ya layers na broilers ni ipi nzuri zaidi kuanza nayo kabla ya kuikuza biashara hapo baadae??
ASANTE!
 
Wewe ni jembe, kula "like". Una-inspire na wengine,
Swali langu ngoja nikimbilie moja kwa moja kwenye faida ulosema,
1. hiyo 1.5 ni faida baada ya kutoa gharama zote, chakula, dawa, kijana wa kazi n.k, yaani ndo pesa unayoiingiza wewe mfukoni wewe mwenyewe??
2. Ulianza na mtaji wa shilingi ngapi?
3. Soko la mayai unalipataje?
4. Je umefikiria pia ufugaji wa broilers? Una kauzoefu/ au ujuzi kidogo na hii?? Na pia kama mtu ambaye unafanya ufugaji, nina uhakika una wasiliana na wafugaji wengine wa poultry, kati ya layers na broilers ni ipi nzuri zaidi kuanza nayo kabla ya kuikuza biashara hapo baadae??
ASANTE!

1. Iyo 1.5 ni faida baada ya kutoa costs zote hii nabaki nayo mfukoni.

2. About 20m pamoja na ujenzi wa banda

3. Soko la mayai linasumbua. Ivi nnavyotype mayai yameshuka tena bei. So nauza from 5500 to 6000. Wazoefu wanasema huwa inatokea na kupita. Soko langu nimejaribu kuy arget sehemu tofautitofauti. Kuna mengine nawauzia wale wa bicycle ila hawa ni walaliaji lakini ni muhim kuwa naona as wanachukua mayai ya kuyosha. Megine napeleka mwenyewe madukani. Hawa ni wazuri kwenye bei as there is no middle man involved

4. Sina uzoefu na broilers as nilianza moja kwa moja na layers. Ila wengi hushauri uanze na broilers upate uzoefu kwanza. Mimi nilijituma mzimamzima which is risky but I believe in taking big risks.
 
kuna kuku nawauza wako kama 90 ni wa mayai nilianza kuwafuga mwaka jana mwezi wa 6 na walianza kutaga mwezi wa 12 mwaka jana, sababu ya kuuza ni kukosa usimamizi bora hivyo mradi una jiendesha kwa hasara wapo kibamba kwa mangi kwa anae hitaji please! Bei mmoja 12,000/-
je katika hao kuku 90 unapata mayai mangapi kwa siku au wanataga kwa % ngapi? Je nikiwatoa sehemu ya joto na kuwapeleka njombe sehemu ya baridi haitaathiri utagaji wao? Nawahitaji sana lakini nina wasiwasi
 

Similar Discussions

6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom