Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

nifahamishenin vizuri basi mbona kama hamutaki kunipa information za kutosheleza
Kutotolesha viranga wa kuku wa kisasa unahitaji kuwa na parent stock (kuku wanaozalisha mayai ya kutotolesha)

Kwa ufahamu tu ni kwamba mayai haya ya kuku wa kisasa yanayotumika kwa chakula sio yanayotumika kuzalisha vifaranga, sababu hayana mbegu (unfertilized eggs) hivyo hayawezi kutumika kupata vifaranga

Kuku wa kisasa wamefanyiwa genetic modifications, ni suala gumu kidogo kuelewa kama hujui chochote kuhusu hawa kuku, lakini kwa ufupi ni kuwa kuna parent stock ya kuku ambao mayai yao ndio yanatumika kuzalisha hawa broiler unaoona mitaani.

Hao parent stock ni sensitive breed na wanahitaji matunzo maalum na chakula maalum na wala hakuna mfugaji anaweza kuwa nao nyumbani maana hata hawazaliani kama walivyo kuku hawa wa kawaida.

Hata viwanda vyenye hizi parent stocks huwa wanaagiza hao kuku wazazi toka ulaya wanawakuza mpaka wanapoanza kutaga ndio wanatumia mayai yao kuzalisha broilers

Good night
 
Tufuge wa kienyeji best na madawa yao ya kienyeji, naamini ni rahisi kuwafuga

Ndio ninachofanya now je hawa kuloiler wanaweza kufugwa kienyeji na kuwapa madawa ya kienyeji pia??me hizo chanjo zao za kizungu siziamini kabisaaa hata kidogo...
 
Habari wadau wa JamiiForums,

Ningependa kuwashirkisha wajasariamali wenzangu na wawekezaji wa ndani kua ufugaji wa kisasa wa kuku wa mayai ni biashara yenye faida nzuri endapo utampata mtu mwenye dhamira na ufugaji kuku.

Hivyo basi ombi langu kubwa natafuta mwekezaji ambaye tunaweza wekeza kwenye ardhi yangu iliopo mwanza Kigongo Ferry eneo lina ukubwa wa acre moja ni zuri na lenye usalama wa hali ya juu maitaji makubwa na kwenye miundo mbinu itakayo tuwezesha kufanikisha uzalishaji wa hali ya juu.

Kwa yeyote alieona fursa hii na kua na uwezo na imani nayo anitafute kwa namba 0688644047. Kwa details nyingizaidi za ku boost uaminifu baina yetu.
 
Habari wadau wa JamiiForums,

Ningependa kuwashirkisha wajasariamali wenzangu na wawekezaji wa ndani kua ufugaji wa kisasa wa kuku wa mayai ni biashara yenye faida nzuri endapo utampata mtu mwenye dhamira na ufugaji kuku.

Hivyo basi ombi langu kubwa natafuta mwekezaji ambaye tunaweza wekeza kwenye ardhi yangu iliopo mwanza Kigongo Ferry eneo lina ukubwa wa acre moja ni zuri na lenye usalama wa hali ya juu maitaji makubwa na kwenye miundo mbinu itakayo tuwezesha kufanikisha uzalishaji wa hali ya juu.

Kwa yeyote alieona fursa hii na kua na uwezo na imani nayo anitafute kwa namba 0688644047. Kwa details nyingizaidi za ku boost uaminifu baina yetu.
Weka detail zaidi mkuu, Mahitaji ni nn na uzalishaji utakuaje. mtaji wa kuanzia unahitajika sh ngapi n.k
 
Pata kuku wataamu kabisa kujiramba mwanzo mwisho
( *Wakienyeji* ) wakubwa wa kutoshaaa 20, 000tsh @1..

*_oda ya kuanzia Kuku 7 unapata punguzo_ ...*
* _Popote ulip0 dar unaletewa..*_
 
Pata kuku wataamu kabisa kujiramba mwanzo mwisho <br />( *Wakienyeji* ) wakubwa wa kutoshaaa 20, 000tsh @1..<br /><br /> *_oda ya kuanzia Kuku 7 unapata punguzo_ ...*<br /> * _Popote ulip0 dar unaletewa..*_
 
Ndio ninachofanya now je hawa kuloiler wanaweza kufugwa kienyeji na kuwapa madawa ya kienyeji pia??me hizo chanjo zao za kizungu siziamini kabisaaa hata kidogo...
Ni madawa yapi ya kienyeji unayowapa?

Tufunze na sisi
 
Usikate tamaa mkuu, mwenyewe nilipeleka mayai 60 ya kienyeji pure kutotolesha vikatoka vifaranga 45, msala ukaja kuvilea vikaanza kuumwa vinatoka kama vidonda(damu) sehemu ya haja, karibu kila siku naokota kimoja walinambia nitumie esb3 lakini hola, vina wiki mbili saizi lakini vimeshakufa sita tayari, sijui kesho nitaokota vingapi
Mkuu totolesha chotara,wanavumilia sana
 
Pata kuku wataamu kabisa kujiramba mwanzo mwisho( *Wakienyeji* ) wakubwa wa kutoshaaa 20, 000@ oda ya kuanzia Kuku 7 unapata punguzo_ .Popote ulip0 dar unaletewa.
 
Leo niuzungumzie ugonjwa wa mafua(Infectious coryza)

Mafua ni ugonjwa mojawapo unaoshambulia mfumo wa upumuaji wenye tabia ya kumfanya kuku kutoa kamasi puani,kupiga chafya,kichwa kujaa maji na kuvimba.Ugonjwa huu huwaathiri kuku,bata mzinga na kanga.
Mafua ni ugonjwa unaowapata jamii ya ndege wa umri wote lakini zaidi ni kwa wakubwa.Ueneaji wake ni kwa njia ya hewa na chanzo chake ni ndege wanaougua au waliougua.

KISABABISHI
Mafua ya kuku husabibwa na Kimelea(Bacteria) kiitwacho Haemophilus paragallinum

DALILI ZA MAFUA
Dalili za mafua huanza kuonekana kuanzia siku ya 3-10 toka kuambukizwa.Sehemu zinazodhihirika zaidi ni pua,macho,mapafu,koo na koromeo.
  1. Kuku kuzubaa na kuto makamasi wakati mwingine yenye damu.
  2. Kubadilika rangi ya mapanga(Comb and wattle) na kuwa ya rangi ya bluu
  3. Huvimba macho,hali inayosabababisha kuku kuziba jicho moja na wakati mwingine yote mawili
  4. Kuvimba mapanga na uso
  5. kukosa hamu ya kula na kupunguza utagaji
  6. Kuku kukoroma wakati wa kupumua
  7. Kuhara uharo wenye harufu mbaya hasa kama kuna maambukizi mengine ya vimelea
  8. Vifo ni vichache na kuku hupona baada ya wiki

NAMNA YA KUZUIA
  • Usafi wa mazingira na kuhakikisha hakuna vimelea wanaosababisha ugonjwa huu
  • Kuku wagonjwa watengwe mbali na kuku wazima
  • Hakikisha vifaranga wanaagizwa kutoka kwenye makampuni yanayofuata kanuni bora za ufugaji
TIBA
Mafua ni ugonjwa unaotibika,mfugaji unaweza kumwona afisa mifugo aliye karibu nawe ili akuandikie dawa sahihi ya kutumia.
Nashukuru Mkuu umelenge penyewe kuku wangu wanasumbuliwa na mafuwa na sasa yanatoka damu.Naomba unitajie dawa kama hutojali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom