UFM ya Azam Media tafadhali naomba Jina la huyo Mama aliyesema Kauli hii ya Kishujaa niliyoipenda ili nimpe Zawadi ya Mbuzi Jike

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,694
109,128
"Mwanamke mwenye Maadili na mwenye Kujitambua ukipigwa na Mumeo hutakiwi Kutangaza kwa Majirani au hata kwenda Kushtaki Kwenu au Ukweni bali unavumilia na unamsubiria Mumeo Hasira zikipungua unamuomba Radhi hata kama unajua kabisa kuwa Mkosaji ni Yeye kwani kwa kufanya hivi utamjengea Kitu Mumeo Moyoni mwake, atabadilika na utashangaa ataanza Kukupenda, Kukusikiliza hadi Watu wataanza kusema kuwa Umemroga" amesema Mwanamke akiongea na UFM ya Azam Media.

Kama GENTAMYCINE nasomwa na Marais Wastaafu (Kikwete) na Aliyeko (Samia) na Waandamizi Wengine mbalimbali mpaka Sekta (Idara) Muhimu (Nyeti) nchini sidhani kama Watu wa Azam Media (na UFM Radio) hamnisomi hivyo basi naomba Ushirkiano wenu mnipe Jina la huyo Mwanamke ili nimtafute na nimzawadie Mbuzi wangu ambaye ataamua amfuge au asubirie Sherehe za Idi au Pasaka amchinje ale.

Na baada ya Kuvutiwa na hili hivi sasa nami GENTAMYCINE namtafuta Mwanamke wangu Mmoja kisha namtafutia Kosa (Sababu) ya Makusudi ili anikere nimzabue / nimfumue kidogo tu ili nione ataufuata huu Ushauri wa huyu Mwanamke Mwerevu niliyempenda wa UFM au ataamua kwenda Kunishtaki Polisi ili niwekwe rumande hata kwa Siku moja ning'atwe vizuri na Mbu na niwe katika Ratiba ya Kusafisha Maliwato za Selo.
 
Kwahiyo mtani unawaza kutafuta wa kumbutua makofi ili uone uvumilivu wake? Haya kachukue wanyoramba wakulishe mlenda kila siku au ukachukue waha ulishwe mawese au wahaya wakupikie ugali na senene ili upate sababu ya kuwabutua
 
Kwahiyo mtani unawaza kutafuta wa kumbutua makofi ili uone uvumilivu wake? Haya kachukue wanyoramba wakulishe mlenda kila siku au ukachukue waha ulishwe mawese au wahaya wakupikie ugali na senene ili upate sababu ya kuwabutua
Mtani bhana, huwa nacheka sana nikiona post yako na kama Mtani wako wa Kizanaki ( kutoka Mkoani Mara ) Nimefurahi kujua Wewe ni miongoni mwa Watani zangu Washamba Washamba Wabaya, Wanyiramba, Waha, Wanyaturu, Warangi, Wakerewe na Wanyamwezi.
 
😂😂😂 ila shemji kazi anayo, nadhani atakuwa uwanja wa majaribio.
Nikimpata naanza kumuuliza kwanini alikuwa hapatikani Hewani najua atanijibu hovyo / nyodo kwakuwa ni Mzaramo Mixa Mkwere ( taabu tupu ) na hapo ndipo nami nitapata sababu / chanzo Kuntu / Jadidi cha Kumzibua / Kumfumuo huko kwa Makusudi ili nione atavumilia au atanipeleka Polisi.
 
Mkuu umesahau kuwa huu mwezi ni wa wanawake, sasa ukimzabatua mkeo makofu hujui kuwa utajikuta pabaya? Wanawake wa siku hizi hawapigwi
 
Back
Top Bottom