Ufisadi Wa Mwakyembe na Eng. Madeni Kipande !

Ufisadi Wa Mwakyembe na Eng. Madeni Kipande !

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2009
Posts
3,444
Reaction score
265
Serikali ya CCM imejawa na uozo kila sehemu. Ufisadi na kulindana. Badala ya kufuata maagizo (mapendekezo) ya Bodi ya Wakurugenzi dhidi ya Mkurugenzi mkuu wa Bandarai TPA, Waziri husika, Prof. Mwakyembe alivunja Bodi ya TPA ili kumlinda Ndg. Madeni Kipande dhidi ya tuhuma mbali mbali zilizomkabili zikiwemo.

1. Kutokutekeleza maagizo ya bodi ya wakurugenzi
2. Jinsi alivyoendesha uajiri wa viongozi wa juu kinyume cha maagizo ya bodi
3. Ubaguzi dhidi ya wafanyakazi, watu wa makabila tofauti. Chuki na wana CHADEMA
4. Sexual harassment. Huyu Mkurugenzi amewasumbua sana wanawake wengi. Asipokubali kulalwa, anafukuzwa au kupewa wakati mgumu ndani ya TPA.
5.
Kuingia kwenye mikataba bila kufuata taratibu hasa kwenye swala la e-CTN. Alikataa ushauri kutoka kwa wanasheria, etc…
6.
Kuchelewesha utekelezaji wa "Big Results Now"
7.
Kumdanganya Waziri. Eng. Kipande alimdanganya waziri kwamba bandari ya Dar. Imeongeza makusanyo yake kutoka Tsh. 28Billion to 50.billion. Ila imekuja kugundulika kwamba mapato yaliongezeka kutoka 24billion to 42billion
8.
Kutokuheshima sheria za ajira. This can be witnessed by his action of directing that the positions of Director of Marketing, and the Director of Procurement and Supplies be advertised only because they have applied for the position of the Director General of TPA.
9.
Shutuma za kijinga dhidi ya bodi ya wakurugenzi. He has alleged some/many of the Board Directors to be CHADEMA or Members of the Opposition, Spreading information to the Media, Incompetent in what they are doing, Wachagga, Wana Udini, etc. 10. Kiburi na jeuri.. Eng. Kipande used disrespectful language against individual Board Directors, such as "Hamnitishi Kitu", "Mna nini kunizidi mimi nyie" "Hamna lolote", etc.

Mapendekezo
Mr. Chairman,
Having said all the above and based on the facts, evidence, and examples I have presented, I would like to end by proposing resolutions to be adopted by your Board in this meeting. Mr. Chairman, I propose that, the Board of Directors of Tanzania Ports Authority resolves to: · Suspend with immediate effect, Eng. Madeni Kipande, the Acting Director General of TPA to allow for further investigations on the above and other matters related to his conduct and behavior since he joined TPA. · Commission an independent investigation on the conduct and behavior of Eng. Madeni Kipande so that the Board can take appropriate measures thereafter. Mr. Chairman, I thank you all for your attention and I beg to submit my motion for deliberation and decision.

NB: Repoti inayofuata inatisha. Soma kwa wakati wako na Uamue kama CCM inafaa kubaki madarakani. Wanawake waokolewe makazini kutoka midomoni mwa manhayang'au waolindwa na watawala kama E.g.Kipande......Tutaendelea kuwaletea ripoti mbali mbali taratibu. Kama unayo ya siri tuna, kupitia barua pepe hapo chini. Jina lako daima litakuwa siri. Badala ya kumtumia Zitto Kabwe kuleta migogoro Chadema, CCM ingefanya busara kushugulikia matatizo kama haya
 
Wana JF vipenzi wa mwakyembe hawatakuelewa hata uwape documents za aina gani isipokuwa hadi pale watakapolazimishwa kunywa maji ya ku-neutralize yale maji ya ziwa kyela waliyokunywa awali. Mwakyembe ni Mungu wao hata akitembea uchi barabarani watamsujudia tu. Utaniambia!
 
Mh I know one of the mentioned ladies, na ubwete wa wanawake wote tena wengine wanajiombea wenyewe huyu mtu bila shaka amepitwa na wakati otherwise yuko possessed na mapepo ya ngono
 
Duh, mkuu, hebu tujuze vizuri, hiyo Motion imeletwa / ililetwa na Board Member??
 
Ni kweli kwamba Mr Kipande ameoa kwa Mzee JK yaani ni shemeji yake na Ridhiwan na kama unataka kazi lazima Ridhiwan kwanza akubali?
 
Hii habari ni tamu na ni sensitive inahitaji muda,ngoja nipige pige kibarua then i will be back.
 
Taasisi karibu zote za serikali kama TANESCO,MSD,SUMATRA,TRA,TPA wakurugenzi wana act Rais hajaona mbadala au yupo busy na safari
 
Hebu sasa jaribu kufanyia kazi mazuri yote waliyowahi kuyafanya hapo TPA ili tuweze kuamini kuwa the motive behind this serious and important investigation siyo conflict ya madaraka.
 
Wana JF vipenzi wa mwakyembe hawatakuelewa hata uwape documents za aina gani isipokuwa hadi pale watakapolazimishwa kunywa maji ya ku-neutralize yale maji ya ziwa kyela waliyokunywa awali. Mwakyembe ni Mungu wao hata akitembea uchi barabarani watamsujudia tu. Utaniambia!
Mtoa mada mwenyewe unasema mapato yameongezeka toka 24 hadi 42 billion. Kwani hiyo achievement ni ndogo? Huyo anayemwaga sumu kwa mwakyembe anaweza kueleza hizo billioni 18 zilikua ziko wapi? Ufisadi unapokithiri wanaofaidika wakikurupushwa wanapagawa na kuona wanahujumiwa. Heri ya mwakyembe aliyeongeza mapato ya bandari kwa bil 18 kwa mwezi.
 
Hao wanawake wote walikuja kukulalamikia wewe kuwa wametongozwa na Kipande au uliamua kufanya utafiti wako mwenyewe, kwa haraka naona hapa kuna wivu wa kike na kuzibwa kwa mirija ya ulaji TPA, ambapo kwa muda mrefu wachache walikuwa wakijinufaisha huku wengi tukiangamia. Nahisi umetumwa na mafisadi waliotimuliwa TPA, ambao walikuwa wakikusanya fedha cash na kuzisweka kwenye viroba badala ya wafanyabiashara kulipia benki kama ilivyo sasa. Watanzania hawana njema bt hii nchi ili iweze kwenda mbele UDIKTETA LAZIMA, vinginevyo tukiwasikiliza wazushi wachache tutaangamia eti.. kwa kutafuta kuungwa mkono umeihusisha CDM ili wadau wakasirike, acha hizo watanzania nowdays tuna akili timamu...shame one u.
 
Majungu tu hayo fanyakazi acha umbea.

Lisemwalo lipo...

Uonevu wa kijinsia,ubaguzi wa kikanda na vitisho ni dalili za utendaji mbove usiohitaji kukosolewa. Mwakyembe (Dr) sio malaika anaweza fanya makosa, na muungwana siku zote hutamthimini makosa yake na kuyasahihisha...!

Lakini kwa kuwa watanzania tumekuwa watu wa kuongea bila vitendo, tuliowapa madaraka watatutendea ndivyo sivyo mpaka tutakapo amka toka dimbwi la ujinga na uoga usio na maana na kuchuka hatua stahiki dhidi ya hizi dhuluma.
 
NB: Repoti inayofuata inatisha. Soma kwa wakati wako na Uamue kama CCM inafaa kubaki madarakani. Wanawake waokolewe makazini kutoka midomoni mwa manhayang'au waolindwa na watawala kama E.g.Kipande......Tutaendelea kuwaletea ripoti mbali mbali taratibu. Kama unayo ya siri tuna, kupitia barua pepe hapo chini. Jina lako daima litakuwa siri. Badala ya kumtumia Zitto Kabwe kuleta migogoro Chadema, CCM ingefanya busara kushugulikia matatizo kama haya

Wewe ni wale wale waathirika wa mageuzi ndani ya TPA.

Jenga hoja na katika hoja wanaJf watatambua mbivu na mbichi. Unapoanza kutafuta sympathy kwenye jamii kwa kuigusa kwa jambo ambalo halipo kwenye msingi wa hoja yako ni kuonyesha kuwa hata wewe unafahamu kuwa huna hoja.

Sasa huyu Zitto anaingiaje kwenye hoja yako?. Una ushahidi gani kuwa CCM tunamtumia Zitto kuleta migogoro CHADEMA na kama CHADEMA mnafahamu hivyo, kwani hakuna taratibu na sheria ndani ya katiba yenu kuhusu usaliti?.

Matatizo ya CHADEMA msiyafiche kwa kutumia hoja na jina la CCM. Kama mnafahamu tatizo ni CCM, kwa nini sasa msilitatue?. Kushindwa kutatua tatizo wakati unafahamu chanzo chake ni namby-pamby. Ya watanzania wote ndiyo mtayaweza kama siyo kuja na majungu kama haya uliyoleta hapa Jf.
 
Ila hii ya kuwataja hao akina mama hapo umeuwa bendi;

Wengine waume zao wako huku huku jf jamani tuwe walau na
staha kidogo;
 
tafadhali futa kauli yako mwakyembe ni prof. kuanzia lini,acha kucheza na taaluma za watu futa kwanza hiyo ndo turudi hapa jukwaani kujadili juu ya hii inshu nyingine
 
tafadhali futa kauli yako mwakyembe ni prof. kuanzia lini,acha kucheza na taaluma za watu futa kwanza hiyo ndo turudi hapa jukwaani kujadili juu ya hii inshu nyingine

Una wazimu nini? Aombwe msamaha kwa lipi?
Ni yeye , badala ya kumfukuza huyo MD, matokeo yake akalivunja bodi la wakurugenzi. Aibu kwake
 
Back
Top Bottom