Ufisadi wa Murza Oil ni hatari kwa Maisha ya WaTZ

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Nimepita madukani sasa hivi kununua sabuni ya unga ya kufulia. Baada ya soko huria viwanda vingi vya sabauni vilianzishwa baadhi ni Foma (Tanga), Tesa (IPP/Mengi), na Murzah.

Hivi karibuni Murzah Oil wamevinunua viwanda vya Tesa na Foma na kuua ushinda katika sokop la sabuni za unga nchini. Nimeshtushwa sana na bei za sabuni za unga tofauti na mwaka jana ambapo nilinunua Foma ya Kg 15 kwa shs 15,000/- kutokana na ushindani w bei kati ya viwanda vya sabuni. Baada ya Murza kuvinunu viwanda vya Tesa na Foma hakuna ushindani wa bei sabuni zote hizo Foma, Tesa, na Murzah zinauzwa Shilingi 29,000/- kwa kg 15! Yaani sabuni zote bei moja.

Hivi hakuna sheria za kuongoza ushindani jamani; huyu Muhindi: Murzah anatumaliza, kanunua viuwanda vya Mengi (Tesa) na Sumaria (Foma)
na sasa bei haikamatiki yaani sekta ya viwanda vya sabuni za unga imeshikwa na Fisadi mmoja (Murzah Oil). Yaani kweli sisi ni shamba la bibi!

Nakumbuka msemo wa hayati John Nollan aliyesema Tanzania ni nchi pekee dunia ambayo unaingia askini na kutoka tajhiri!

Wizara ya Viwanda na CTI lazima wafanye kitu huyu Murza kila siku anapandisha bei za sabuni kadiri atakavyo na hakuna wa kumbabaisha, siku akigoma kuzalisha sabuni basi Tanzania yoote ni uchafu mtuppu.
 
Hivi si tuna fair competition commission wanafanya nini au hizi business purchases and merger zao hazihitaji ruhusa kutoka kwenye hii tume?
 
Nimepita madukani sasa hivi kununua sabuni ya unga ya kufulia. Baada ya soko huria viwanda vingi vya sabauni vilianzishwa baadhi ni Foma (Tanga), Tesa (IPP/Mengi), na Murzah.

Hivi karibuni Murzah Oil wamevinunua viwanda vya Tesa na Foma na kuua ushinda katika sokop la sabuni za unga nchini. Nimeshtushwa sana na bei za sabuni za unga tofauti na mwaka jana ambapo nilinunua Foma ya Kg 15 kwa shs 15,000/- kutokana na ushindani w bei kati ya viwanda vya sabuni. Baada ya Murza kuvinunu viwanda vya Tesa na Foma hakuna ushindani wa bei sabuni zote hizo Foma, Tesa, na Murzah zinauzwa Shilingi 29,000/- kwa kg 15! Yaani sabuni zote bei moja.

Hivi hakuna sheria za kuongoza ushindani jamani; huyu Muhindi: Murzah anatumaliza, kanunua viuwanda vya Mengi (Tesa) na Sumaria (Foma)
na sasa bei haikamatiki yaani sekta ya viwanda vya sabuni za unga imeshikwa na Fisadi mmoja (Murzah Oil). Yaani kweli sisi ni shamba la bibi!

Nakumbuka msemo wa hayati John Nollan aliyesema Tanzania ni nchi pekee dunia ambayo unaingia askini na kutoka tajhiri!

Wizara ya Viwanda na CTI lazima wafanye kitu huyu Murza kila siku anapandisha bei za sabuni kadiri atakavyo na hakuna wa kumbabaisha, siku akigoma kuzalisha sabuni basi Tanzania yoote ni uchafu mtuppu.

Nchi nyingi sana duniani wanavitengo maalum vya "CONSUMER PROTECTION", Kazi zao kubwa ni kuhakikisha walaji wanalindwa hasa kutoka kwa makucha ya mabepari wafanyabiashara ambao kila siku wao wana target kuu mbili. Moja kupata superprofit (Maximization of profit) ambalo hufanyika kwa kuzidisha bei ya bidhaa huku wakipunguza gharama za uzalishaji ( kutumia malighafi duni na kunyonya wafanyakazi). Pili ni kuhakikisha kuwa hawapati challenge kutoka kwa wafanyabiashara wengine katika soko (Monopoly power), wanafanya hivyo kwa kuhujumu wenzao au kuwashawishi waungane na kuwa kitu kimoja kitakacho wamaliza watumiaji, au kuwakamua. Hivyo kazi ya "CONSUMER PROTECTION" ni kuhakikisha bidhaa zinakidhi viwango na kuwapa watumiaji uhuru wa kuchagua zaidi.

Bongo hawa jamaa sijui kama wapo na hata kama wapo wamelala au kwa kutokana na rushwa au kutokuwa na uelewa wa nini kifanyike maana hawajui wapo kwa ajili gani. Na hawa ndiyo adui mkubwa kuliko hata wafanyabiashara wenyewe. Serikali lazima iingilie kati katika mambo haya siyo watu kuhudhuria vikao tu na kusign "honorarium".
 
FCC wapo labda hawana "meno" ila bandarini hawabanduki, situnawaona wakikanyaga TV feki kwa kijiko.
 
FCC wapo labda hawana "meno" ila bandarini hawabanduki, situnawaona wakikanyaga TV feki kwa kijiko.

Kusema kweli hichi kitengo kipo, ofisi zake zipo Jengo la Azikiwe gorofa ya 7. Swala ni kwamba kukamata bidhaa feki ni sehemu ndogo sana ya majukumu ya Fair Competition Commission (FCC). Ntanukuu kutoka katika Sheria hio ya mwka 2003

"The key objectives of the Fair Competition Act are to:
(a) Increase efficiency in the production, distribution and supply of goods and services;
(b) Promote innovation;
(c) Maximize the efficient allocation of resources; and
(d) Protect consumers.

The overall goal of the Fair Competition Act (2003) is to enhance people's welfare and achieve a high level of economic efficiency by ensuring a level playing field in the economy."
Source: Fair Competition Commission: Home

Utaona kwamba lengo kubwa ni kuhakikisha walaji kwa ujumla wanafaidika ila pia kusaidia katika kufikia hali ya juu ya ufanisi wa uchumi. Hili la kuharibu mali za bandia ni sehemu ndogo sana ila, lina amsha hisia za jamii zaidi kwamba kazi inafanyika. Ukimwuliza mtu kazi za FCC ni zipi nadhani wengi watasema kukamata bidhaa feki. Naona Hawa jamaa wameanza kwa kufanya kile ambacho kitaonyesha wapo. Nimatumaini yangu watahamia sasa kwenye kazi halisi iliyoainishwa kwenye sheria iliyo wapa kazi.

Naamini swala hili la Muzra kununua makampuni mengine (kama ni kweli) na kujijengea 'monopoly power' ilibidi wawe wameliangalia. Kwa vile hatuna taarifa yoyote kuhusu wao kufanya hivyo haimaanishi hawaja fanya hivyo. Kabla ya kuhukumu tupate taarifa zaidi.

Nakumbuka swala ka TBL kununua kiwanda cha bia cha Kibo (Moshi) kilichokuwa chini ya East Africa breweries lilileta pia manung'uniko kuhusu afanyaji wa kazi wa FCC. La msingi ni kwamba chombo tunacho cha kuangalia haya, tena kinasheria na meno yakutosha. Sasa wahusika wafanye kazi na watuonyeshe wapo sio tu kwa kuharibu mali feki, ila kwa kuwalinda walaji na kuleta ufanisi wa juu wa uchumi

..vitu vingapi vimepanda bei kwa kasi toka mwaka jana?
..just wondering.

Hili pia ni muhimu kuangalia. Je upandaji huu wa bei ni wa kawaida au ni kutokana na nguvu hodhi za kampuni mpya na kubwa iliyonunua wengine? Ili kuweza kufikisha maoni yetu vizuri tunahitaji tufanye uchunguzi zaidi. Ikiwa kila kitu tunachopata habari tetesi ju yake tunakimbilia kuaandika bila kutafakari zaidi, ukumbi huu utapoteza mwamko wake wa kuwa sehemu ya kupata habari zilisofanyiwa kazi.
 
Asante Mzeeba kwa kutuhabarisha ni upi wajibu wa FCC. Sijui kama hiki ni kitu tofauti lakini ofisi za hawa jamaa ziko Ubungo Plaza kwa sasa. Just in case mtu anataka kwenda kuwaona!!!!!!!
 
FCC ni sehemu ya watumishi serikalini walizoea kufanya kazi kwa mazoea nadhani ndio tatizo, hawaangalii kuwa mazingira na nyakati zimebadilika.
 
Last edited:
Angalizo: Mkuu Ibrah hicho kipindi ulichonunua 15,000 inflaton ilikuwa ngapi na sasa ni ngapi? Well hoja yako ni msingi lakini........
 
Watanzania tumelala. Siku tukiamka huyu Mhindi wa Murzah atakuwa ameshapata kitita chake. Kama yule mzungu alivyoseama Tanzania unaingia mikono mitupu unatoka na briefcase ya pesa.
 
Kwa kweli kuna haja ya kuanzisha taasisi kama EWURA kwa ajili ya bidhaa zingine,Walaji ni vema walindwa kwani wafanyabiashara wanachojali wao ni faida tu.Lakini pia Watanzania kwa nini tunawaachia Wahindi washikilie uchumi wa nchi yetu kiasi hiki,watu hawa watatutesa sana kwani wanahamisha utajiri wa nchi yetu kwao.Hawana uchungu nasi wanachojali wao ni kuzinufaisha nchi zao na familia zao.Angalia ufisadi wa EPA,Richmond na zingine wanahusika wakishirikiana na Wahindi weusi.Tuwe macho kuilinda nchi yetu dhidi ya uharamia huu,mafuta yanashuka bei halafu bidhaa zingine zinapanda bei inangia akilini kweli?
 
Ni sawa ipo FCC lakini ninavyojua mimi mara nyingi katika utumishi wa umma kuna tabia ya kufanya kazi kama zimamoto.
Hii ndiyo inafanya watu watunue wanavyotaka ili ikija operation fulani aaahhh wanakuwa wadogo.
 
ebwana huyo jamaa hawezi kuwa hivyo kama hana back up, mpaka hiyo issue iwe critical keshakusanya mabilioni, halafu hata ukiangalia sabuni hizo zote hazina tofauti zilizokua nazo mwanzo, tofauti ni jina tu
 
..vitu vingapi vimepanda bei kwa kasi toka mwaka jana?

..just wondering.

DSL, ni vingi vimepanda lakini nakuhakikishia hizi sabuni za unga zimepanda bei mno tena bila hata sababu. Mimi ni mnunuzi wa bidhaa kwa bei ya jumla hivyo nazunguzmza nachokijua, Sukari haijapanda bei, Ngano almost bei ni ile ile pamoja na ngano kupanda bei duniani kutokana na kushuka kwa uzalishaji na hasa kwa nchi za Marekani na Canada.

Tembela maduka ya jumla na ulizia kuhusu bei za sabuni ya unga inayotengezezwa Taznania, unaweza kulia, waulize bei imepanda mara ngapi tangu mwazoni mwa mwaka jana.
 
Back
Top Bottom