Wacheni kumsulubu MuuzaChai,hivi kosa lake ni lipi ? Au kwa kuwa tu hali yake na umasikini wake ndio mnaoutumilia kumdharaulisha ,si kila mtu anaweza kupata source za habari na ushahidi wa maandishi ,ila hata tetesi zinatosha kabisa kuwa anachokizungumza kina ukweli flani flani,kushindwa kwake kuweka ushaidi isiwe wala isionekane kuwa hakuna tatizo ambalo amekusudia kuliwakilisha.
Kama imeamuliwa kuwa JF ni jukwaa la Jamii ,hivyo yeye kama mwanajamii anayohaki ya kuandika kile anachokiona kimetokea na huenda pengine yaliomkuta hayo aliyokusudia kuyaeleza yametokea kwa ndugu,jamaa au rafiki yake ,sasa kama kuna watu wameamua kufanya haki kwa kila mtu na wana uwezo wa kuyafuatilia mambu ,hao itakuwa jukumu lao kuzamia na kutoa yalioko huko kulikoshutumiwa.
Ila kama wengi mliomtisha na kumdharau Muuza Chai ni wa kabila la Mengi ,ni watu wa karibu na Mengi,mnafaidika na mapato ya Mengi hapo mtakuwa hamtendi wema kwa kumvurumishia maneno Muuza Chai , mnaonyesha ni watu mliojaa dharau kwaq wengine kwa kuwa tu ni masikini na hawana wa kumsikitikia na kueleza shida zao ,kama kujiunga kwa Muuza Chai hapa JF ni katika kuona kuwa JF ni sehemu ya kupeleka kilio Chake na kuona wahusika wanafuatilia malalamiko yake bila ya upendeleo ,kwa nini hutimizi wajibu wako katika kumsaidia Muuza Chai na hoja zake na kumpa kilicho na uhakika ambacho huenda hana uelewa kuliko kuzidi kumtia unyonge ,mwenyewe ametoka huko kwa furaha kuelekea JF na kujipa matumaini kuwa hata Mengi ni fisadi na kueleza kile anachokijua akitumaini haki anayoililia itapigiwa makelele hapa JF ,wacheni kulinda manyang'anyi.